Dk Shein Atoa Mkono wa Pole
Na Salma Said, ZanzibarRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein amewapa mkono wa pole wananchi na wanaCCM waliopata ajali ya gari huko Jambiani wakiwa njiani kuhudhuria mkutano wa mwisho wa CCM wa ufungaji kampeni za uchaguzi uliopita.
Akizungumza na wananchi hao, huko Jambiani Mfumbwi, Shehia ya Jambiani Kikadini, Dk. Shein aliwapa pole wale wote waliopata ajali hiyo na kuwaombea kwa MwenyeziMungu wale ambao wamepoteza maisha yao na kuwataka ndugu na jamaa wa marehemu kuwa na subira.
Katika mazungumzo yake Dk. Shein aliwataka wananchi hao wa Jambiani pamoja na wananchi wengine wa Zanzibar kwa jumla kuishi kwa umoja na mshikamano na kusaidiana katika shughuli zote za kimaendeleo na kijamii na kusisitiza kuwa ajali hiyo iliyotokea ni miongoni mwa rehema za Mwenyezi Mungu (SW).
Dk. Shein ambaye alifuatana na Mama Mwanamwema Shein katika ziara yake hiyo, aliwaeleza wananchi hao kuwa ajali hiyo iliowakutia wanaCCM hao ni ishara tosha inayoonesha kuwa walikuwa wakienda kukiunga mkono kwa vitendo chama chao safari ambayo waliifanya kwa mapenzi makubwa ya chama chao.
“Nawapa pole wale wote walipata ajali hiyo, tuko pamoja na nyinyi, tulikuwa karibu wakati wa tukio lilipotokea na tutaendelea kuwa nanyi katika muda wote…”,alisema Dk Shein.
Aidha, Dk. Shein alitoa Shukurani kwa wanachama wote wa CCM na wale wasiokuwa wanachama wa CCM wa Jimbo la Muyuni, Mkoa wa Kusini Unguja kwa kuendelea kukiunga mkono chama chao na hatimae kikapata ushindi mkubwa katika uchaguzi huo mkuu uliopita, uchaguzi uliompelekea yeye kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi.
Aliwaeleza wananchi hao kuwa jambo kubwa la kumshukuru MwenyeziMungu ni kuwa nchi yao inaendelea kuwa ni ya amani na utulivu.
Alisema kuwa amani, mshikamano ndio jambo kubwa katika kujenga nchi na kuleta maendeleo endeleo.
Kutokana na hatua hiyo, Dk. Shein aliwasisitiza wananchi kuendelea kuitunza amani, utulivu pamoja na mshikamano uliopo kwani ndio njia pekee ya kuendeleza nchi.
Dk. Shein alisisitiza kuwa amani na umoja yaende sambamba na kuwaombea dua wale wote waliopata ajali hiyo. “Waliopoteza roho zao tumuombe MwenyeziMungu awaweke mahali pema pemoni na wale walioumia MwenyeziMungu aendelee kuwaponya haraka lakini jambo kubwa tusisahau kusaidiana kwani sote sisi ni ndugu”,alisema Dk. Shein.
Nao wazee,vijana na wanachama wa CCM waliopata ajali hiyo walitoa shukurani zao kwa Rais Dk. Shein kwa ziara yake hiyo na kutoa shukurani zao kwa uongozi wa CCM kwa kuendelea kuwajali na kuwa karibu nao katika kipindi chote.
Kwa niaba ya wazazi wa watoto waliopata ajali hiyo bwana Hassan Haji alitoa maelezo mafupi na kutoa shukurani hizo kwa Dk. Shein na kuendelea kumshukuru kwa kwenda kijijini hapo yeye na Mama Mwanamwema kwa ajili ya kuwapa mkono wa pole.
WanaCCM, wazee na vijana wa Shehia ya Jambiani Kikadini wapatao 76 walipata ajali mnamo tarehe 30 mwezi wa Oktoba mwaka jana wakati wakija mjini kuhudhuria mkutano wa mwisho wa ufungaji wa kampeni za Chama Cha Mapinduzi za kujiandaa na uchaguzi mkuu uliopita.
Katika ajali hiyo wanachama watatu walipoteza maisha yao na wengine kuumia vibaya na kulazwa katika hospitali ya MnaziMmoja ambapo wengine walipata majeraha na miongoni mwao waliruhusiwa kurudi nyumbani.
Wakati huo huo, Dk Shein alipokuwa akielekea Jambiani alipita katika kijiji cha Paje na kuangalia shughuli za matayarisho ya Ijtimai ya Kitaifa inayotarajiwa kufanyika kijijini hapo mwezi ujao.
Akiwa katika viwanja vinavyotarajiwa kufanyika Ijtimai hiyo, Dk. Shein alipata maelezo juu ya shughuli zinavyokwenda katika matayarisho ya Ijtimai hiyo.

No comments:
Post a Comment