Wednesday, 2 February 2011

Noti mpya ya Sh5000yazua balaa Dar

  
Mariam Sagafu, MUM
NOTI mpya ya Sh5,000  juzi ilisababisha balaa baada ya mwanamke mmoja aliyenunua nguo kwa machinga katika Soko la Karume jijini Dar es Salaam, kupigwa na kujeruhiwa vibaya.

Hawa Hassan alifikwa na mkasa huo juzi sokoni hapo baada ya kumpa noti hiyo mmachinga ambaye jina lake halikufahamika mara moja kulipia nguo aliyonunua.“Mimi sijui kama pesa hii ni bandia kwani nimerudishiwa kwenye daladala,” alisema Hawa.
Hawa aliongeza kuwa “Ninapigwa lakini mimi sina kosa lolote kwani hizo fedha zipo mitaani na siku zote tunazitumia halafu leo hii naambiwa eti fedha hii si halali.”Hili ni tukio la pili kutokea katika kipindi cha mwezi mmoja.

Ijumaa iliyopita, mama mmoja aliitwa mwizi baada ya kutoa noti ya Sh500 alipokuwa akinunua chakula kwenye duka la chakula katika soko la Tandika.

Baada ya mama huyo kutoa noti ya Sh500  mmiliki wa duka hilo akishirikiana na wananchi walianza kumshambulia kwa kumpiga wakidai fedha hiyo siyo halali.

Mfanyabiashara Joseph Katundu ambaye ni mfanyabiashara sokoni hapo alisema wao si rahisi kuwapa pesa bandia kwani wamekuwa makini sana hasa kwa pesa hizi mpya kwani kuna watu wana imani pesa hizi mpya hazipo bandia na ndio maana wanabambikizwa.
Hata hivyo Mkuu wa kituo cha polisi Chang’ombe ACP  Samuel Bunda alisema  hana taarifa za tukio hiloJuzi tukio kama hilo lilitokea katika soko la Karume, Ilala jijini Dar es Salaam, ambapo mfanyabiashara huyo wa nguo  (Machinga ) alimshushia mteja kipigo baada ya kupewa noti mpya ya Sh5,000 ambayo mfanyabiashara huyo alidai ni feki.
Kituko hicho kiliwavuta wananchi mbalimbali na kuleta mkusanyiko mkubwa katika eneo hilo maarufu kwa biashara za mitumba.

No comments:

Post a Comment