Wednesday, 26 January 2011

Kutoka Barazani

 
milioni Sh 81 kukarabati nyumba ya wazee Zanzibar
Salma Said,  Zanzibar

SERIKALI YA Zanzibar inakusudia kutumia Sh 81 milioni kwa ajili ya kukarabati  nyumba ya Wazee Sebuleni baada ya kuungua moto paa la nyumba  hiyo.
Waziri wa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Vijana, Wanawake na watoto,  Zainab Mohammedalisemahayo alipokuwa akijibu suali la Mwakilishi wa Jimbo la Mwajuni Mbarouk Wadi Mussa (Mtando), aliyetaka kujua ni kiasi gani cha fedha kinachotarajiwa kutumika kwa ajili ya kufanya marekebisho ya nyumba hiyo.

Alisema fedha hizo serikali inatarajia kuzitumia kwa ajili ya kufanya marekebisho hayo ikiwa ni hatua muhimu itayoweza kurejesha uasilia wa nyumba hiyo.

 Waziri huyo akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Magogoni,  Salmini  Awadh Salmin, aliyetaka kujua hatua ilizozifikia katika kukarasbati nyumba hiyo, alisema ukarabati wa nyumba hiyo utahitaji kutumia Sh 80 ambapo makisio hayo yanatarajiwa kuwasilishwa serikalini ili kuweza kupatiwa fedha hizo kufanikisha ujenzi huo.

Wakati huo huo serikali imekusudia kutekeleza sera ya dawa ambayo inahimiza kuwepo kwa viwanda vya dawa nchini.

Mpango huo wa utekelezaji wa sera ya dawa wa 2008-2012 ambao unahimiza kuwepo kwa viwanda vya dawa kutokana na viwanda hivyo kuhitaji utaalamu mkubwa na wizara ilianzisha mafunzo ya ufundi sanifu wa dawa katika chuo cha afya Mbweni mwaka 2009 .

Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Dk Sira Mamboyo

katika kikao cha baraza la wawakilishi wakati akijibu suali la mwakilishi wa Jimbo la Magomeni (CCM) Salmin Awadh Salmin.

Alisema  hatua hiyo itaongeza ufanisi katika utoaji wa huduma hospitalini pia kuwarahisishia wenye nia ya kuanzisha viwanda vya dawa hapa Zanzibar chini ya utekelezaji wa mpango wa utengenezaji wa dawa kwa kipindi cha 2010-2016.

 Katika miaka ya 80 kwa msaada wa UNIDO Serikali ilijenga kiwanda cha

dawa kilichokuwa kikitengeneza dawa za vidonge na maji ambapo kilibinafsishwa kwa mwekezaji ambaye baadaye alikirejesha kwa Wizara hiyo ya Afya.

 Hata hivyo alisema kuwa Wizara ina mpango wa kulitumia jengo hilo kwa

upanuzi wa Hospitali ya Mnazimmoja kujumuisha sehemu ya kupokelea wagonjwa wa dharura, sehemu ya wagonjwa wa nje na wodi ya watoto.

No comments:

Post a Comment