Friday, 4 February 2011

Makampuni ya Simu Yagoma Kudhamini Maridhiano Cup

         seif&karume
Na Salma Said 
BAADHI ya makampuni ya simu za mikononi yaliopo nchini tamekataa kudhamini michuano ya kombe la maridhiano yaliopangwa kufanyika leo Zanzibar yakiwa na lengo la kuimaridha umoja na mshikamano uliopo nchini baada ya kuafikiwa kwa maridhiano ya kisiasa ya mwaka juzi hapa nchini.
Kombe hilo ni hatua moja ya kutilia nguvu umoja na mshikamano kwa wananchi wote Zanzibar ambapo vijana wameandaa mashindano ya mpira wa miguu kwa lengo la kuhamasisha maridhiano yalofikiwa mwishoni mwa mwaka juzi ambayo yamepewa jina la Kombe la Maridhiano.
Makampuni ya simu yalikataa mashindano hayo ni Zantel na Tigo ambayo yote mawili kwa mujibu wa maafisa uhusiano wao wamesema hawawezi kudhamini wala kuchangia mashindano hayo kwa kuwa yana mrengo wa kisiasa na wao hawachangii mambo ya siasa katika misaada yao .
Mashindano hayo ambayo yataanza leo yatafanyika uwanja wa Amani Mjini Unguja yanatarajiwa kufunguliwa na Makamu wa kwanza wa Rais, Maalim Seif Sharif Hamad na kufungwa na Rais Mstaafu Amani Abeid Karume viongozi ambao ni waanzilishi wa maridhiano hayo.
Pambano lakufungua dimba katika michuano hiyo, limepangwa kuzikutanisha timu za kombani za Wilaya za Mjini na ndugu zao wa Magharibi ambazo zitaundwa na Vijana wa Vyama vya CCM na CUF.
Kwa mujibu wa kamati ya mashindano hayo ambayo ina wajumbe saba akiwemo mweyekiti Suleiman Aboud (CCM) Katibu Shaaban Iddi (CUF) mashika fedha Aisha Mohamme (CUF) na wajumbe wanne ambao ni Kombo Mwinyi na Abeid Mohammed wote ni CUF na upande wa CCM ni Burhan Ali na Ali AbdulGulam.
Akizungumza na kamati inayoratibu michuano hiyo ofisini kwake Migombani, Maalim Seif amesema lengo la mashindano hayo ni kuendeleza mshikamano na amekusudia kuyafanikisha mashindano hayo hivyo amewasiliana na wa Soka waishio Dar es Salaam ili kutoa michango yao itakayosaidia kufanikisha mashindano hayo ambapo tayari wameitikia wito huo.
Wadau walioitikia wito wa kusaidia mashindano hayo ni pamoja na marafiki wa Simba na wadau wa bodi ya wadhamini wa Yanga ambapo kwa pamoja wametoa vifaa ikwemo viatu, mipira, jezi na vitu vyengine mbali mbali ambayo vyenye thamani ya shilingi millioni 12.
Maalim Seif amewaeleza wajumbe hao kuwa ni muhimu kwa maridhiano yaliopo kulindwa na kuwataka wanamichezo nchini kuachana nakasumba zilizopita na kuamini kuwa mgongano wa mawazo katika nchi ndio chachu katika kukuza demkrasia.
Hata hivyo Maalim Seif alieleza kufurahishwa kwake na hatua ya vijana wa vyama vya CCM na CUF kufikiria kuanzisha mashindano hayo, na kuwasifia kwa kuwa waumini wa kweli wa mabadiliko na wenye kupenda demokrasia na kuwataka wananchi wengine kuiga mfano huo kwa kuwa jambo hilo litawaezesha vijana kuachana na tabia ya kufanyiana chuki za kisiasa.
“Michuano hii ni muhimu kwani inalenga kukuza umoja na mshikamano miongoni mwa wazanzibari, na ni hatua njema katika kufikia maendeleo ya haraka’’, aliifafanua Maalim Seif.
Awali Katibu wa kamati inayoratibu michuano hiyo Shaaban Iddi alisema mashindano hayo yanalenga kuimarisha maridhiano yaliyofikiwa, ili kuendeleza umoja na mshikamano miongoni mwa wazanzibari ambao kwa miongo kadhaa wamekuwa wakiishi kwa chuki.
Kombe la michuano hiyo limetengenezwa kwa umbo lenye sura ya umoja, likiwa na picha mbili za Rais mstaafu Amani Abeid Karume katika pembe ya kulia, na upande wa kushoto itaonekana sura ya makamu wa kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif Hamad

No comments:

Post a Comment