Fish

Wednesday, 30 May 2012

Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Sheria na Mawasiliano, Salim Bimani
--

THE CIVIC UNITED FRONT
      (CUF- Chama Cha Wananchi)
 

Office of the Secretary General
Party Headquarters,  P.O.  Box 3637, Zanzibar, Tanzania
E-mail:cufhabari.co.uk   Homepage: www.cuftz.org


Our Ref:      CUF/HQ/ONKM/U/003/2012/13                                     Date:                     29/05/2012
Umma unashuhudia hali tete ya machafuko ambayo hayakutarajiwa yakiibukia tena Zanzibar, wakati ambapo Nchi ilishaanza kunawiri matunda ya utulivu na maridhiano, chini ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa.

Pamoja na sababu au visingizio mbali mbali vilivyotajwa kuwa chanzo cha hali hiyo, zikiwamo za hamasa za wananchi, chuki binafsi, ukosefu wa hikma, matumizi ya nguvu za dola, na hata uchochezi wa makusudi wa wale wanaoonekana kutopendelea Maridhiano ya Kisiasa ya Zanzibar.

Kwa thamani yoyote hakuna asiyeweza kubaini umuhimu wa hali ya amani na utulivu, na madhara ya kukosekana kwake, hasa katika Visiwa hivi vya Unguja na Pemba ambavyo vimewahi kuelemezewa athari kubwa ya machafuko kwa muda mrefu.

Chama cha Wananchi,CUF, kama sehemu muhimu ya Umma wa Watanzania, hakiwezi kukaa kimya kutokana na mwelekeo mzima wa hali tete ya amani katika nchi, ingawa ni dhahiri wapo baadhi ya watu wasioitakia mema Zanzibar wakibainika kufurahia mazingira hayo, kwa maslahi binafsi, na pia kutoa kauli za kutatanisha za kisiasa.

Chama cha CUF, kinatoa wito kwa wananchi wote kuwa watulivu, wavumilivu, na kuitumia fursa ya kutoa mawazo yao bila ya jazba, pamoja na kutowanyima wengine nafasi ya kuwasilisha mitazamo yao.

Vitendo vya watu wachache kuchoma makanisa na kuharibu mali za watu ni vya uvunjifu wa sheria na kinyume na Utamaduni wa Kizanzibari; uchunguzi wa kina ufanyike na waliohusika wachukuliwe hatua za kisheria, bila uonevu wala upendeleo.

Tahadhari iwepo ya kuepuka matumizi ya mabavu yanayoweza kuleta hamasa kwa wananchi, hatimaye ikachochea vitendo vya hujuma dhidi ya watu na mali zao, na pia kuepuka tabia isiyokuwa ya haki, ya kuwabambikizia kesi wananchi.

Ni lazima kwa wakati huu, na haraka iwezekanavyo, Serikali ikazungumza na Masheikh, bila ya kuona muhali, na kwa uwazi kabisa, ili kutafuta suluhu ya kudumu, kwa faida ya Nchi na Taifa kwa Ujumla.

HAKI SAWA KWA WOTE

…………………………………….

Salim  A Bimani
Mkurugenzi wa Haki za Binaadamu, Habari na
Uenezi na Mahusiano na Umma


Hatutarudi nyuma – Sheikh Farid

Kiongozi wa Maimamu Zanzibar, Farid Hadi Ahmed akiongea na waumini katika msikiti wa Mbuyuni Zanzibar jana baada ya sala ya alaasiri

JUMUIYA ya Mihadhara ya kiislamu (Uamsho) imetoa msimamo mkali shidi ya Serikali ikisema kuwa haitarudi nyuma katika kudai uhuru wa Zanzibar.
Wakizungumza katika msikiti wa Mbuyuni uliopo eneo la Darajani mjini Zanzibar, viongozi wa Uamsho wamewataka Wazanzibari kutolegeza msimamo wao hata kama jeshi la polisi limezingira mji wao.
Umoja wetu ndiyo utakaotukombolea nchi yetu, msikubali kuyumbishwa na kitu chochoe ili kulegeza msimamo wetu. Jambo moja tu, ni mpaka kieleweke.
Bila hivyo hakuna jeshi, hakuna polisi atakaye tuyumbisha” alisema Sheikh Mussa Juma wa msikiti huo na kuitikiwa na wafuasi waliokuwa wamefurika katika msikiti huo “ndiyooooo!”
Wafuasi hao walikuwa wameshikilia karatasi zilizoandikwa “hatuutaki muungano, tunaitaka Zanzibar yetu”.
Naye Sheikh Mussa Juma aliyekuwa amekamatwa na jeshi la polisi kabla ya kuachiwa kwa dhamana aliwapongeza wanachi waliotokana kuandaana akisema kuwa hawatarudi nyuma, Tunawashukuru Wazanzibari kwa sababu mmeonyeshwa kutotaka kutawaliwa” alisema na kuwauliza wafuasi hao “mko tayari” nao wakijibu “Tuko tayariii”
Naye Sheikh Farid Hadi Ahmed alisema kuwa kundi hilo linafuata taratibu hivyo halipaswi kulaumiwa kwa kufanya vurugu. Aliwataka pia Wazanzibari kutogawanyika kwa vyama vya siasa,Muone katika silaha kubwa wanayotumia maadui ni kutugawa kivyama na kikabila au kirangi, inasikitisha sana.”
Huku akinukuu Katiba ya Zanzibar ibara ya 23 Farid alisema kuwa kila Mzanzibari anapaswa kuhifadhi mamlaka na uhuru ya Zanzibar.
Aliwahamasisha wafuasi hao kuonyesha mabango waliyokuwa wameshikilia na kumtaka mkuu wa jeshi la polisi kutambua hitaji kubwa la Wazanzibari.
Hebu mwonyesheni IGP mlichonacho….. mnautaka muungano hamuutaki? (wote wakajibu) “hatuutaki!).
Huku akitoa mifano, Farid aliendelea kusema kuwa kilichopo ni wimbi la Wazanzibari kudai nchi yao.
Alisema kuwa kama vile maji ambayo yakizibwa katika njia yake husambaa mitaani, hivyo ndivyo Wazanzibari wanavyosambaa mitaani kudai nchi yao.
Alitetea kitendo cha jumuiya hiyo kuandamana akisema kuwa si kosa kisheria kutembea barabara.
Kwani mtu akitembea kwenye nchi yake anatembea kwa kibali? Sisi tumeamua kutembea… waliokuja na wake zao wametembea na Mwenyezi Mungu kajalia tumetembea kwa furaha yote. Mbona timu zinafanya mazoezi, zinachukua vibali, watu wanakwenda hitimani wanapewa vibali?” alihoji.
Faridi alitangaza siku ya Mei 26 kuwa ni ya maandamano kwa Wazanzibari na kuwataka wanajeshi wa Kizanzibari kujiandaa kuwaunga mkono katika maandamano hayo.
Huku akikwepa lawama kwa kundi hilo kwamba limekuwa likichoma na kuharibu makanisa, Sheikh Farid aliwalaani watu wanaounganisha kundi hilo na tuhuma hizo, Tunamwambia IGP kamishina hana uwezo hana uwezo. Wanajeshi tunao…. Vikosi vina watu 8000 waambie wajiadae wasibebe silaha ni ndugu zetu… waje wakae barabarani wala sisi hatuhitaji ulinzi” alisema na kuongeza,
Lakini tuna wasi wasi na hawa wanaolipua makanisa na sisi tunawalaani vibaya, hawa tunaamini ndiyo wale wale waliokuwa wakisimama na kutukana matusi, tena wana visu, wana nondo, wana pesa Mheshimiwa IGP waambie wakupe rekodi.”alisema Farid.
Licha ya Waziri katika Ofisi ya makamu wa kwanza wa Rais Mohammed Aboud kukemea mihadhara hiyo, jeshi la polisi halikuthubutu kuingilia mkutano huo.
Magari yaliyosheheni askari polisi yalionekana yakipita mbali na eneo hilo bila kuwabughudhi.

Tuesday, 29 May 2012

VIDEO YA BAADHI YA PICHA ZA MATOKEO HAPO MICHENZANI 27/05/2012

Mhe. Spika akutana na Balozi wa Canada hapa nchini, afanya kikao na kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama

Spika wa Bunge Mhe. Anne Mkainda akimsikiliza kwa makini Balozi wa Canada hapa nchini Mhe. Robert Orr alipomtembelea ofisini kwake leo. Balozi huyo alifika Ofisini kwa Mhe. Spika kwa lengo la Kumuaga.
Mjumbe wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mhe Mohamed Seif Khatibu akifafanua jambo mbele ya Mhe. Spika wakati kamati hiyo ilipokutana na Mhe Spika kujadili maswala mbalimbali yanayohusu kamati hiyo. kulia kwa Mhe. Spika ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Edward Lowasa na baadhi ya wajumbe wa kamati hiyo.

Dk. Shein akutana na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,akizungumza na Uongozi wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, katika utekelezaji wa mpango wa kazi za Ofisi za Wizara hiyo huko Ikulu Mjini Zanzibar jana ,(kushoto) Makamo wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad.



Baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Makamo wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,wakiwa katika mkutano chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,mkutano huo unahusu masuala mbali mbali ya kiutendaji,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
 Movement For Change Ya CHADEMA Yafunika Mtwara
 Aliyekuwa Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, akihutubia katika mkutano wa hadhara waM4C, kwenye Uwanja wa Mashujaa mjini Mtwara, jana.
Sehemu ya maelfu ya wananchi wa mji wa Mtwara na vitongoji vyake, wakiwasikiliza viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), katika mkutano wa hadhara wa M4C (Movement For Change), uliofanyika kwenye Uwanja wa Mashujaa.

Ofisi ya Makamu wa Rais





Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal amekutana na Waziri wa Maendeleo wa Finland Mheshimiwa Deidi Hautala ambapo wamezungumzia masuala mbalimbali kuhusu ushirikiano na maendeleo wa nchi hizi mbili.

