Tausi Ally SHAHIDI wa tano wa upande wa mashtaka, Inspekta Anthony Mwita (45), katika kesi inayomkabili mtangazaji wa TBC, Jerry Muro, jana aliiambia Mahakama kuwa mshtakiwa huyo aliwahi kumkabidhi stakabadhi ya pingu aliyoinunua katika duka la Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Upanga, jijini Dar es Salaam.Mwita alitoa madai hayo mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama Kisutu jijini Dar es Salaam, Gabriel Mirumbe alipokuwa akitoa ushahidi wake katika kesi inayomkabili Muro na wenzake Deogratius Mgasa na Edmund Kapama. Kabla Mwita kutoa ushahidi wake alitanguliwa na Inspekta Msaidizi wa Polisi, Issa Seleman (37), aliyeieleza Mahakama jinsi alivyoweka mtego na kufanikisha kumkamata Muro. Katika ushahidi wake, Mwita alidai kuwa Muro aliwahi kumkabidhi stakabadhi ya kununulia pingu yenye namba 34357310 inayoonyesha kwamba ilinunuliwa kwa Sh 25,000 katika duka la Jeshi lililopo Upanga Mei 26, 2009. “Nilifika Upanga katika duka hilo ili kupata uthibitisho kama risiti hiyo kweli ni ya kwao, walinithibitishia ni kweli walimuuzia pingu hiyo,” alidai Inspekta Mwita. Awali shahidi huyo wa upande wa mashtaka, alidai mahakamani hapo kuwa Februari 2, 2010 alienda katika Hoteli ya Sea Cliff kuonana na Meneja wa kitengo cha mawasiliano cha hoteli hiyo ili awapatie picha za CCTV za watu waliongia na kutoka Januari 29, 2010. Shahidi huyo pia alidai kuwa alichukua kitabu cha kumbukumbu cha usajili wa magari yanayoingia na kutoka katika hoteli hiyo ya Sea Cliff kutoka kwa mlinzi wa kampuni ya ulinzi ya KK Security, Briton Banyika ambaye alikuwepo kazini Januari 29, 2010 kuanzia saa 12 asubuhi hadi saa 12 jioni. Alidai alikipata kitabu hicho, ambacho kilikuwa na kumbukumbu ya usajili wa gari la Muro aina ya Cresta ambalo lilipewa kadi namba 673 ya hoteli hiyo ambalo liliingia saa 7:33 mchana na kutoka saa 8:48 mchana. Akitoa ushahidi wake, Inspekta Msaidizi wa Polisi, Issa Seleman (37) aliieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jinsi alivyoweka mtego na kufanikiwa kumkamata Jerry Muro katika Hoteli ya City Garden kutokana na tuhuma za kutishia na kuomba rushwa ya Sh10 milioni. Akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Boniface Stanslaus kutoa ushahidi wake, Seleman alidai kuwa Januari 30, mwaka 2010, saa 4 asubuhi akiwa kwenye kazi zake za nje za kipolisi alipokea simu kutoka kwa Sajini Gervas ikimtaarifu kuwa kuna watu wamemtishia Mhasibu wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Wage na kumuomba rushwa ya Sh10 milioni. Alidai kuwa baada ya kupata taarifa hiyo alikwenda ofisini kwao na kumkuta Sajini Gervas akiwa na Wage ambaye alimueleza malalamiko yake ya kutishiwa na kuombwa rushwa ya Sh10 milioni na Muro. Aliongeza kudai kuwa baada ya kuyasikiliza malalamiko hayo, aliwasiliana na viongozi wake akiwemo Mkuu wa Upelelezi Mkoa wa Ilala, SSP Duwan Nyanda ambaye alimuamuru kufungua jalada la uchunguzi na utaratibu wa kuwakamata kina Muro ufuate. “Nilifungua jalada hilo la uchunguzi na nilimuomba Wage awasiliane na watu waliomtisha na kumuomba rushwa mbele yetu,”alidai Seleman. Alidai kuwa Wage aliwaambia kuwa anawasiliana na Muro na kuwa amemwambia wakutane katika geti la TBC, lakini akabisha na kumtaka wakutane Bamaga. “Nilimwambia Wage ampigie Muro amwambie kuwa wakutane kesho yake yaani Januari 31, 2010 saa 4 asubuhi katika Hoteli ya City Garden. Siku hiyo ilipofika mimi kama inspekta wa zamu, niliamuru Sajini Omar na Koplo Masaka wakae nje ya hoteli na mimi na Sajenti Gervas tulibakia ndani ya hoteli hiyo,”alidai. Alidai kuwa nyakati za saa 6 mchana, Muro aliwasili hotelini hapo na kumtaka Wage atoke nje ya hoteli hiyo ili waonane na kwamba iliwabidi wao wajipange kwa kutumia ishara. “Wage alibeba 'sweetcase' (mkoba) kutaka kuingia ndani ya gari la Muro, lakini kabla hajaingia nilimuamuru ashuke na nikamuuliza Muro kama anamfahamu Wage,”alidai shahidi huyo. Aliendelea kudai kuwa Muro alijibu kuwa hamjui, lakini Wage alidai anamfahamu Muro na ni moja kati ya watu waliokuwa wakimtisha na kumuomba rushwa na kwamba yeye hakuwahi kumhoji Muro wala kumpekua katika gari yake. Kesi hiyo itaendelea kusikilizwa leo. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Wednesday, 26 January 2011
Shahidi: Jerry Muro alinunua pingu duka la JWTZ
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment