Ubalozi wa Tanzania nchini Misri wafungwa
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Hosni Mubarak ajiuzulu wadhfa wa chama chake
Serikali imetangaza kufunga ubalozi wa Tanzania nchini Misri kwa muda usiojulikana na kwamba kwa sasa inafikiria kukodi ndege ili izirejeshe familia za maofisa kwenye ubalozi huo.
Akizungumza na waandishi wa habari mjini hapa baada ya kuteta na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), tawi ya UDOM, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, alisema wizara yake imelazimika kufunga ubalozi huo kufuatia maandamano yanayoendelea nchini humo kwa siku ya 13 hadi leo.
Alisema Rais Jakaya Kikwete ameagiza kufungwa kwa ubalozi huo na kuagiza kurejeshwa nchini kwa maofisa wa ubalozi na wanafunzi 80 wanaosoma nchini humo.
Wakati huo huo, kabla ya gazeti kwenda mitamboni, televisheni ya Taifa nchini Misri, jana jioni iliripoti kwamba Rais Hosni Mubarak, amejiuzulu wadhifa wa uongozi ndani ya chama tawala.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
No comments:
Post a Comment