Andrew Msechu na Mshirika ILIANZIA Tunisia, sasa ni nchini Misri, ambako waandamanaji zaidi ya milioni mbili wamekusanyika katika miji mikubwa wakitaka kuondoka madarakani kwa Rais Hosni Mubarak, kama alivyoondoka Rais Ben Ali aliyelazimika kukimbilia uhamishoni nchini Saudia. Jeshi nchini Misri limechagiza msimamo wa waandamanaji hao kutokana na kuweka wazi msimamo wake kwamba “halitatumia silaha za moto kuwanyamazisha mamilioni ya waandamanaji”. Kwa pamoja, wanafunzi, madaktari na wafanyabiashara na watu masikini wasio na kazi maalum zaidi ya milioni moja walianza siku maalum iliyopewa jina la “Maandamano ya Watu milioni moja” mjini Cairo, wakibeba mabango yaliyoandikwa “Kwaheri Mubarak” huku wakiimba nyimbo za kumdhihaki na kumtaka kiongozi huyo mkongwe akamatwe. Katika miji ya Alexandria na Suez, hali kadhalika waandamanaji kwa pamoja walikuwa wakiimba: “Ondoka, ondoka. Mapinduzi, mapinduzi” wakikataa kabisa hatua alizochukua za kuvunja Serikali ya awali na kuunda Serikali mpya. Maandamano hayo makubwa kabisa kuwahi kutokea nchini humo yanamweka katika nafasi ya kutokuwa na chaguo Mubarak (82), ambaye amedumu madarakani kwa miaka 30 sasa, yakiripotiwa kusababisha vifo vya zaidi ya watu 140 waliokuwa wakipambana na askari polisi wiki iliyopita. Akizungumza kuhusu msimamo wa wapinzani, mkuu wa zamani wa shirika la Atomoiki la Umoja wa Mataifa na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Mohamed El Baradei alisema Mubarak hana budi kuondoka nchini humo kabla wanamageuzi hawajaanza majadiliano juu ya utekelezaji wa mahitaji ya umma, hasa kuhusu uundwaji wa Serikali. “Kutakuwana majadiliano, lakini yatafanyika mara tu mahitaji ya umma yatakapotekelezwa, la kwanza ni hili kwamba lazima Rais Mubarak aondoke,” alisema. Mubarak, mshirika wa siku nyingi wa Marekani amekuwa katika shinikizo la wiki nzima sasa kumtaka aondoke madarakani, wakati muungano wa vyama vya siasa kikiwemo chama kikuu cha upinzani cha Muslim Brotherhood vimekuwa katika msimamo mmoja, “Mubarak aondoke”. Tayari mataifa mengi ya magharibi, ikiwemo Marekani yenyewe imeamuru raia wake waondoke nchini Misri ili kuepuka umwagaji damu unaohofiwa kuwa huenda ukaendeela kutokea. Waandamanaji hao wameapa kutoondoka katika viwanja walivyokusanyika hadi matakwa yao yatimwizwe, huku shughuli zote za kiuchumi zikiwa zimesimama, maduka na ofisi zote za Serikali zikilazimika kufungwa pia. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Wednesday, 2 February 2011
Misri hakukaliki, hali yazidi kuwa tete
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment