GADDAFFI AISHUTUMU NATO KWA MAUAJI YA WALIBYA
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi (pichani) ameshtumu mataifa yanayounda muungano wa Nato kwa mauaji,siku mbili baada ya watu wa familia ya mshirika wake wa karibu kuuawa kufuatia shambulio la angani.
Kupitia kituo cha taifa cha Televisheni,alitoa ujumbe kwa kanda siku ya Jumatano, akielezea wale waliotekeleza mashambulio kama "wahalifu" na "makatili".
Nato imeomba radhi kwa vifo vya raia, lakini wakasema kuwa nyumba iliolengwa ni "kituo kinachoratibu harakati za vikosi vya Gaddafi". Jamii ya kimataifa imegawanyika Mapema waziri wa mambo ya nje wa Italia alitoa wito wa kusitishwa kwa mapigano mara moja.
Francisco Frattini alisema muhimu mapigano yasitishwe ili kutoa fursa kwa misaada kuwafikia raia.
No comments:
Post a Comment