Wednesday, 9 March 2011

Zombe aidai Serikali fidia ya Sh5.2bilioni
 
James Magai na Tausi Ally
ALIYEKUWA mshtakiwa wa kwanza katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu wa madini kutoka Mahenge, Morogoro na dereva wa teski wa Manzese, Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Abdallah Zombe juzi ameishtaki serikali akiiomba mahakama iiamuru imlipe fidia ya Sh5.2bilioni.

Zombe alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Juni 9, 2006 na kuunganishwa na askari wenzake wengine ambao jumla yao walikuwa 13 wakituhumiwa kuhusika na mauaji ya Sabinus Chigumbi (Jongo), Ephrahim Chigumbi, Mathias Lunkombe na dereva teksi Juma Ndugu, katika msitu wa Pande wilayani Kinondoni nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam, Januari 14 mwaka 2006. Hata hivyo, Agosti 17, 2009 watuhumiwa wote waliachiwa huru na Mahakama Kuu Dar es Salaam, mbele ya Jaji Salum Massati baada ya kuonekana kutokuwa na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.

Kiasi hicho anachodai Zombe ni fidia ya madhara ya jumla na Sh200 milioni ikiwa ni fidia kwa adhabu ya kumweka ndani, riba pamoja na gharama za kesi hiyo.Wakati Zombe akifungua kesi hiyo ya madai, Serikali imekata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga hukumu iliyomwachia huru yeye na wenzake wanane ambayo bado haijatolewa uamuzi wala kusikilizwa.

Kwa mujibu wa hati ya madai iliyoandaliwa na Wakili Mwandamizi, Richard Rweyongeza, Zombe anadai alipwe fidia ya kiasi hicho au kingine ambacho Mahakama itaona kifaa kutokana na madhara aliyopata kutokana na kesi hiyo kwa kosa la kukamatwa na kumshtaki kwa tuhuma hizo akidai kuwa ni ukiukwaji wa sheria.

Katika kesi hiyo iliyosajiliwa kwa namba 35 ya mwaka 2011, mbali na kuomba mahakama hiyo iiamuru Serikali imlipe fidia, Zombe pia anaomba hiyo itamke kuwa alikamatwa na kushtakiwa kinyume cha sheria na ni batili.
Zombe anadai kuwa kabla ya kukamatwa alikuwa amehamishiwa katika Mkoa wa Rukwa na alirejeshwa Makao Makuu ya Polisi siku 14 baada ya kuwa ameripoti katika kituo chake hicho kipya cha kazi. Anadai kuwa siku hiyo kabla ya kukamatwa na kupandishwa kizimbani aliitwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) ambaye alimjulisha kuwa anatakiwa kuunganishwa na washtakiwa wengine waliokuwa wameshapandishwa kizimbani kwa tuhuma hizo.

Anadai kuwa baada ya taarifa hizo alichukuliwa ghafla na kupelekwa mahakamani ambako Hakimu Mkazi Mkuu alikuwa akimsubiri na kwamba mara baada ya kusomewa mashtaka yake alipelekwa katika Gereza la Ukonga mahali ambako kila kitu kilikuwa kimeandaliwa kwa ajili ya kumpokea.
Lakini analalamika kuwa baada ya kukamatwa, polisi walikuwa na wajibu wa kumwuliza kama alikuwa na jambo lolote la kusema ikiwa ni pamoja na kuweka kumbukumbu maelezo yake. Hati hiyo inadai kuwa kinyume chake, kukamatwa kwake kulifanyika kinyume cha wajibu huo, yaani bila kusikilizwa mlalamikaji kama alikuwa na cha kusema kuhusu ushiriki wake katika tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa hati hiyo, wakati akiwa mahabusu katika Gereza la Ukonga na baadaye Keko, Zombe aliwasilisha malalamiko yake kwa waziri mwenye dhamana ya masuala ya kisheria jinsi alivyotendewa lakini hakupata mwitiko wowote.
Analalamikia pia polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria na kutopewa haki ya kujieleza akiwa mtuhumiwa na matokeo yake kushtakiwa bila ushahidi wowote wa kumuunganisha katika tuhuma hizo.

“Kukamatwa na kushtakiwa kwa mlalamikaji kulifanywa kama matokeo ya Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wao wa kisheria waliopewa chini ya sheria za nchi,” inasema sehemu ya hati hiyo ya madai na kuongeza;
“Matokeo yake mlalamikaji ambaye alikuwa na uelewa wa matakwa ya sheria alijeruhiwa sana kiakili na kupata usumbufu.
Mlalamikaji alifedheshwa na aliathirika kwa maumivu ya kiakili kutokana na mchakato wa mashtaka.” Zombe katika hati hiyo anadai kuwa Polisi kwa makusudi waliacha kuchukua maelezo yake kuepuka uchunguzi linganifu ambayo yangewezesha kumwachia kabla ya kufikishwa mahakamani, kosa ambalo anadai fidia ya Sh200 milioni kwa madhara aliyopata.

“Kama matokeo ya Polisi kushindwa kutimiza wajibu wake na madhara yaliyompata mlalamikaji, sasa anadai fidia ya Sh5 bilioni kwa madhara ya jumla au kiasi chochote kadri mahakama itakavyoona,” inasisitiza hati hiyo ya madai. Sambamba na madai hayo ya fidia, pia Zombe katika hati hiyo ametoa utetezi wake kuhusu tukio la mauaji hayo aliyohusishwa akianza na alivyojiunga na jeshi hilo na kupanda vyeo na nyadhifa hatua kwa hatua, kabla ya kukumbwa na tuhuma hizo.

Anasema alijiunga na jeshi hilo mwaka 1977 akiwa na cheo cha Konstebo huku akijinasibu kuwa alifanya kazi kwa uadilifu na uaminifu mkubwa na kwa kujitoa na kupanda katika vyeo mbalimbali hadi alipofikia cheo cha ACP Juni 25, 2003. Anasema Julai, 2001 alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Dar es Salaam (RCO) na kwamba Julai 2 mwaka 2006 aliteuliwa kuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa.

Anasema kabla ya kwenda kuripoti aliyekuwa RPC wa Dar es Salaam alikuwa likizo hivyo yeye akawa anakaimu nafasi hiyo wakati huo pia akiwa bado anafanya kazi kama RCO. Anaeleza kuwa wakati akiendelea na wadhifa huo, Januari 14, 2006 watu wanne waliuawa na mauaji yao yalihusishwa na askari polisi na kwamba yeye alijulishwa kuhusu tukio hilo na Mkuu wa Polisi wa Wilaya (OCD) wa Kinondoni.

Anasema Januari 30, 2006 alikabidhi madaraka aliyokuwa akitumikia na aliyokuwa akikaimu kisha Februari 2, mwaka huo akaondoka kwenda katika kituo chake kipya kutumikia wadhifa wa RPC mkoani Rukwa. Anasema kabla ya kwenda Rukwa, Rais alikuwa ameunda Tume ya kuchunguza tukio la mauaji hayo na kwamba ingawa na yeye alihojiwa na tume hiyo lakini anadai kuwa haikupendekeza akamatwe na kushtakiwa.

No comments:

Post a Comment