Na Salma Said
Zanzibar yetu
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa India na Zanzibar zina maeneo mengi ya kushirikiana pamoja katika kuimarisha sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya afya kutokana na nchi hiyo kupiga hatua.
Dk. Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi mdogo wa India anaefanya kazi zake hapa Zanzibar, Dalip Sigh Singal, aliyefika Ikulu mjini Zanzibar kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Rais.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Singal kuwa India imepata mafanikio makubwa katika uimarishaji wa sekta ya afya na kueleza kuwa kupatikana kwa wataalamu wa sekta ya afya kuja kutoa huduma hapa Zanzibar kutasaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha sekta hiyo.
Alieleza kuwa kuna umuhimu mkubwa wa kupata wataalamu wa sekta ya afya ambao watasaidia kuimarisha na kuanzisha vitengo vya maradhi mbali mbali yakiwemo maradhi ya moyo, figo na saratani katika hospitali kuu ya MnaziMmoja.
Aidha, Dk. Shein alieleza kuwa kufanikiwa kwa vitengo hivyo katika hospitali kuu ya MnaziMmoja kutasaidia kwa kiasi kikubwa kutoa huduma kwa wananchi na kuepuka gharama kubwa inayotumika kwa kuwasafirisha wagonjwa kuwapeleka nje ya nchi ikiwemo India.
Pia, alieleza kuwa hatua hiyo ya kuja kwa wataalamu kutoka nchini India kutasaidia kwa kwa kiasi kikubwa kutoa huduma na utaalamu kwa madaktari wazalendo ili nao waweze kusaidia huduma kwa wananchi wa Zanzibar kwa ufanisi zaidi juu ya maradhi hayo.
Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati ya nchi mbili hizo, na kutoa shukurani kwa misaada inayotolewa na India pamoja na kusisitiza kuwa Zanzibar itaendelea kuudumisha kwa madhumuni ya kupata mafanikio zaidi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Singal kuwa Zanzibar ina maeneo mengi ya uekezaji hivyo ipo haja kwa waekezaji na wafanyabiashara wa India kuja kuekeza Zanzibar.
Pia, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa kwa upande wa sekta ya utalii, Zanzibar imepiga hatua kubwa na hivyo ipo haja kwa waekezaji wa nchi hiyo kuja kuekeza Zanzibar katika sekta ya utalii.
Dk. Shein alimueleza Balozi Singal kuwa Zanzibar na India zina maeneo mengi ya kushirikiano ikiwemo pia, sekta ya Kilimo na kusisitiza uendelezaji mashirikiano katika sekta ya elimu.
Nae Balozi mdogo wa India anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Mhe. Dalip Sigh Singal alieleza kuwa alitoa pongezi zake kwa Zanzibar kwa kufanya uchaguzi kwa amani na utulivu, uchaguzi ambao ulikuwa huru na wa haki.
Balozi Singal alisema kuwa India inajivunia uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati yake na Zanzibar ambao umeweza kupata mafanikio makubwa ya kimashirikiano na kusifu mafanikio yaliopatikana Zanzibar kisiasa.
Alieleza kuwa wananchi walio wengi kutoka Zanzibar wamekuwa wakipata huduma za afya nchini India kutokana na nchi hiyo kupiga hatua katika sekta ya afya hivyo kuna haja ya kushirikiana pamoja ili huduma hiyo iendelee kutolewa kwa ufanisi zaidi kwa wananchi wa Zanzibar.
Alisema kuwa nchi yake inamatumaini makubwa ya mafanikio ya kiuchumi, kijamii na kisiasa chini ya uongozi wa Dk. Shein.
Balozi Singal alimueleza Dk. Shein kuwa yeye mwenyewe binafsi atachukua juhudi za kuhakikisha anakutana na Waziri wa Afya wa nchi hiyo kwa lengo la kuzungumza juu ya mashirikiano ya uimarishaji wa sekta ya afya hapa Zanzibar hasa kuhusu wataalamu katika uimarishaji wa vitengo vya maradhi ya moyo, figo na saratani.
Balozi huyo wa India alisema kuwa nchi yake itaendelea kutoa nafasi za masomo kwa Wazanzibar watakaokwenda nchini humo kujifunza kada mbali mbali.
Aidha, Balozi Singal alisema kuwa sekta ya biashara nayo imepata nafasi kubwa kwani wafanyabiashara wengi wa Zanzibar wamekuwa wakifanya biashara zao nchini India na kutoa fursa nzuri ya kibiashara.
Balozi huyo pia, alimueleza Dk. Shein amani na utulivu uliopo Zanzibar ni hatua moja wapo iliyowafanya wananachi wengi kutoa nchi hiyo kuja kuishi Zanzibar miaka mingi iliyopita ambapo India ilianzisha Ubalozi wake hapa Zanzibar mnamo mwaka 1974.

No comments:
Post a Comment