Hukumu ya Mwanangu Namuachia Subhanna-Mama Ghailan
Na Salma Said
KUFUATIA hukumu ya kifungo cha maisha cha Mtanzania, Ahmed Ghailan, Mama Mzazi wa kijana huyo, Bimkubwa Suleiman amesema hawezi kuongea chochote kwa kuwa hali yake sio nzuri kutokana na hukumu hiyo ya mwanawe.
Bimkubwa ambaye amekuwa akifuatilia hukumu ya mwanawe huyo jana alionekana akiwa na simanzi kubwa na kushindwa kuzungumza tofauti na siku moja iliyopita ambapo alisema chochote kitakachoamuliwa na mahakama hiyo kitakuwa kimeshapangwa na Mwenyeenzi Mugu na hakuna wa kuweza kukipangua.
Mama huyo ambaye amekuwa akipewa pole na ndugu, jamaa na majirani amesema hukumu iliyotolewa kwa mwanawe anamuachia Mungu kwa kuwa yeye ndio hakimu wa kweli kuliko mahakimu wote hivyo hana la kusema zaidi ya kusema kumshukuru Mungu kutokana na hukumu hiyo.
“Sina la kusema zaidi ya kusema Alhamdulillah ‘Thanks God’, kwa sababu chochote kitakachotokea na kilichotokea ni mipango yake mwenyewe Subhana sina zaidi ya kumshukuru na kumuomba Mwenyeenzi Mungu anipe subra mimi na mwanangu inshaallah na hayo yaliomfika ni mipango ya Mungu mwenyewe” alisema kwa huzuni Mama Ghailani.
Alisema amesikitishwa kwa kuwa hajenda kumuona mwanawe lakini hata angekwenda hangeweza kuona na kusikia hukumu mbaya dhidi ya mwanawe ikitolewa na yeye yupo hapo hapo.
Babu wa Ghailan, Maalim Seif Nassor kwa upande wake amesema kitendo cha mjukuu wake kukubali kosa ni madhila yasiokwisha juu yake kwani kufanya hivyo kutamsababishia kupata mateso ya maisha akiwa gerezani huko Marekani.
Mimi naona hukumu ni ngumu sana kwake na kwetu sisi wazee wetu na huko kukubali kwake makosa ni mateso yake ya maisha” alisema Babu huyo na kuongeza kwamba.
“Kifungo cha maisha, mimi naona ajabu sana kesi yenye masuala 200 bora auliwe kabisa” alisema kwa hasira.
Maalim Seif alisema kitendo cha Ghailan kukubali kosa na kupitishwa hukumu ya kifungo cha maisha kutaifanya familia yake isionane tena na mtoto wao huyo.
“Ahhh tutakufa hatuonani tena maana ndio ishatokea sisi tutaondoka duniani hatuonani tena lakini walioo labda watamuona lakini sisi tena ndio tunasema basi kuonana na Ahmed” alisema huku akilia.
Katika hatua nyengine babu wa Ghalan ameitupia lawama serikali ya Tanzania na ile ya Zanzibar kwa kushindwa kufanya lolote tokea kutokea kwa tukio hilo licha ya kuwa wanafahamu kuwa huyo ni raia wa nchi yao.
“Mimi nailaumu serikali na viongozi huyo Kikwete na huyo Dk Shein wameshindwa kuja kutuona hata mara moja miaka yote hata kutuletea ile salamu kwamba tusubiri hukumu itolewe” alisema Babu huyo

No comments:
Post a Comment