Katika mazungumzo hayo Dk. Bilal alimweleza Waziri huyo hatua zinazochukuliwa na serikali ya Awamu ya Nne katika kufikia dira ya Taifa ya maendeleo 2025 ikiwa ni pamoja na kutekeleza kauli mbiu ya kilimo kwanza na kuhakikisha kila mtoto anapata elimu.
Alisema katika kutekeleza kilimo kwanza, serikali inafanya jitihada ya kuhakikisha maafisa ugani wa kutosha wanapatikana ili kusaidia wakulima vijijini kujua mbinu bora za kilimo cha kisasa na namna zitakavyowawezesha kuzalisha kwa tija.
“Hata hivyo, tunajaribu kuongea na taasisi za fedha waweze kuwasaidia wakulima kwa kuwapatia mikopo kwa ajili ya kuendeleza shughuli zao,” alisema na kuongeza
“Tuna tatizo la soko kwani vijiji vingi havijaunganishwa na barabara, bado tunawapa msaada wa kutosha kuhakikisha mazao yao yanafika sokoni. Tunaamini kupitia kilimo kwanza tutawawezesha wakulima wetu kutoka kwenye kilimo cha mashamba madogo na kwenda kwenye mashamba makubwa ya biashara.”
Alipotakiwa kuzungumzia kuhusu mabadiliko ya hivi karibuni ya Baraza la Mawaziri Dk. Bilal alisema hali hiyo inatokana na serikali kutoa madaraka kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za serikali na kuruhusu Bunge kuwa huru zaidi.
Makamu wa Rais alimhakikishia Waziri huyo kuwa, wale wote watakaobainika na ubadhirifu wa mali za umma watafikishwa kwenye vyombo vya sheria na kusema kwamba serikali inatambua kuwa Mahakama ni chombo muhimu na kamwe hakuna mwenye mamlaka ya kuingilia katika kutimiza majukumu yake.
Akiwa nchini, Waziri Hautala ambaye anafuatana na ujumbe wa watu 12 anatarajia kuhudhuria mkutano wa Benki ya Maendeleo Afrika utakaofanyika mjini Arusha.
Imetolewa na 
Ofisi ya Makamu wa Rais
Dar es slaam
Mei 29, 2012
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na wa Waziri wa Maendeleo wa nchini Finland, Heidi Hautala (wa pili kushoto kwa Makamu) aliyeongozana na ujumbe wake wakati walipofika Ofisini kwake Ikulu Dar es Salaam leo asubuhi, Mei 29, 2012.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya pamoja kwa kumbukumbu na Waziri wa Maendeleo wa Finland na Ujumbe wake mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika Ofisini kwa Makamu Ikulu Dar es Salaam, leo asubuhi Mei 29, 2012.

Watu 30 wafikishwa mahakamani

Na Salma Said
Zanzibar leo hii imejikuta ikirejea kule ilipotoka baada ya matukio ya uvunjifu wa amani kujitokeza kwa mara nyengine tena ambapo wananchi na jeshi la polisi kwa pamoja wamekuwa wakifanya vitendo vya uvunjifu wa haki za binadamu. Vijana wenye hasira wamechoma moto matairi barabarani na kuharibu mali za watu lakini na Polisi nao wamekuwa wakiwakamatwa vijana hao na kuwapiga kwa marungu na mateke jambo ambalo ni kinyume na haki za binaadamu ambapo Tanzania imeridhia azimio la umoja wa mataifa la kuheshimu haki hizo.

JUMLA ya watu 30 wakiwemo wanaodaiwa kuwa viongozi wawili wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, leo walifikishwa mahakamani chini ya ulinzi mkali na kusomewa mashitaka ya uzembe, uzururaji na uvunjifu wa amani.

Shitaka jengine walilosomewa mahakamani chini ya Hakimu Mohammed Ali Mohammed Shein hapo ni pamoja na kufanya mkusanyiko usivyo halali ambapo Mbarouk Said Khalfan (45) Mkaazi wa Taveta Meli nne na Mussa Juma Issa (57) Mkaazi wa Makadara wote wakaazi wa Mjini Zanzibar.

Washtakiwa hao ambao walisomewa mashtaka matatu ikiwemo kufanya mkusanyiko isivyo halali, uzembe na ukorofi pamoja kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa aman, walifikishwa mahakamani hapo wakiwa chini ya ulinzi mkali wa askari Polisi.

Viongozi hao kwa pamoja walisomewa mashitaka ya kujikusanya na kufanya maandamano kinyume na sheria kifungu 55 (1)(2)(3)  sheria nambari 6 ya mwaka 2004. ambapo Hakimu Shein alisema mahakamani hapo kwamba mnamo Mei 26 mwaka huu majira ya saa 6:30 za  mchana viongozi hao walijikusanya kinyume na sheria za Zanzibar.

Hakimu huyo alisema wananchi hao walifanya maandamano ambayo yalianzia katika uwanja wa Lumumba kupitia Msikiti wa Biziredi na kumalizia uwanja wa Lumumba, ambalo ni kosa kwa vile linaweza kuhatarisha amani na utulivu na kuweza kusababisha
uharibifu wa mali za wananchi wa Zanzibar.

Mbali ya viongozi hao wanaodaiwa wa Uamsho wengine walijumuisha katika kesi hiyo ni Mbwana Hamadi Juma (50) Mkaazi wa Nyerere, Masoud Hamadi Mohammed (17) Mkaazi wa Mtoni Kidatu, Mohammed Juma Salum (35) Mkaazi wa Kianga na Abdulrahman Simai Khatib (19) Mkaazi wa Mbweni.

Wengine ni Hashim Juma Issa (54) Mkaazi wa Mbweni Matar Fadhil Issa (54) Mkaazi wa Mbweni, walifikishwa katika kizimba cha mahakama ya hakimu Mdhamini Janet Nora Sekihola kujibu shitaka la  uzembe na ukorofi kinyume na kifungu cha 181 (d) cha kanuni ya adhabu sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Watuhumiwa wengine walifikishwa katika mahakama ya hakimu Omar Mcha Hamza na Valentine Andrew Katema, wakikabiliwa na mashitaka ya kufanya kitendo kinachoweza kuleta uvunjifu wa amani, ambao walishitakiwa chini ya kifungu cha 74 (1) (b) cha sheria namba 6/2004 sheria za Zanzibar.
Mashitaka yote hayo yaliwasilishwa kwa nyakati tofauti na waendesha Mashitaka, Wanasheria wa serikali Mohammed Kassim Hassan, Suleiman Haji Hassan pamoja na Ramadhan Abdallah, kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashitaka Zanzibar (DPP).
Katika mahakama ya hakimu Mohammed Ali Mohammed, Mwendesha Mashitaka Mohammed Kassim alidai kuwa watuhumiwa Mbarouk Said na Mussa Juma, bila ya halali walipatikana wakiandamana kupitia katika maeneo mbali mbali ya manispaa ya mji wa Zanzibar, kitendo ambacho kingeweza kuleta uvunjifu wa amani.
Watuhumiwa hao wote kwa pamoja walikana makosa hayo na kupewa dhamana ya masharti ya shilingi 300,000 kila mmoja ambapo walitimiza masharti hayo na wapo nje ya dhamana hadi Juni 16 mwaka huu, kwa kesi hiyo kutajwa.
Awali mahakamani hapo vikosi vya ulinzi na usalama walionekana kujipanga imara na kuhakikisha usalama umedhibitiwa wakati wote wa uendeshaji wa kesi hiyo ambapo maeneo yote ya Mahakama ya Mwanakwerekwe yaliimarishwa ulinzi ndani na nje ya eneo hilo.

Mamia ya wananchi walifika katika eneo la mahakama hiyo na kuja kusikiliza kesi hiyo lakini waliishia nje ya mahakama hiyo kutokana na ulinzi uliozunguka katika eneo hilo mwanzo hadi mwisho wa kesi hiyo.

Licha ya watu hao 30 kufikishwa mahakamani leo lakini hali ya amani bado haijatengeneza kutokana na baadhi ya maeneo kurushwa mabomu ya machozi na watu kadhaa kutawanywa katika maeneo ya Mwanakwerekwe, Darajabovu, Amani na Mikunguni muda mfupi baada ya wananchi kutoka katika eneo la mahakama hiyo.

WAZIRI wa Mambo ya Ndani Akutana na Viongozi wa Dini na Waandishi Zanzibar



Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk.Emmanuel Nchimbi, akizungumza na Viongozi wa Jumuiya za Kiislam na Wadau wac Sekta ya Utalii Zanzibar, kuhusiana na fujo zilizotokea juzi Zanzibar, kulia Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema na kushoto Kamishna wa Polisi Zanzibar Mussa Ali.



Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania IGP Said Mwema, akizungumza katika Mkutano huo uliofanyika Makao Makuu ya Polisi Zanzibar Kilimani.



Viongozi wa Jumuiya za Kiislam Zanzibar  wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza nao kuhusiana na matukio yaliotokea katika Visiwa vya Zanzibar. 



Viongozi wa Jumuiya  za Sekta ya Utalii Zanzibar wakimsikiliza Waziri wa Mambo ya Ndani, akizungumzia hali iliojitokeza juzi ya fujo katika mitaa ya Mji wa Zanzibar. na kulani hali hiyo.isitokee tena  ikaharibu  Amani ya Visiwa vya Zanzibar ambavyo vinasifika kwa Amani katika Afrika Mashariki.



  Ofisa wa Ubalozi wa Marekani aliopo Zanzibar Jefferson Smith, amelipongeza Jeshi la Polisi kwa jitihada zake za kurudisha hali ya Amani katika Mji wa Zanzibar bila ya kutokea madhara kwa Wananchi na kulipongeza kuwakutanisha Viongozi mbalimbali wa Jumuiya ya Dini na Wadau wa Sekta ya Utalii kuzungumza  nao, jinsi ya kuzuiya tatazo hili lisitokee tena.



SHEKH. Saleh Zam, akitowa shukrani kwa niaba ya Wanajumuiya za Kiislam Zanzibar baada ya kumalizika kwa Mkutano huo uliofanyika katika Ukumbi wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar. 

Monday, 28 May 2012

Maamuzi ya kesi ya LULU kusikilizwa Juni 16

 Msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael a.k.a Lulu akiwa Mahakamani mapena leo wakati alipofika kusikiliza mashtaka yake yanayomkabili kuhusiana na tuhuma za mauaji ya msanii mwenzake,Marehemu Steven Kanumba 



Lulu akiwa mahakamani hapo.Lulu akiwasili Mahakamani hapo.

Mahakama Kuu kanda ya Dar es salaam imepanga kutatoa uamuzi juu ya umri wa msanii wa filamu nchini Elizabeth Michael maarufu kwa jina la Lulu anayekabiliwa na kesi ya mauaji ya msanii mwenzake Steven Kanumba Aprili 7 mwaka huu.
Jaji Fauz Twaib leo alisikiliza mapingamizi ya mawakili wa serikali kuhusiana na maombi ya mawakili wanaomtetea Lulu waliyowasilisha mahakamani hapo kuiomba korti hiyo aidha ichunguze umri wa Lulu anayedai ana miaka 17 au iamuru mahakama ya kisutu kuchunguza.
Baada ya kuwasilishwa maombi hayo leo ilikuwa ni siku ya kusikilizwa maombi mahakamani ambapo wakili Shadrack Kimaro wa Serikali alipinga vikali maombi hayo kuwepo mahakamani hapo akidai kuwa hayakustahili kuwepo na badala yake yatupwe.
Alidai walichofanya ni kinyume cha sheria ilipaswa wakate rufaa kwasababu maombi yalishafika mahakama ya kisutu inakosikilizwa kesi hiyo na kutolewa maamuzi hivyo haikuwa sahihi kufungua maombi mapya wakati sio maombi mapya.
Aliwashauri mawakili wa Lulu aidha kukata rufaa maamuzi ya Kisutu au kuomba maamuzi yale kufanyiwa mapitio. Hata hivyo alidai kifungu cha sheria kilichotumika kuwasilisha maombi hayo sio sahihi ilipaswa kitumike kifungu ambacho kitaipa mamlaka korti hiyo kusikiliza maombi.
Mawakili wa Lulu, Furgence Masawe, Peter Kibatala na Kennedy Fungamtama hawakukubaliana na hayo,ambapo Fungamtama aliiomba mahakama kupokea maombi yao na kutolea uamuzi kwasababu ndiko maombi yao yanakotakiwa kupelekwa.
Aliusoma upya uamuzi uliotolewa Kisutu na kudai kuwa haukuwa uamuzi bali maelekezo ya mahakama na wao wamefata maamuzi hayo yaliyowataka kuwasilisha maombi yoyote Mahakama Kuu kwasababu mahakama ile haina mamlaka ya kusikiliza kesi ya mauaji.
Baada ya kusikiliza mabishano hayo ya kisheria mahakama hiyo imepanga kutoa maamuzi Juni 16 mwaka huu.

Wednesday, 23 May 2012

Nzi zaidi ya wawili wasipige kelele China





Serikali ya China imetangaza kuwa choo chochote cha umma hakitakiwi kuwa na nzi zaidi ya wawili wanaoruka kwa wakati wowote.
Hiyo ni moja kati ya mfululizo wa viwango vipya vilivyowekwa na mamlaka hiyo kujaribu kufanya bora maeneo ya umma mjini humo.
Malengo mengine yanahusu usafi, matumizi ya vifaa na mafunzo kwa watendaji.
Mwandishi wa BBC aliyeko Beijing anasema sheria hizo mpya zimelenga watu wanaoishi katika maeneo ya zamani ya mji huo.
CCM, yageuka paka, yatapika na kuramba



Elias Msuya
BAADA ya kuwa na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM na baadaye kuwa na semina kuhusu ‘Mwongozo wa CCM katika kushiriki mjadala wa Katiba mpya’ iliyofanyika mkoani Dodoma hivi karibuni chama hicho kimeibuka na maazimio yanayooneka kama ni kumeza matapishi yake.

Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na kuhoji mahakamani matokeo ya uchaguzi wa Rais, uwezekano wa kuwa na Serikali tatu, kupunguza madaraka ya Rais, kuwa na Tume Huru ya Uchaguzi, kuwa na mgombea huru na kujadili kero za Muungano.

Kwa muda mrefu kumekuwa na shinikizo kutoka kwa watu wa kada mbalimbali, wakiwemo wanaharakati na wanasheria wamekuwa wakihoji kuhusu mambo hayo na hasa kuelekea katika Katiba mpya, huku chama hicho kikipinga.

Kwa mfano suala la mgombea binafsi limekuwa likipingwa na chama hicho kwa muda mrefu kwa hofu kuwa lingeweza kukiumiza pindi wanachama wake wanaposhindwa kura za maoni, kwani wangeweza kusimama binafsi na kushinda.

Suala la kupinga matokeo ya urais nalo limekuwa likilalamikiwa, lakini walalamikaji wamekuwa wakikosa nguvu kutokana na Katiba Ibara ya 41 (7) inayosema, “Iwapo mgombea ametangazwa na Tume ya Uchaguzi kwamba amechaguliwa kuwa Rais, hakuna mahakama yoyote itakayokuwa na mamlaka kuchunguza kuchaguliwa kwake.”

Madaraka ya Rais wa Zanzibar nayo yamezua mjadala hasa kwa Wazanzibari wakihoji rais wao kushushwa hadhi.
Hayo yanatokana na mabadiliko ya 11 ya Katiba yalipomwondoa Rais huyo kutoka kuwa Makamu wa Rais na kubakia kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kuhusu Tume ya Uchaguzi, makundi mbalimbali yamekuwa yakishinikiza kuwapo kwa tume huru kwa madai kuwa tume ya sasa inaundwa na makada wa CCM wanaokipendelea chama hicho.

Kuhusu uteuzi wa mawaziri na Waziri Mkuu, kumekuwapo na maoni kutoka makundi mbalimbali kwamba mfumo wa Westminster wa kuteua mawaziri kutoka bungeni uachwe badala yake utumike mfumo wa mawaziri kuteuliwa nje ya Bunge ili kuwezesha uwajibikaji.

Kwa mujibu wa Katiba ya sasa Ibara ya 51 (2) Rais anaruhusiwa kumteua mbunge wa kuchaguliwa kutoka jimbo la uchaguzi anayetokana na chama cha siasa chenye wabunge wengi bungeni au kama hakuna chama cha siasa chenye wabunge wengi zaidi anayeelekea kuungwa mkono na wabunge walio wengi kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.

Lakini akizungumza na waandishi wa habari hivi karibuni jijini Dar es Salaam, Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema mambo hayo yanahusu uendeshaji wa serikali na kutaka wananchi wapewe fursa ya kuchangia maoni yao kwa kadiri wanavyoona inafaa kwa kuzingatia maslahi ya taifa.

Ametaja mengine kuwa ni kuhusu muundo wa Bunge na Baraza la Wawakilishi na aina ya wabunge na wawakilishi, uwapo wa baraza la pili la kutunga sheria, ukomo wa idadi ya wabunge, mfumo wa mahakama na nafasi ya Rais wa Zanzibar katika uongozi wa serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Katiba

Licha ya kufunguka na kutaka mabadiliko yafanyike, Nape ameshauri mambo 15 kubakizwa katika Katiba kwa kuwa ndiyo misingi mikuu ya Taifa.

Ameyataja mambo hayo kuwa ni muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano kuwa wa serikali mbili yaani Serikali Jamhuri ya Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar akiongeza kuwa ni sera ya CCM isiyo na upungufu.

Mengine ni kufanyika kwa uchaguzi wa mara kwa mara katika vipindi maalum na kuzingatia haki ya kupiga kura kwa kila mtu mwenye sifa zinazohitajika kwa mujibu wa sheria, kuendeleza uhifadhi na ukuzaji wa haki za binadamu na kuheshimu usawa mbele ya sheria, kuendeleza sera ya dola kutokuwa na dini rasmi, bali inaruhusu kila mtu awe na uhuru wa kufuata dini anayoitaka mwenyewe.

Mengine ni kuendeleza sera ya serikali kuwa ndiye mmiliki wa rasilimali kuu za nchi, hususan ardhi, kuendeleza sera ya kuwapo kwa usimamizi madhubuti wa maadili ya viongozi kwa kuupa nguvu za kikatiba na kuimarisha madaraka ya umma.

Mengine ni kuhamasisha sera ya msingi ya kujitegemea, kusimamia usawa wa jinsia na haki za wanawake, watoto na makundi mengine maalum katika jamii, kusimamia hifadhi ya mazingira na kuendelea kuwapo kwa Rais Mtendaji.

Kwa nini mabadiliko sasa?
Kutokana na msimamo huo mpya wa CCM ambayo zamani haikuwa nao, kumekuwa na hisia kwamba sasa chama hicho kimeanza kuhisi anguko hivyo kinajipanga kwa kutafuta ushawishi zaidi kwa wananchi.

Wakizungumza kuhusu hali hiyo, baadhi ya wataalamu wa siasa na wanasiasa wenyewe, wanasema hiyo ni dalili ya CCM kusoma mchezo wa mabadiliko yanayokuja siku za usoni hasa uchaguzi wa mwaka 2015.

Mhadhiri wa Sayansi ya Siasa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Benson Bana anasema CCM kimesoma alama za nyakati.

“Hilo siyo suala la kushtuka, chama chochote cha siasa lazima kisome alama za nyakati za siasa, ndiyo maana utaona wamekubali hata suala la mgombea binafsi kama hivyo.”anasema Dk Bana.

Anaongeza kuwa CCM kimeshahisi homa ya mabadiliko nchini hasa nguvu ya upinzani inayokua kwa kasi na kutoa mfano wa Chadema.
“Kwa sasa kuna nguvu ya mabadiliko inakuja, kuna chama mbadala cha Chadema kwa hiyo lazima CCM kiwe ‘flexible’.”

Amengeza pia kwamba vyama vya siasa havipaswi kufungwa tu na itikadi na misimamo isiyovisadia kwani hufika mahali ikashindikana kutumika.

“Vyama vya siasa huunganishwa na itikadi zao, lakini wananchi hawaangalii itikadi, wao wanaangalia nani kafanya nini, kwa hiyo kung’ang’ania itikadi ni kufanya kosa,” anasema na kuongeza,

“Kwa mfano watu kama kina Shibuda (John) wangeweza kuhama CCM na kuwa wagombea binafsi kama wangeruhusiwa. Nadhani haya ni maendeleo mazuri kuliko kung’ang’ania misimamo ambayo hailisaidii Taifa.”

Kwa upande wake mhadhiri wa Chuo Kikuu Guria cha Tanzania Emmanuel Mallya, anasema tatizo la CCM ni ukongwe hivyo kinatafuta kujiepusha na matatizo yote yanayoelekezwa kwake.

“Tatizo la CCM ni ukongwe wa chama kma vilivyo vyama vingine vya muda mrefu kwa hiyo kila tatizo la nchi hii wanahusishwa nalo. Halafu hayo mabadiliko ambayo tunaita ni mabadiliko ya sura tu, kwa sasa yanahitajika mabadiliko kwenye chama na serekalini.”anasema Mallya.

Mallya anaonyesha wasiwasi kama kweli CCM kinadhamira ya kweli kukifanya kuwa chama cha wananchi wote, au ni yale yale ya kulindana?

“Je, katika mabadiko wanayofanya wanahusisha kukipeleka chama kwa wananchi? Jiulize wewe mwenyewe ni rahisi kugombea nafasi ya uongozi kupitia CCM kama si Mnauye, Mwinyi, Nyerere, Kikwete, Malecela au Mzindakaya?” anahoji Mallya.

Naye kada wa muda mrefu wa CCM Dk Hassy Kitine anasema kinachofanyika ndani ya CCM ni upanuzi wa demokrasia kutokana na kupanuka kwa demokrasia ndani ya chama na nchi kwa ujumla

“Mabadiliko ya CCM kama kuhoji madaraka ya Rais ni kupanuka kwa demokrasia ndani ya chama na nchi kulingana na hali ya siasa ya nchi” anasema Dk Kitine.
Ameongeza kuwa hali ya siasa imebadilika huku nguvu ya upinzani ikikitisha chama hicho kikongwe.

