Saturday, 4 December 2010

Nauli za daladala kupanda Dar

na Chalila Kibuda


DSC_0026-small
WAMILIKI wa Daladala Mkoa wa Dar es Salaam (DARCOBOA) wamesema kuna uwezekano wa kupandisha nauli za daladala kutokana na kupanda kwa bei ya vipuri vya mabasi ya usafirishaji wa abiria. Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Mwenyekiti wa Darcoboa, Sabri Mabruk, alisema mgomo ambao walipanga kufanya wiki ikashindikana kutokana na serikali kukubali malalamiko yao katika mkutano wa wadau wa usafirishaji unaotarajia kufanyika Desemba na kwamba ongezeko la nauli itakuwa ni sehemu ya ajenda yao.
“Bei ya nauli itajulikana baada ya kikao ambacho kitajadili ajenda mbalimbali ikiwamo na kuongeza bei ya nauli ya sasa kuwa juu zaidi ili kuweza kurahisisha ufanisi,” alisema Mabruk.
Alisema wamiliki wa daladala wanakabiliwa na changamoto nyingi katika kuweza kusafirisha abiria hivyo wanahitaji kuongeza gharama hizo, ili wafanye kazi katika ufanisi zaidi.
Kuhusu ukamataji hovyo wa magari yao, Mabruk alisema waliiomba serikali kuingilia na kusema hawana ugomvi na serikali, hivyo wanahitaji makubaliano ambayo kwao yataweza kufanya sekta ya usafirishaji yenye ufanisi.

No comments:

Post a Comment