Wednesday, 2 February 2011

Ulipaji fidia wa DOWANS

*Waislam wataka DOWANS walipwe haki yao
*Kafulila apingana nao

Stella Aron na Anneth Kagenda, jijini
SAKATA la ulipaji wa fidia ya Sh.bilioni 94 kwa kampuni ya DOWANS kwa kile kilichodaiwa ni kutokana na kukiuka mkataba,Taasisi ya Kutetea Haki za Waislam,imeibuka nakuishauri Serikali kuharakisha malipo hayo harakaiwezekanavyo kwani ni haki yao kisheria.

Wakati taasisi hiyo ya Imam Bukhary ikiishauri hivyo Serikali, Mbunge wa Kigoma Kusini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi, David Kafulila ameiomba Serikali itoe maelezo ya kina kuhusiana na ulipaji wa fidia hiyo.

Mwenyekiti wa taasisi ya kiislam, Sheikh Khalifa Khamis akizungumza na Dar Leo amesema kuwa, DOWANS inatakiwa ilipwe kwakuwa ina mikataba ya kisheria hivyo kitendo cha kutokulipwa ni sawa na unyanyasaji na si uungwana.

" Mikataba ipo na inaonyesha Serikali inaitambua, hivyo kwanini wasilipwe fedha zao, kwani kuvunja mkataba kwa sheria yetu ya dini ya Kiislam ni haramu kama waliandikiana mkataba walipwe hata kama ni matapeli sisi ndiyo wenye makosa,"amesema Sheikh Khamis.

Amesema kuwa, Serikali ndiyo yenye makosa kwa kuingia mkataba na kampuni hiyo bila ya kujiridhisha hivyo inapaswa kuilipa ili ijifunze siku nyingine kuingia mikataba bila kuifanyia uchunguzi wa kina.

Ameongeza kuwa, kuna baadhi ya wabunge ndiyo walioshinikiza kuvunjwa kwa mkataba huo kutokana na chuki zao binafsi hivyo kitendo hicho ndicho kinachoigharimu Serikali hivi sasa.
 

No comments:

Post a Comment