“Vyama vya upinzani ni vikubwa, ‘that’s obvious’, vimepanuka mno, lakini hata ndani ya CCM yenyewe kwa wanachama na wasio wanachama, wote wanataka demokrasia. Siyo kwamba CCM kimekuwa kikizuia demokrasia siku zote, hapana ni mabadiliko ya kupanuka tu kwa demokrasia,” anasema Dk Kitine.

undefined









 .





 .

 .

 .



 .





 .

  







Mkutano kundi la G77 and China katika mkutano wa mazingira jijini Bonn

undefined
Bi Fauzia Mwita, kutoka Idara ya Mazingira Zanzibar, akishiriki katika majadililiano ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendele katika mkutano wa kundi la G77 and China, katika mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaoendelea mjini Bonn.
 
Mkurugenzi wa mzingira zanzibar Bw Sheha Mjaja, akifuatilia mjadala wa kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika mkutano wa kundi la G77 na China, kwenye Mkutano wa mabadiliko ya Tabia nchi unaendelea mjini Bonn
 
Bw. Ladsalus Kyaruzi, na Injinia Alphonce Bikulamchi Maafisa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais wakishiriki katika majadiliano ya kuweka msimamo wa pamoja wa nchi zinazoendelea katika kundi la G77 na China.katika mkutano wa mabadiliko ya tabia nchi unaoendelea mjini Bonn.
.
WACHAWI WANASWA KATIKA KANISA LA UFUNUO JIJINI MWANZA
VIDEO YA FREEMAN MBOWE AKIZUNGUMZA MABADILIKO YANAYOKUJA KWA KASI NA TAFSIRI YAKE KATIKA NCHI

Epukeni udanganyifu katika michezo- Maalim


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akisalimiana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ligi ya vijana “Central Taifa” waliofika ofisini kwake Migombani kwa ajili ya kubadilishana nae mawazo. Katikati ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk na pembeni (kulia) ni mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sherry Khamis.

Na Salma Said
Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar imesema itafanya kila liwezekanalo ili kuiwezesha ligi ya vijana Zanzibar iweze kusonga mbele. Waziri wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk alitoa ahadi hiyo mbele ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, wakati kamati ya ligi hiyo Central Taifa ilipokutana na Maalim Seif ofisini kwake Migombani.
Aliahidi kuwa Wizara ya habari itatafuta fedha kwa njia yoyote ili kuhakikisha kuwa fainali za ligi hiyo inayotarajiwa kufikia kilele chake July mwaka huu kwa timu za Juvinail, Junior na Central zinafanikiwa. Alisema ligi hiyo ni muhimu katika kuibua vipaji vya vijana ambavyo vitasaidia kuinua soka la Zanzibar.
Kwa upande wake Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amewataka viongozi wa ligi hiyo kuwa na dhamira ya kweli katika kuendeleza ligi hiyo, sambamba na kuepukana na vitendo vyovyote vya udanganyifu katika kuibua vipaji vya wanasoka vijana.
“Sisi serikali tuko very serious na mimi binafsi niko interested kuona hadhi ya michezo inarejea Zanzibar, kwa hiyo na nyinyi viongozi muwe serious kwa hili”, alisistiza Maalim Seif.
Amewatahadharisha viongozi hao kuzitumia fedha wanazopewa kwa kutimiza malengo yaliyokusudiwa na sio kuzitumia kwa maslahi binafsi. “ Wakati mwengine tunakosa ufadhili kwa kuwa hatuko serious, hao wafadhili nao wanaangalia ni kwa kiasi gani fedha zao zinatumika kwa malengo yanayokusudiwa, vyenginevyo ndio wanaona hakuna haja ya kutoa ufadhili” aliongeza.
Nao viongozi wa chama cha soka Zanzibar ZFA wakiwemo kaimu Rais wa ZFA Haji Ameir na mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar Bi Sherry Khamis, wamesifu utendaji wa Waziri mpya wa Wizara hiyo Mhe. Said Ali Mbarouk, na kwamba unawapa changamoto katika utendaji wao.
Wamesema Waziri huyo amedhamiria kweli kufanya kazi aliyotumwa na kamwe hakuna mzaha wala muhali, kama ambavyo mwenyewe amekuwa akieleza mara kwa mara.
Ligi ya vijana kwa ngazi za Juvinail, Junior na Central inazishirikisha timu za mitaani za vijana zilizopata usajili ambazo hushindana hadi ngazi ya Wilaya Unguja na Pemba ambapo hupatikana mshindi mmoja kwa kila Wilaya, na kuanzia hapo ndio kamati ya Central Taifa hushughulikia kwa ajili ya kuandaa fainali ambazo hufanyika Unguja na Pemba.

Ngonjera za CCM na upepo wa mabadiliko

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Pius Msekwa
Na Abdallah Vuai, Zanzibar
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Tanzania Bara, Pius Msekwa akihojiwa na Shirika la Utangazaji la Ujerumani wiki iliyopita aliweka bayana msimamo wa Chama chake kubakia na sera ya Serikali mbili katika Muungano. Katika mahojiano na DW Msekwa alisisitiza na kuwakumbusha wanachama wa CCM wakati watakapotoa maoni mbele ya Tume ya Katiba kukumbuka sera ya Chama hicho katika Muungano ni kubakia na Serikali mbili.
Ama kweli Msekwa ameachwa nyuma katika wakati mpya, anaonekana wazi kuwa anashindwa kubaini hisia za Wazanzibari na hata zile za wanachama wake ndani ya CCM kwamba wamechoka na sera zisizowaletea manufaa.
Muundo wa Serikali mbili umeelezwa na watu wengi kwamba ndio kiini cha matatizo mengi ya Muungano,lakini mtu kama Msekwa ambaye ameshiriki kuandika katiba ya mwaka 1977 angeweza kutoa ushauri ambao unaendana na mazingira ya sasa.
Wazanzibari wengi hawautaki Muungano wa kikatiba, wanapendelea kuwepo na muundo mpya wa Muungano usio wa Serikali mbili wenye manufaa kwao.
Sera ya Serikali mbili ni sawa na nyumba kongwe na nguo iliyochakaa, lakini kwenye macho ya CCM bado inaonekana mpya, fikra za watu wengi walitegemea kikao cha NEC kingekuja na mkakati wa ujenzi wa nyumba mpya iwe na haiba mpya na yenye mvuto hata kwa wapiti njia wakatamani nao kuwa na nyumba ya aina hiyo au ramani yake.
Nyumba hiyo iliyojengwa kwa mawe na chokaa Wazanzibari hawaipendi, hata ukiifanyia matengenezo ni yake yale,mbwa kumwita jibwa , ukiacha mawe,chokaa,udongo wake hauwezi tena kushika chokaa na pia haiwezi kuhimili vishindo,ni lazima ijengwe upya katika mtindo mpya na wa kisasa.
Ikiwa CCM itaendelea kupuuza ujenzi wa nyumba mpya ya matofali,saruji,basi ijiandae kukataliwa na wapigakura katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 kwani kwa hali ilivyo Zanzibar Chama chochote cha siasa ambacho kitakumbatia sera ya Serikali mbali au tatu hakitaweza kupata uungwaji mkono na wapigakura.
Ingawa Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais mstaafu Amani Abeid Karume kabla ya kustaafu aliweka misingi imara ya kukihakikishia Chama chake kubakia ndani ya Serikali hata kikishindwa uchaguzi chini ya maridhiano ya kisiasa yaliyosababisha katiba kurekebishwa na kuwepo kwa Serikali ya umoja wa kitaifa.
Karume amemaliza kazi ya Urais na mwishoni mwa mwaka huu atamaliza kazi ya Umakamu Mwenyekiti wa CCM kwa kujijengea mazingira ambayo hata kikishika nafasi ya pili katika uchaguzi kitakuwepo,lakini hilo halikuwa lengo la Karume,lakini kwa hali ya leo mwendo wa CCM Zanzibar ni mbaya hauridhishi na zaidi tangu kumalizika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010.
Wana CCM wanamtaja pia Naibu Katibu Mkuu mstaafu,Saleh Ramadhan Ferouz kuwa aliweza kukiongoza Chama hicho katika ushindi katika uchaguzi wa mwaka 2005 na ule uliopita,lakini wanamashaka kama rekodi hiyo inaweza kuendelezwa au la.
Ile Maskani kaka ya muembe kisonge imekuwa daraja na jiko la kutafuta chejio kwa wengine, magari makubwa kwa kunufaika na siasa za kushupaliana, iwapo CCM itashindwa kukabili wimbi la mabadiko kitajikuta kikimbiwa na wanachama kama wenzao Bara wanavyohamia CHADEMA.
CCM Zanzibar inapita katika kipindi kigumu na ikiwa Naibu Katibu Mkuu Vuai Ali Vuai mtendaji mkuu wa shughuli za kila siku za CCM anayefanyia kazi zake Zanzibar asipokuwa makini na kukubali kusoma wakati anaweza kuingia kwenye historia ya Chama chake kuwa mshindi wa pili katika uchaguzi mkuu.
Mabadiliko ni lazima hakuna atakayeweza kuyazuia kwani wakati umebadilika,ni matarajio kwamba CCM ndio chama kilichoshinda kwa maana ya Chama tawala kiwaongoze Wazanzibari kufikia katika muundo wa Muungano wanaoutaka ambao ni ule wa mkataba sio tena wa kikatiba.
Na iwe itakavyokuwa, hali halisi ya muundo wa Muungano unahitaji mabadiliko ambayo yatakubaliwa na Wazanzibari,lakini hatua yoyote ambayo inawanyima haki hawatakubali kwani nguvu ya umma ambayo imeoneshwa katika mikutano tofauti ya kudai kuwepo kwa mfumo mzuri wa muungano haiwezi kuzuilika kwa ngonjera za CCM.
CCM inapaswa kutumia fursa ya kuandika kwa Katiba mpya kutoa ushawishi wa kubadili mfumo wa muundo wa muungano ambao kilio cha Wazanzibari kwa sasa kama walivyoamua kuvuana magamba basi nawaamuwe kuvua muundo mkongwe wa Serikali mbili, kwani “ukiamua kula Mbwa ule Mbwa wa Kizungu, usile Popi anayeshinda kwenye majaa. ”
Mfano wa Popi isije kutafsiriwa kuwa ndio kitoweo sahihi cha Watanzania ni kujaribu kutoa tofauti ya Mbwa wa Kizungu na Popi wa Tandale kwa tumbo au Chwaka.
Waafrika wengi wana imani kuwa kitu kizuri na chenye thamani hakiwezi kuwa cha Kiswahili, bali lazima kiwe cha Kizungu. Kuna Kuku wa Kizungu,mayai ya kizungu, embe ya kizungu, na Kuku wa Kienyeji!
Katika Muungano ni hivyo hivyo, Miungano ya kizungu imekuwa haina malalamiko,tazama Muungano wa Ulaya, Uingereza, Ubelgiji na hata Marekani,lakini Afrika wapi leo uko wapi Muungano wa Senegal na Gambia,uko wapi Muungano wa Ginneu, Misri na Morocco,Sudan, Ethiopia?
Yawezekana kabisa kusambaratika kwa Muungano wa Mataifa hayo kumetokana na kuwepo kwa mfumo dhaifu wa muundo,hivyo kwa kuwa Tanzania itaandikwa Katiba mpya wakati ndio huu kuweka sawa nyumba yetu.
Kwa wale wote wanaopenda kuiona Zanzibar ikirudia zama zake za kuwa kituo cha kibiashara katika ukanda wa Afrika Mashariki hawana budi kuunga mkono kubadili muundo wa muungano kwani ikiwa tutakuwa na muungano wa mkataba Zanzibar inaweza kuwa kituo kikubwa cha biashara kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Bandari huru itafanya kazi kama ilivyo katika nchi za Dubai, Emirate, Singapore, Malasyia, Hong Kong, ambapo itachangia kukuza uchumi wa eneo la maziwa makuuu.

