Taasisi ya Sayansi za Bahari Ipewe Hadhi ya Chuo Kikuu
MAKAMU wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amesema ipo haja kwa serikali kufikiria upya juu ya Taasisi za Sayansi ya Bahari Zanzibar kuwa na hadhi ya Chuo Kikuu kamili kinachojitegemea.
Maalim Seif ametoa ushauri huo jana wakati akifungua sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya cha Dar es Salaam, (UDSM) sherehe zilizofanyika katika jengo la Taasisi ya Sayansi za Bahari Malindi Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja.
“Ni miaka zaidi ya thelathini tangu taasisi hii kuanza kufanya kazi zake hapa Zanzibar. Ni wakati sasa kwa chuo cha dare s salaam kuigeuza taasisi hii na kuifanya kuwa chuo kikuu cha mambo ya bahari. Tumeyaona hayo kwa MUHAS na ARU” amesema Maalim Seif ambapo nae ni miongoni mwa wahitumu waliowacha rekodi nzuri katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam wa mwaka mnamo 1975 katika fani ya sayansi na siasa(Political Science).
Alisema Taasisi hiyo iwapo itapewa hadhi ya chuo kikuu kamili itasaidia kuongeza fursa ya elimu ya chuo kikuu kwa vijana nchini katika nyanja za elimu ya sayansi za bahari ambapo Zanzibar uchumi wake kwa njia moja au nyengine unategemea sana habari.
“Ni wazi basi nchi hii inahitaji wataalamu wengi wa elimu hizi. Ni mategemeo yangu kwamba katika siku za karibuni taasisi hii itafanya juhudi maalumu za kupata wanafunzi wengi sana kutoka visiwa hivi. Sambamba na hilo ni mategemeo yangu pia kuwa taasisi hii itachukua hatua za makusudi ili kuona kuwa idadi ya watafiti wanafanya kazi humu kutoka hapa Zanzibar inaongezeka ili watusaidie katika kueneza elimu hii muhimu kwa wananchi kwa haraka” alisema Maalim Seif.
Kazi za utafiti zinazofanywa na taasisi hiyo, Maalim Seif alisema matokeo yake ni muhimu kwa sababu yanasaidia serikali katika uwekaji wa sera za utunzaji wa mazingira na mtumizi endelevu ya raslimali katika bahari ya Zanzibar .
“Visiwa kama Zanzibar vinakabiliwa na tishio la baadhi ya sehemu yake kumezwa na bahari kutokana na ongezeko la kiwango cha maji kinachosababishwa na kuyeyuka kwa mapande ya bahari kaskazini na kusini mwa dunia,” alisema Maalim Seif
Aidha kuna haja ya kuzingatia kwa kuwa visiwa vya Zanzibar vinakabiliwa na tishio la kumezwa baadhi ya sehemu zake kutokana na ongezeko la kiwango cha maji kutokana na kuyeyuka kwa mapande ya barafu kazkazini na kusini kabisa ya dunia ambapo alisema ni vyema tafiti za chuo hicho zilenge juu ya kukabiliana na maangamizi ya aina hiyo.
Alisema ni jambo gumu lakini ni changamoto ambayo inaweza kuchukuliwa hatua ambapo aliwasihi watafiti wa chuo hicho kufanya tafiti zao zitakazolenga kunyanyua uwezo wa kiuchumi wa wananchi wa pwani ili ziwe ni njia mbadala za kuzuwia matumizi mabaya ya bahari na fukwe nchini.
“Tuunganisheni utaalamu wa kisosiologia, uchumi na sayansi katika kufika hatua hiyo. Pamoja na tafiti hizo nakuombeni pia mfikirie juu ya tafiti za kuoneza thamani za mazao ya bahari ili yalete tija zaidi kwa wananchi. Wakati njia zetu za kuhifadhi samaki nyingi ni za kizamani wenzetu wa Asia ya kusini wananjia kadhaa za kuhifadhia samaki, hasa wanaovuliwa kwa wingi kama dagaa, na kuzalisha bidhaa kadhaa ambazo ni nzuri na kwa chakula. Samaki wetu hatujawatumia vizuri. Tusaidieni” alisisitiza Maalim Seif.
Mapendekezo ya serikali ya Zanzibar kutaka Taasisi ya Sayansi za Bahari kuwa na hadi kamili ya chuo kikuu, Tanzania itakuwa na vyuo vikuu vine ambavyo vimetokana na taasisi tanzu za Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Maalim Seif alisema chuo kinapofikisha miaka 50 huwa kimeshafanya mambo mengi hivyo taasisi ya sayansi za bahari nayo ina mengi ambayo kitapenda yatekeleze ambapo aliahidi serikali kutoa ushirikiano wa dhati kuifanikisha mipango ya chuo hicho kulingana na uwezo wa fedha na vipaumbele vya kitaifa.
Alisema kwamba dunia imekumbwa na balaa kubwa la mabadiliko ya hali ya hewa yaliotokana na ongezeko la joto duniani ambapo majanga ya yaliotokea 1997/98 ya El-Nino na athari iliyoleta katika viumbe vya bahari.
“Tunaelewa kwamba kuna maeneo ambayo hali yake ya kimaumbile imebadilika sana na itachukua miaka kadhaa kurudi, na hakuna uhakika kama itarudi katika utando wake wa asili. Hali hii haijamalizika na inaweza kutokea tena wakati wowote. Tujiandae. Nawaomba sana tafiti zenu pia mzielekeze katika kutambua muelekeo wa mabadiliko ya hali ya hewa na jinsi yanavyoweza kuathiri maisha ya vuimbe na wanaadamu” aliomba Maalim Seif.
Makamu huyo wa kwanza wa rais alisema anafahamu kuwa taasisi ya sayansi za bahari ni kituo cha utafiti kilichobobea kimataifa katika shughuli mbali mbali kama utafiti wa matumbawe, na matumizi ya satelaiti katika tafiti ambapo sambamba na hilo pia ni kituo cha taifa cha takwimu za mambo ya bahari (Tanzania National Oceanographic Data Center) ambapo ni mafanikio na jambo la kujivunia kwa taasisi hiyo pia.
Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika sherehe hizo, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Rwekaza Mukandara alisema Taasisi ya sayansi za Bahari imetoa mchango mkubwa katika kwa maendeleo ya taaluma ya utafiti na kuiomba serikali kushughulikia suala la kuliinua jengo ambalo hadi sasa limewekwa jiwe la msingi tu.
“Mheshimiwa mgeni rasmi Taasisi Sayansi za Bahari imetoa wahitumu wengi ambao hivi sasa wametawanyika kila seheu mbali mbali ndani na nje ya nchi na wengine hivi sasa wamekuwa ni walimu wa vyuo vikuu tofauti ….haya ndio mafanikio ya taasisi hii” alisema Profesa Mukandara.
Aidha Professa Mukandara alimuomba Maalim Seif na serikali yake kufikiria suala la jengo la taasisi yake ambayo hadi sasa imeweka jiwe la msingi katika eneo la Buyu lakini ujenzi wake ukisuasua jambo ambalo kimsingi Maalim alikubali kuwepo kwa mazungumzo ya pande mbili hizo uongozi wa chuo kikuu na serikali na kufuatilia suala hilo na kushauri watendaji wafuatulie suala hilo ambapo serikali itawasiliana na serikali ya Muungano kuona namna gani ya kusaidia ujenzi huo.

No comments:
Post a Comment