Assalaamu alaykum warahmatullahi wabarakaatuh
Tunapenda kutoa taarifa kwa ndugu zetu wote kwamba Alnoorcet imefanikiwa kwa uwezo wa Allah kupata jengo lenye permission ya kufanya Islamic Centre ikiwemo kusali salaa zote za jamaa. Allah awalipe kheri wanakamati wa Alnoorcet walioendea mbio usiku na mchana kulifanikisha jambo hili ambalo lilikuwa linavikwazo vigumu ndani yake. Lakini kwa rehmaa yake Allah ruhusa zote nzito zimetoka na lease contract ishasainiwa na jumba tumeshakabidhiwa siku ya Jumatano tarehe 1 Dec 2010.
Kazi za kufanya ukarabati zimeanza na tunategemea kukamilisha kabla ya Jumamosi ya tarehe 18 Dec 2010 Inshaaallah.
Hii ni Islamic centre yenu waislamu kwa hiyo kila anayetaka kujikurubisha na kujitukuza kwa Allah kwa kutasadaq chochote basi anakaribishwa. Unaweza kuweka standing order ya kiasi chochote kwa kila, au kila mwezi katika account ya alnoorcet. Kama unahitaji standing order forms zinapatikana hapo kwenye Alnoorcet Islamic Centre 11-13 Broadway, Barking, IG11 7LS au tutumie alnoor@alnoorcet.co.uk tutakutumia inshaallah kwenye email yako au unaweza kuidownload kwenye website ya alnoorcet kuanzia Thursday 16 Dec 2010.
Kama mnavyojuwa kutakuwa na baadhi ya vifaa vinahitajika katika centre hiyo kwa hiyo tutawatangazia kila kinachohitajika inshaallah. Kwani kwa hivi sasa wapo waliyokwishajitolea lakini tunaamini vipo vya ziada vitakavyohitajika inshaallah.
Centre iko wazi kuanzia 10:30am, kwa yoyote anayetaka kuitembelea anakaribishwa.
Jazaakumullahu khayran
Management
No comments:
Post a Comment