Tuesday, 22 May 2012

Makali ya Kamati Teule Yaaza Kazi. Ocean View Yaubomoa Mkahawa Uliojengwa ufukweni



Wafanyakazi wa Hoteli ya Zanzibar Ocean View Kilimani wakibomowa jengo la mgahawa huo uliojengwa katika ufukwe wa pawani ya hiyo baada, kama inavyooneka mafundi wakiwa katika harakati za uvunjaji huo uliofanyika hivi karibuni katika eneo hilo.


Jengo la Mgahawahuo likionekana mandhari yake katika ufukwe wa pawani hiyo ya Kilimani kuelekea ngazi mia.
HOTELI ya Zanzibar Ocean View iliyopo Kilimani mjini hapa, imevunja na kuubomoa mkahawa iliyoujenga kinyume na sheria pembezoni mwa ufukwe wa bahari.
Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa kuvunjwa kwa mkahawa huo kumekuja ndani ya kipindi cha mwezi mmoja kufuatia kutolewa kwa ripoti ya kamati teule ya Baraza la Wawakilishi, ambayo ilielezea kwa kina ukiukwaji wa sheria unaofanywa na wawekezaji wa miradi ya hoteli za kitalii.
Ripoti hiyo ilizitaja hoteli kadhaa zilizopo katika visiwa vya Unguja na Pemba ambazo ujenzi wake umekiuka sheria kwa kujengwa ufukweni, huku kamati hiyo ikiibuka na mpendekezo kadhaa.
Pamoja na Meneja Mkuu wa hoteli hiyo Gilbert Kazungu kushindwa kuliweka wazi gazeti hili kuwa hatua hiyo ni kufuata maagizo ya kamati teule ya Baraza, lakini alisema hoteli imeamua kuvunja mkahawa huo uliokuwa ukijulikana kwa jina la Vero kutokana na kuwepo malalamiko kutoka kwa vyombo husika.
Maneja huyo alisema kutokana na malalamiko hayo, mmiliki wa hoteli hiyo Amani Ibrahim Makungu, amekubali uvunje, ikiwa ni kuitikia wito wa serikali juu ya kufuatwa kwa sheria zinazokwenda kinyume na ujenzi ufukweni.
“Mmiliki wa hoteli ameamua tuuvunje kwa kuelewa kuwa hakuna aliye juu ya sheria, alisema tumevunja sheria ya mazingira hakuna budi kuuvunja mkahawa huu bila ya kujali hasara tutakayopata kwa hatua tunayoichukua”, alisema Meneja huyo.
Alifahamisha kuwa mkahawa wa Vero, ulijengwa mwaka mmoja na nusu uliopita kwa gharanma za shilingi milioni 7.5 kwa lengo la kuongeza eneo la kupata huduma ya chakula kwa wateja pamoja na wateja wa hoteli hiyo kupata mandhari nzuri ya bahari.
Hata hivyo meneja huyo alijitetea kuwa kujengwa kwenye ufukwe haikuwa na lengo la kuvunja makusudi sheria, ila walilenga kupanua wigo wa biashara hasa ikizingatiwa kuwa hoteli nyingi zilizopo Zanzibar tayari zimeshafanya ujenzi kama huo.
Kazungu alilamika kuwa lazima hoteli zote zilizovunja sheria ya ujenzi ufukweni ziwajibike kama ilivyowajibika hoteli yake na isiwe miradi ya wazawa tu ndiyo inayopewa shindikizo huku miradi ya wageni ikiachwa iendelee kuvunja sheria.
Katika ripoti ya kamati teule, hoteli ya Zanzibar Ocean View ilitajwa kama miongoni mwa zile zilizokiuka ujenzi kwa kujengwa ufukweni mwa bahari.
“Kuna uvamizi mkubwa wa maeneo ya fukwe na uharibifu wa mazingira na kamati imejiridhisha kwamba, ujenzi wa miradi ya mahoteli Zanzibar hauzingatii matakwa ya sheria zinazoelekeza juu ya masuala ya ardhi na mazingira”, ilieleza sehemu ya ripoti hiyo.
Miongoni mwa mapendekezo ya kamati hiyo ni kutaka hatua za kisheria zichukuliwe kwa dhidi ya wawekezaji waliojenga kwa kukiuka sheria ya mazingira.

Sauti:Bei ya umeme yapandishwa kwa asilimia 85 Zanzibar

Salma Said ,
Wakati wananchi katika visiwa vya Zanzibar wanalalamikia kupanda kwa bei za mahitaji muhimu ikiwemo vyakula, serikali katika visiwa hivyo imepandisha bei ya umeme kwa asilimia 85 ambapo wananchi watalazimika kulipia huduma ya umeme kuanzia tarehe mosi mezi ujao. Zanzibar yenye idadi ya watu wanaokisiwa zaidi ya million moja, ina watumiaji wa umeme zaidi ya laki moja na elfu tano.
Kasi ya matumizi ya Umeme Zanzibar imekuwa ukiongezeka kila mara kutokana na matumizi ya nishati hiyo kuongezeka pamoja na kampeni za kutaka wananchi watumie zaidi umeme na kupunguza ukataji miti ili kuepuka uharibifu wa mazingira.
Meneja Mkuu wa Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO), Hassan Ali Mbarouk akitangaza hatua hiyo mbele ya waandishi wa habari ambapo alisema bei mpya itaanza kutumika Juni 1, mwaka huu.
Alisema shirika limepandisha bei kwa watumiaji wote kwamba bei hiyo mpya imepangwa katika viwango vya makundi matano.
Alisema makundi hayo ni pamoja na huduma ya kiwango cha kiwango cha uwezo mdogo, huduma ya jamii, viwanda vidogo, viwanda vya kati na vikubwa na taa za barabarani.
Mbarouk alisema kuamnzia Juni 1, umeme utauzwa shilingi 66 kwa uniti badala ya shilingi 50, kwa watumiaji wa kiwango cha uwezo mdogo.
Alisema watumiaji wa huduma ya jamii watalipa shilingi 161 kwa uniti badala ya bei ya sasa ya shilingi 120 na watumiaji wa kiwango cha viwanda wanunua umeme kwa bei mpya ya shilingi 172.00 kwa uniti badala ya shilingi 140.00.
Alisema watumiaji wa kiwango cha viwanda vya kati na vikubwa watalipa shilingi 169.00 badala ya shilingi 140.00 kabla ya bei mpya na kwamba gharama ya umeme wa taa za barabarani umepanda kufikia shilingi 141.00 kwa uniti kutoka bei ya shilingi 105.00.
Mbarouk alisema ongezeko la bei mpya litafanyika katika awamu tatu kabla ya kufikia lengo la kuongeza gharama ya huduma hiyo kwa asilimia 85.
Alisema katika utekelezaji wa awamu ya kwanza umeme utapanda kwa asilimia 40, awamu ya pili bei itaongezeka kwa asilimia 30 na ya tatu pia kwa asilimia 30.
Alipoulizwa sababu za ongezeko hilo, Mbarouk alisema shirika limechukua uamuzi huo kutokana na kupanda kwa gharama za uendeshaji.
Ni kipindi ambacho sauti za wananchi kulalamikia kupanda ovyo kwa bei imekuwa ikiongozeka, lakini viongozi wa serikali wanasema kwamba hali za bei visiwani bado ni nafuu sana kulinganisha na nchi jirani.
Licha ya maelezo ya viongozi wa serikali, wananchi wanasema kuwa serikali haijaweza kujipanga vizuri ili kudhibiti mfumko wa bei wa bidhaa muhimu, hali ambayo inawaathiri wananchi wengi masikini na sasa kuongezeka bei ya umeme lakini Meneja wa shirika la umeme anasema pamoja na kupanda kwa bei za umeme Zanzibar, wananchi watalipia bei mpya kwa awamu tatu.
Zanzibar inanunuwa umeme wake kutoka Tanzania bara kupitia mkonga (Waya) wa umeme unaopita chini ya bahari hadi katika kisiwa cha Unguja na Pemba.
Hata hivyo waya unaoleta umeme Unguja umechakaa, na serikali kwa msaada wa Dola za Kimarikani milioni 72 kutoka serikali ya Marekani inafanya juhudi za kuweka waya mpya.
Licha ya Zanzibar imo katika juhudi za kutafuta vyanzo vyengine vya umeme mfano matumizi ya nguvu za jua na upepo na wawekezaji kadhaa kutoka nje tayari wamejitokeza. Lakini bado itaendelea kuitegemea Shirika la Tanesco la Tanzania bara.
Watoto yatima waenda Uturuki


Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akikabidhi bendera ya Zanzibar kwa watoto mayatima na viongozi wao wanaokwenda nchini Uturuki kuiwakilisha Zanzibar katika kongamano la kimataifa kuhusu siku ya watoto yatima litakalofanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28/05 hadi 03/06/2012

Makamu wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad leo amekutana na uongozi wa Jumuiya ya Muzdalifat inayoyojishughulisha na utunzaji wa mayatima, pamoja na watoto wanaotarajia kusafiri kuelekea nchini Uturuki. Mwenyekiti wa jumuiya hiyo sheikh Abdallah Hadhir Abdallah amesema watoto hao wanne wanakwenda nchini Uturuki kwa ajili ya kushiriki katika kongamano la kimatifa kuhusu maadhimisho ya siku ya watoto yatima linalotarajiwa kufanyika mjini Istambul Uturuki kuanzia tarehe 28 mwezi huu hadi tarehe 3 mwezi ujao.
Watoto hao Salum Ali Mohd (miaka 10), Hajir Khalid Haji (miaka 11), Shufaa Mohd Ali (miaka 12) na Lutfia Sheha Mussa (miaka 11) wataongozana na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Muzdalifat Sheikh Abdalla Hadhir, Katibu wa Jumuiya ustadh Farouq Hamad Khamis na Mkuu wa kitengo cha mayatima Zanzibar Nassra Suleiman Abdallah.
Mapema Maalim Seif aliwakabidhi watoto hao bendera ya Zanzibar na kuwataka kuiwakilishi vyema nchi yao. Watoto hao na viongozi wao wanatarajiwa kuondoka nchini tarehe 28 mwezi huu.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif akutana na Balozi wa Msumbiji.
Na Hassan Hamad. (OMKR)



Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema inaendelea na juhudi zake za kuimarisha kilimo cha umwagiliaji ili kupunguza utegemezi wa chakula kutoka nchi za nje.

Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad alipokuwa na mazungumzo na balozi wa Msumbuji nchini Tanzania Bw. Amour Zacaria Kupela huko Ofisini kwake Migombani.

Amesema katika jitihada hizo serikali inakusudia kumwagilia jumla ya ekari elfu nane ambapo hadi sasa imefanikiwa kumwagilia ekari elfu mbili chini ya ufadhili wa serikali ya Korea.

Maalim Seif amefahamisha kuwa tayari washirika wengine wa maendeleo wameshaonesha nia ya kushirikiana na Zanzibar katika kilimo hicho cha umwagiliaji, na kwamba iwapo azma hiyo itakamilika Zanzibar itapunguza kwa kiasi kikubwa utegemezi wa chakula.

Sambamba na hilo Makamu wa Kwanza wa Rais amesema serikali pia inaimarisha utafiti wa kilimo na mbegu ili kupata mbegu bora ambazo baadaye zitasambazwa kwa wakulima kwa ajili ya kuendeleza kilimo.

Kwa upande mwengine amesema serikali bado inaendelea na mikakati ya kupunguza tatizo la ajira kwa vijana kwa kutoa elimu ya mafunzo ya amali ili vijana waweze kujiajiri pale wanapomaliza masomo yao.

“Serikali imeanzisha Wizara ya Kazi, Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi na Ushirika kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira ingawaje wapo vijana waliomaliza vyuo vikuu bado hawana ajira”, alifahamisha.

Maalim Seif amefafanua kuwa tatizo hilo linatokana na vijana wengi kusomea masomo ambayo yana wataalamu wa kutosha, na kutoa wito kwa vijana kutafuta masomo yatakayowawezesha kujiajiri baada ya kuhitimu.

Akizungumzia kuhusu suala la maji, Maalim Seif amesema Zanzibar bado inakabiliwa na tatizo hilo kutokana na uchakavu wa miundombinu ya maji pamoja na upungufu wa maji kwenye vianzio unaotokana na mabadiliko ya tabia nchi.

Hata hivyo amesema serikali tayari inalijua tatizo na imo katika mikakati ya kuliondosha.

Kuhusu mafanikio ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa Maalim Seif amesema mafanikio makubwa yamepatikana ikiwa ni pamoja na kuendelea kwa amani na utulivu, hali inayovutia wawekezaji wengi kuja kuwekeza Zanzibar.

Kwa upande wake balozi huyo wa Msumbiji anayemaliza muda wake Bw. Amour Kupela, amepongeza hatua iliyochukuliwa na Zanzibar ya kufikia maridhiano ya kisiasa na kupelekea kuundwa kwa serikali ya Umoja wa kitaifa ambayo inaonyesaha kupata mafanikio makubwa.

Balozi Kupela ameongeza kuwa Msumbiji na Zanzibar zina uhusiano wa kindugu wa muda mrefu na kutaka uhusiano huo uendelezwe kwa maslahi ya pande hizo mbili.

 
Wanahabari Zanzibar wapewa somo

Na Salum Vuai, Maelezo
WAANDISHI wa habari Zanzibar, wameaswa kufanya uchunguzi wa kina kabla kuandika au kutangaza taarifa wanazopewa na vyanzo mbalimbali.
Wameelezwa kuwa, si kila jambo wanaloambiwa, kusikia au kuona, kulichukulia kuwa ndiyo habari na kukimbilia kuitoa kwa umma.
Nasaha hizo zimetolewa na mwandishi wa habari mkongwe Salim Said Salim, wakati akitoa mafunzo katika warsha inayofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, juu ya namna hya kuandika habari kwa kuzingatia maadili na haki ya kujibu.
Salim alifahamisha kuwa, mara mwandishi anapoambiwa jambo, hana budi kulifanyia utafiti wa kina kabla kuliandika au kulirusha hewani, ili kuepuka migogoro.
"Taarifa mnazopata kuhusu jambo lolote, liwe kama mbegu ya kutafuta undani badala ya kukurupuka na kuandika, kwani watu wengine wanakuwa na ajenda zao, ambazo zinaweza kukutieni kwenye matatizo", alifafanua.
Alisisitiza kuwa mwandishi anapaswa kufanya maamuzi sahihi kabla kushika kalamu na kuandika taarifa anayoikusudia ili kujiepusha na kuwavunjia watu heshima.
Aidha aliwataka kupima juu ya kile wanachokiandika, na kujiepusha na habari zinazoweza kuwakashifu watu wengine mbele ya jamii kwa kuelezea mambo yao ya ndani ambayo hayana faida yoyote kwao na jamii wanayoiandikia zaidi ya kupandikza chuki na uhasama.
Akizungumzia juu ya matukio yanayopigwa picha, Salim alieleza kukerwa kwake na jinsi wapiga picha wengi wasivyojali wala kuzingatia staha ya mtu wanayempiga picha na hivyo kuijengea jina baya tasnia ya uandishi wa habari.
Alitoa mfano kwa wapiga picha katika mchezo wa netiboli, kusubiri sketi za wachezaji ziinuke, na kuona hapo ndipo pahala pa kupata picha nzuri, akisema ni lazima wanawake wastahiwe kwani ni mama na dada katika jamii inayowazunguka.
"Tusipendelee kuandika habari za kashfa hata kama ni za kweli kwani pamoja na kuishi katika zama za uwazi na ukweli, lakini kila mtu ana haki ya kuheshimiwa faragha yake", alieleza mwanahabari huyo mkongwe.
Alisisitiza kuwa mwandishi anapaswa kufanya maamuzi sahihi kabla kushika kalamu na kuandika taarifa anayoikusudia ili kujiepusha na kuwavunjia watu heshima.
Alisema hata pale kunapokuwa na makosa yaliyofanywa na viongozi wakuu wa nchi ambayo mwandishi nataka kuyabainisha, asitukie lugha ya kejeli, dharau na kusuta, na badala yake atoe yaliyo moyoni mwake kwa njia nzuri na lugha yenye staha huku lengo likiwa ni kufikisha ujumbe kwa muhusika na jamii kwa jumla.
Mafunzo hayo ya siku nne yameandaliwa na Baraza la Habari Tanzania (MCT) kupitia ofisi yake ya Zanzibar.

Monday, 21 May 2012

Kesi ya Terreblanche inamuliwa leo SA


Polisi wameimarisha doria hii leo katika mji wa Ventersdorp, nchini Afrika Kusini ambapo mahakama inasubiriwa kutoa hukumu kwa vijana wawili wa Kiafrika wanaotuhumiwa kumuua Eugene Terre' Blanche miaka miwili iliyopita.
Bwana Terre' blance alikuwa kiongozi wa mrengo wa kulia wa vuguvugu la kupigania utawala wa kizungu la Afrikaan Resistance Movement.
Wanaharakati wengi wa kutoka vuguvugu hilo hii leo wanatarajiwa kupiga kambi nje ya mahakama hiyo wakiwa wamevalia sare za chama hicho na wamebeba bunduki.
polisi
Polisi wamejitayarisha kupambana na ghasia

Chris Mahlangu mwenye umri wa miaka 28, na mvulana mmoja ambaye hawezi kutajwa kwa sababu ya umri wake, wanakabiliwa na mashtaka ya kumpiga aliyekuwa kiongozi wa AWB, Eugene Terreblance, hadi kufa nyumbani kwake viungani mwa mji wa Ventersdorp miaka miwili iliyopita.
Wawili hao wamekanusha mashtaka ya kumuua muajiri wao na kutekeleza uwizi wa mabavu.
Mahlangu anadai kuwa alikuwa akijitetea ili hali mvulana anayeshtakiwa pamoja naye amekanusha kuhusika na uhalifu huo.
Kizingiti kikubwa katika kesi hii ni kuwa Mahlangu na mvulana huyo walikataa kutoa ushahidi wao, wakati wa kesi hiyo.
Hali ya wasi wasi inatarajiwa kutanda nje la makahakama hiyo kama ilivyokuwa wakati wa kuanza kusikilizwa kwa kesi hiyo miaka miwili iliyopita.
Wakati huo, polisi walikabiliwa na wakati mgumu kuwatenganisha makundi ya wafuasi wa pande hizo mbili.
Lakini idara ya polisi na chama cha AWB zimesema kuwa ghasia zozote hazitarajiwi.
Polisi wamesema ikiwa mambo yatakwenda kinyume na matarajio yao, imeweka mikakati thabiti ili kuhakikisha kuwa hakuna mtu yeyote atakayevuruga shughuli za mahakama.
Mwezi uliopita, wakati mawakili walipokuwa wakitoa tetesi zao za mwisho mbele ya mahakama hiyo, jaji alionya kuwa hukumu huenda ikachukua muda mrefu lakini haijulikani, ikiwa uamuzi huo utachukua zaidi ya siku moja kutolewa.
Hata hivyo pande zote zinatarajiwa kukata rufaa baada ya hukumu kutolewa.
Zanzibar yaanza mchakato wa kutaka kujenga bandari mpya
Na Nafisa Madai Maelezo Zanzibar
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ) ipo mbioni katika kuhakikisha inajenga Bandari mpya katika eneo la Mpiga Duri kutokana na uhaba uliopo kwenye bandari inayotumika hivi ya Mlaindi.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Issa Haji Ussi mara baada ya kumaliza kwa ziara yake katika maeneo ya kuwekea makontena bandarini na Bwawani.
Amesema kuwa katika ziara yake hiyo ameona kuwa Shirika la Bandari Zanzibar linakabiliwa na changamoto kubwa ya uhaba wa eneo la kuwekea makontena pamoja na gati ya kufungia meli kubwa za mizigo.
Alisema kuwa hii inatokana na eneo hilo kuwa dogo la kuwekea makontena hayo na biashara mbali mbali ambazo zinatoka nje ya Zanzibar zinapitishwa hapo kwa ajili ya kuwafikia wananchi.
“Bandari ya Zanzibar inakabiliwa na changamoto kubwa sana ya uhaba wa eneo la kuwekea makontena pamoja na gati ya kuegeshea meli kubwa zinazobeba mizigo,”alisema.
Naibu Waziri huyo alisema kwamba Serikali ya Mapinduzi Zanzibar mwaka huu imeshuhudia ongezeko kubwa la makontena katika bandari ya Zanzibar ukilinganisha na miaka iliyopita.
Alisema kuanzia mwezi Januari hadi Machi mwaka huu jumla ya makontena 11,430 yaliingia katika bandari ya Zanzibar,ambapo pia alisema kuwa meli za makontena hivi sasa zinabeba kati ya makontena 400 hadi 800 kwa ajili ya Bandari ya Zanzibar ikilinganishwa na Makontena 100 hado 500 miaka ya nyuma.
Aidha Gavu alitoa mfano wa meli ya MV Lara Rickmers ambayo iliwasili visiwani humu Mei 19 mwaka huu ikiwa na makontena 668 ya kuteremesha,ililazimika kufunga gati Mei 20 baada ya Shirika kuandaa nafasi kwa kuyahamisha makontena 334 yaliokuwa matupu.
Alieleza kuwa meli hiyo ilianza kazi ya kushusha makontena hayo siku ya pili na mpaka jana tayari ilikuwa imweshashusha makontena 284 na inatarajiwa kumaliza kazi ya ushushaji Jumatano jioni ikiwa ni pamoja na kupakia makontena 500 matupu ya kampuni hiyo yaliokuwepo katika bandari ya Zanzibar.
“Hii inaonesha wazi kuwa wafanyakazi wa Shirika la Bandari wanafanya kazi kwa ufanishi wa hali ya juu na wanafanya ipasavyo isipokuwa nafasi ya kuwekea makontena na gati ndio tatizo kubwa,”alieleza.
Aidha Gavu alifahamisha kuwa kutokana na uhaba wa gati ya kufungia meli,iwapo meli mbili au tatu za makontena zitawasili siku moja au kukaribiana sana,ni lazima meli nyengine zibakie zimetia nanga zikisubiri nafasi.
Alieleza kuwa jumla ya meli tisa za mizigo kutoka nchi mbali mbali zinashusha mzigo katika bandari ya Zanzibar kila mwezi,ambapo alisema kuwa inasaidia kuingiza fedha nyingi ambazo hutumika katika kuleta maendeleo mbali mbali katika nchi.
Hata hivyo Naibu Waziri huyo alifahamisha kuwa bandari mpya ambayo inatarajiwa kujengwa katika maeneo ya Mpiga Duri itakuwa na ukubwa wa kilo mita tano ambayo itaweza kufunga gati kwa meli nne za mizigo tofauti na sasa ambapo meli moja tu ya mizigo ndio inayofunga gati.
Kuhusu bandari ya Pemba,Naibu Waziri huyo alisema kuwa bandari ya hiyo mpaka hivi sasa haina matatizo ambayo yaweza kuathiri utendaji wa kazi za Shirika hilo.
Alifahamisha kuwa matatizo yaliyopo kwenye bandari ya Mkoani na Wete kisiwani humo ni madogo sana, hivyo alifahamisha kuwa mara baada ya kumalizika kwa ujenzi wa bandari ya Zanzibar,fedha zitakazopatikana ndizo zitakazofanyia matengenezo bandari ya Pemba.
RAIS KIKWETE AFANYA UTEUZI WA MAJAJI WA MAHAKAMA YA RUFANI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amewateua Majaji wawili wa Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa Majaji wa Mahakama ya Rufani.
Walioteuliwa ni Jaji Semistodes S. Kaijage na Jaji Kipenka M. Musa na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo, Jumatatu, Mei 21, 2012 na Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Y. Sefue, uteuzi wao ulianza tokea Machi 15, mwaka huu, 2012.
Kabla ya kuteuliwa kwake kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji Kaijage (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam tangu Mei 17, 2007. Aliteuliwa kuwa Jaji Mahakama Kuu Novemba 28, mwaka 2000.
Naye Jaji Musa (57) alikuwa Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Tanga kabla ya kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Pia amewahi kuwa Wakili wa Serikali, Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jaji Mfawidhi, Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba. Aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu Septemba 13, 2004.
Imetolewa na:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,Ikulu.Dar es Salaam.21 Mei, 2012

Hasira zako Dk. Shein, ni hasara kwako


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein

Na Jabir Idrissa

RAIS wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein ni dhahiri amepandwa na hasira. Naona tayari “watu wake” wamemlisha fitna. Inawezekana kweli amechukizwa kubaini kundi kubwa la wananchi wa Zanzibar limepata hamasa ya namna ya kuja kutoa maoni yao mbele ya Tume ya Katiba ya Tanzania au kuikwepa wasiione. Wapambe watakuwa wamempa taarifa sizo. Na desturi inaonyesha mtu alopewa taarifa za uongo na kuziamini kwa kuwa waliompa ni “watu wake” anaowaamini, hujenga hasira. Sasa rais amepandwa na hasira. Nimethibitisha kwa matamshi yake alipokuwa kwenye hafla ya chama chake – Chama Cha Mapinduzi (CCM) – katika kijiji cha Koani, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Wakati nilipokuwa naandaa makala hii, pembeni yangu alikuwepo jamaa yangu mmoja kutoka Fuoni, nje kidogo ya mji wa Zanzibar, aliyekuja kunisalimia ofisini, akanihoji, “Mbona unasema hafla ya chama chake wakati taarifa nilizosoma zimeonyesha rais alikuwa katika ziara ya kiserikali akizuru mikoa yote ya Zanzibar na alianzia kisiwani Pemba.”
Sasa niseme sina hakika ziara yake ni ya kiserikali au ya kichama. Sikupata mtu wake ili kuthibitisha jambo hili. Angalau katika moja ya picha nilizoziona kupitia vituo vya televisheni vya Dar es Salaam, nimeona wanaokuwa chini yake ni wakuu wa mikoa zaidi ya ilivyo wenyeviti wa CCM wa mikoa anamopita.
Lakini hiyo si mada leo. Akili yangu imenielekeza katika kile ninachokiona kama matokeo ya watu wa Dk. Shein kumpotosha rais, na sasa kukuta tunaye rais aliyejaa hasira rohoni.
Tatizo la hasira, ni kwamba mtu mzima anapokasirika hata watoto watagunduwa haraka atakapojitokeza kwao. Wananchi wa Unguja na Pemba, tayari wanajua “baba yao” – Rais Dk. Shein – amekasirika. Sikiliza anachokisema Dk. Shein: “Naelewa fika kuna watu wanaoleta mambo ya ajabu ajabu lengo lao likiwa ni kuvuruga amani tuliyonayo.” “… lakini nasema tena, maana nimeshasema hakuna mwenye ubavu wa kuivunja amani ya Zanzibar na kama mtu kachoka na amani iliyopo, ahame hapa hapamfai; atafute sehemu nyingine akaishi.”
Rais akamalizia, kauli ambayo naifananisha na alichowahi kukisema rais mstaafu mmoja mwaka aliokuwa anatafuta ridhaa ya mara ya pili ya uongozi. Alitaja “mapanga, myundu na mashoka” yaliyotumika kufanikisha mapinduzi.
Dk. Shein yeye hakutaja majina hayo ya silaha makini na za asili, bali alichokisema kinafanana. Amesema hivi: “Hii (Zanzibar) ni nchi ya kimapinduzi.” Anakumbusha yaleyale. Tafsiri yangu kwa matamshi haya, ni kwamba ukurasa mpya wa uongozi wa mabavu (wengine wanaweza kusema ni udikteta) umefunguliwa.
Kweli Zanzibar ilifanya mapinduzi 12 Januari 1964 baada ya Wazanzibari waliokuwa mbele ya harakati za kuondoa utawala wa wageni, kutoridhika na uongozi wa serikali ya uhuru iliyoundwa kufuatia uhuru wa 10 Desemba 1963, kupindua serikali hiyo. Lakini uhuru huu si ushetani kama unavyoonekana na wapinduzi hao. Ikiwa hivyo ndivyo, basi huko ni kufuta historia ya kule nchi hii ya visiwa vikuu viwili na vingine vingi vidogo, ilikotoka.
Ukweli ulio mchungu kwa baadhi ya makada wa CCM hasa wasiopenda mabadiliko ya mfumo na sera za uongozi wa nchi, ni kwamba kama si uhuru huo, hakungekuwa na mapinduzi. Wangempindua nani? Dk. Shein huna haja ya kukasirikia wananchi. Badala yake ni muhimu sana utambue kuwa hata wao wanaipenda nchi yao kama uipendavyo wewe na ujivuniavyo kuiongoza. Wanaipenda sana. Hebu afikirie kwani wananchi wanaposema “hatutaki Muungano huu” unadhani tafsiri ni kutaka uvunjike au uvunjwe? Hapana. Wanataka viongozi wao mtambue maoni yao na kuyafanyia kazi.
Dk. Shein una bahati kuiongoza Zanzibar ndani ya zama za mapambazuko. Hakuna hata moja sasa linaloweza kufichwa lisijadiliwe na wananchi. Usikhofu maoni ya watu bali yazingatie, ndio sauti yao. Zama hizi zinahitaji sana uongozi unaosikiliza kile wanachokisema wananchi. Hawa wananchi wanaosema hawataki “muungano huu” si wajinga.
Wanajua wanachokisema, nawe wapaswa kujiuliza, “Lakini kwanini hawautaki.” Itakuwa ni jambo la hatari iwapo Dk. Shein na serikali unayoiongoza mtapuuza maoni ya; mtayachukulia kama ni kelele za mlango; mkiyachukulia ni kero kwenu. Viongozi mtakuwa mnafanya kosa kubwa ambalo linaweza kuwagharimu.
Siku hizi, kiongozi anayestarehe madarakani ni yule anayefikiria wananchi wake wanachokitaka. Wanasema nini? Wanachokifikiria. Wanawaelewa vipi viongozi wao. Haya ni mambo muhimu viongozi kuyajua. Hivi tuseme Dk. Shein unakosa nini kuwasikiliza wananchi wanaoamini muungano hauwanufaishi bali unawakandamiza? Sasa si ndivyo waonavyo? Kumbe mtu kufikiri hivi anakusumbua rais?
Dk. Shein kama unataka kuongoza vizuri, basi zingatia vilio vya wananchi unaowaongoza. Tena ungeshukuru na kufurahia kuwasikia wanasema au kulalamika hadharani.
Kama hujanielewa ninachokusudia, panda ndege hadi London. Fika pale eneo ambapo serikali ya Uingereza imefunga vinasa sauti na kupandikiza makachero na kuruhusu watu kutoa maoni kuhusu wanavyoiona serikali yao na wanavyomuona kiongozi wao mtukuka Malkia. Kama kupuuza maoni ya watu ni ushujaa, wangeanza viongozi Uingereza. Hawapuuzi bali wanayasikiliza maoni au malalamiko ya Waingereza. Na si hivyo tu, wanayafanyia kazi yanayosemwa.
Kama ni kero viongozi hujitahidi kuziondoa, kama ni uchafu wanausafisha na kama ni vikwazo vya kupatikana kwa maisha bora, wanaviondoa. Sasa Dk. Shein unataka wananchi walale usingizi hata pale unapohutubia? Unataka uongoze mazombi au majuha kalulu? Uongoze watu wasiofikiri siyo, wala kujinafasi pao? Unataka kuongoza watu muflisi?
Itakuwa ni bahati mbaya sana – kuongoza watu majuha kalulu. Kumbuka tayari Wazanzibari kiasili ni watu wenye akili sana, wanafikiri kabla ya kuamua, wanauliza maswali wakitaka majibu. Dk. Shein unajua vizuri kwamba kwa sababu ya ukweli huo, ndio maana Wazanzibari wengi wanafanya kazi kubwakubwa kwingineko Afrika, na hasahasa Marekani, Ulaya na Uarabuni.
Unajua fika mamia kwa mamia ya wale walioondoka nyumbani kukimbia vitimbi vya utawala mbaya baada ya mapinduzi, wamejijenga na kukabidhiwa dhamana zenye hadhi kubwa ughaibuni. Ni muhimu kutambua vipaji/vipawa vyao. Ukitambua hili huwezi kupata shida kuwaongoza. Utakuwa unajua tangu awali unao watu makini ambao ukiwatumia vizuri watakusaidia kuibadilisha nchi iwe kweli ya maziwa na asali badala ya tope na harufu mbaya.
Ila ukiamua kuwapuuza na kuwakandamiza, utabaki kuongoza kwa shida. Huwezi kuwashinda japo una dola, maana wao ndio wenye dhamana ya uongozi. Nakuaidhi punguza hasira maana hujaipata bado sababu ya kukasirikia wananchi wasioridhika na mfumo wa muungano. Hivi hutaki kujisikia raha kwa kuongoza watu ndani ya mfumo wanaoukubali? Nakusihi sasa, hasira zako ni hasara kwako!

Sunday, 20 May 2012

ATCL yaanza mchakato wa kupata ndege nyingine



Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi (katikati) akikata utepe kuzindua rasmi safari za ndege hiyo kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza wikendi hii.



 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) Paul Chizi akiongea na waandishi wa habari kwenye uwanja wa ndege wa Mwanza mara bada ya kuzindua safari za ndege mpya ya Shirika hilo aina ya Boeing 733-500 wikendi hii.



                       Ndege ya ATCL aina ya Boeing 737-500 inavyoonekana kwa mbele





                             Wahudumu wa ndege wa Shirika la ATCL wakipozi



Abiria wakishuka kwenye ndege aina ya Boeing 737-500 ya ATCL kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) wakati wa uzinduzi wa safari za ndege hiyo wikendi hii. Ndege hiyo itafanya safari za kila siku za Dar es Salaam-Kilimanjaro-Mwanza mara mbili kwa siku.
Na Mwandishi wetu.
MARA baada ya wiki moja tu baada ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) kupata ndege aina ya Boeing 737-500 iliyoanza rasmi safari za Dar es Salaam-Kilimaanjaro-Mwanza wikendi hii, Shirika hilo limeanza mchakato utakayoliwezesha kupata ndege nyingine kati ya wiki tatu au sita zijazo.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya safari hiyo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa ATCL Paul Chizi alisema shirika lake linatarajia kupata ndege nyingine aina ya Boeing ambayo italiwezesha shirika hilo kufanya safari za nje zikiwemo Dar es Salaam-Lusaka, Dar es Salaam-Harare and badae Dar es Salaam-Dubai.
“Tumeanza utekelezaji wa mpango kazi wetu wa muda mrefu ambao utatuwezesha kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.“Katika mpango wetu ,tunatarajia kupata ndege nyingi na bora zaidi. Kwakuanzia,tunarajia kupata ndege nyingine katika kipindi cha wiki tatu mpaka sita na ndege hiyo itatuwezesha kuanza safari za kimataifa,’ alisema Chizi.
Chizi aliwataka wananchi pamoja na mashirika mbalimbali kuunga mkono jitihada za Shirika lake na kuahidi kuwa shirika hilo litazingatia utoaji wa huduma bora kwa bei nafuu. “Mafanikio ya shirika yatategemea mchango wa wadau mbali mbali. Tunaomba wananchi watuunge mkono ilituweze kupata mafanikio zaidi,” alisema.
Chizi alisema kuwa katika wiki chache zilizopita kampuni yake ilizindua tovuti ambayo itasaidia katika kuboresha huduma ya ukataji tiketi kwa wateja kwa wakati wao na kuboresha utoaji huduma wa kampuni.
“Kitu cha kujivunia ni kuwa wateja sasa wanaweza kutaka tiketi kupitia mtandao bila kufika katika ofisi zetu au kupitia mawakala wetu kama ilivyo zamani,” alisema.
Nae Jaji Mstafu wa Mahakama Kuu ambaye alipata nafasi ya kusafiri kwa kutumia ndege mpya ya shirika hilo aliomba Serikali kutoa ruzuku kwa Shirika hilo na kusisitiza kuwa uboreshaji wa shirika hilio utaongeza pato la taifa kupitia sekta ya Utalii.
Maalim Seif awataka walimu wa vyuo kuimarisha elimu ya dini




Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akihutubia katika mahafali ya 14 ya Madrasat Nuur Islamiyat ya ukutani yaliyofanyika Skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar. Kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Sheikh Omar Othman Makungu na kushoto ni Mudir wa Madrasa hiyo ustadh Khalid Mohammed Mrisho.

   Baadhi ya wazazi, walezi na waalikwa mbali mbali wakihughuria maadhimisho ya sherehe ya Mahafali ya Madrasat Nuur yaliyofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.


Wanafunzi wa Madrasat Nuur Islamiya ya Ukutani Zanzibar wakisoma Kasida katika Mahafali ya Madrasa hiyo yaliyofanyika skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.


Wanafunzi wa kiume wa Madrasat Nuur Islamiya ya Ukutani Zanzibar wakisoma kasida katika sherehe za Mahafali ya Madrasa yao yaliofanyika katika Ukumbi wa Skuli ya Haile Sellassie mjini Zanzibar.


 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wahitimu (wanaume) wa madrasa hiyo.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Al-haj Maalim Seif Sharif Hamad amesema mafanikio yaliyopatikana katika chuo cha Madrasat Nuur Islamiya cha Ukutani Zanzibar ni neema kwa Wazanzibari wote na wanapaswa kuithamini na kuiendeleza neema hiyo. Amesema Madrasa hiyo ina historia ndefu ya kutoa wanazuoni na wasomi mbali mbali wa dini ya kiislamu na kusambaa katika nchi tofauti duniani, ambao husaidia harakati za kuiendeleza dini ya kiislamu.
Maalim Seif ametoa kauli hiyo leo alipokuwa akihutubia katika mahafali ya 14 ya na Madrasa hiyo yaliyofanyika Skuli ya Haileselassie mjini Zanzibar.
Amesema madrasa hiyo ni chemchem ya elimu ya dini ya kiislamu kwa Zanzibar na Afrika Mashariki kwa ujumla, na imetoa wanazuoni wengi wanaotajikana duniani tangu kuanzishwa kwake na Marehemu Sheikh Abdallah Bakathir mwaka 1967.
Makamu wa Kwanza wa Rais amewapongeza walimu wa madrasa hiyo kwa kusimama kidete katika kuendeleza mema yaliyoachwa na muanzilishi wa madrasa hiyo na kuzitaka madrasa nyengine kuiga mfano huo katika kujenga jamii yenye maadili bora.
Katika hatua nyengine Maalim Seif ametoa wito kwa jamii kushirikiana katika malezi ya watoto ili kurejesha malezi bora ambayo kwa kiasi kikubwa yanaonekana kupotea, sambamba na kuwahimiza watoto kutafuta elimu bila ya kubagua elimu ya dini na ile ya dunia.
“ Mazoweya ya wenye nacho kuwasaidia wanaohitaji yamepotea, heshima ya watoto kwa wazazi na jamii kwa ujumla imepungua sana” alikumbusha Maalim Seif.
Sambamba na hilo Maalim Seif amewataka wazazi na walezi kusimamia elimu ya mtoto wa kike kama ilivyo kwa watoto wa kiume, ili kusaidia kurejesha heshima na maendeleo kwa taifa.
“Kuna usemi kuwa unapomuelimisha mwanamke mmoja, unaelimisha jamii yote. Hivyo wazazi na walezi tujitahidi kuwaelimisha watoto wetu bila kubagua”, alisisitiza,
Katika risala ya wanafunzi hao iliyosomwa na mwanafunzi Abdulhalim Majid wamewaomba wazazi kuwa karibu zaidi na walimu, sambamba na kutoa kipaumbele kwa elimu ya akhera ambayo ni nuru katika maisha ya kila siku ya mwanadamu.
Mapema akitoa nasaha zake kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Mudiri wa madrasa hiyo ustadh Khalid Mohd Mrisho amesema lengo la kuandaa mahafali ni kuwashajiisha na kuwajengea ari zaidi wanafunzi, hali inayopelekea kuwa na ushindani mkubwa wa kimasomo.
Amefahamisha kuwa kwa sasa chuo hicho chenye wanafunzi 1300, kina mpango wa kuanzisha elimu ya Sekondari, ili kuwawezesha vijana kuielewa vyema dini yao, sambamba na kuwajengea uwezo katika masomo yao dunia.
Amesema licha ya mafanikio makubwa yaliyopatikana lakini chuo hicho bado kinakabiliwa na matatizo ya ufinyu wa nafasi pamoja na vifaa vya kusomea vikiwemo kompyuta, hali inayowafanya kuchukua wanafunzi mara moja tu kwa mwaka.
Katika mahafali hayo Makamu wa Kwanza wa Rais ameahidi kuchangia shilingi milioni moja pamoja na komputa tatu kwa ajili ya kusaidia maendeleo ya madrasa hiyo.
Mahafali hayo ya Madrasat Nuur Islamiya ya Ukutani Zanzibar, yamehudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo Jaji Mkuu Sheikh Omar Othman Makungu na Naibu Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Hassan Ngwali