Mwandishi Maalum WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha ameiagiza mara moja, Idara ya Uhamiaji kufanya operesheni maalumu ya kuwakamata na kuwarejesha watu wote katika nchini zao ambao wanaishi nchini kinyume cha sheria.Waziri Nahodha aliyasema hayo jana wakati akizungumza na viongozi na watumishi wa Idara ya Uhamiaji jijini Dar es Salaam katika ziara ya siku moja kufuatilia utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa mapema mwaka huu. Baada ya kuteuliwa kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Waziri Nahodha alitembelea idara hiyo. Waziri Nahodha alisema idara hiyo inapaswa kufanya operesheni kwa kuwa wahamiaji haramu nchini wamekuwa wakiongezeka kwa kasi. Pia alishauri Watanzania wanaoishi nchi jirani kinyume cha sheria, wakamatwe na kurejeshwa nchini ili kujenga utamaduni wa kuheshimu sheria za nchi nyingine. “Hata ukitembea tu barabarani utajua tu mtu huyu si mtanzania wako watu wengi ukipishana nae njiani, bila hata kupata taarifa zake za kina utagundua ni mgeni, ndugu zangu yafaa jambo hili litizamwe upya na kwa kina zaidi ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea baadaye,” alisema Vuai. Katika hatua nyingine Waziri Nahodha aliitaka Idara ya Uhamiaji kutafuta na kuanzisha mfumo mpya wa kisayansi wa kukusanya mapato yanayotokana na huduma za uhamiaji, ikiwamo, pasi za kusafiria, ukaazi na hati nyingine ili kukusanya mapato stahiki. Waziri Nahodha alisema hivi sasa haridhishwi na mfumo unaotumika katika kukusanya mapato kwani mfumo huo, unakwamisha Idara ya Uhamiaji kukusanya mapato stahiki. Alisema mfumo wa sasa unawapa ushawishi mkubwa watumishi wa Idara hiyo kutokuwa waaminifu kutokana na hali ya udhaifu wa kibinadamu. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Monday, 7 March 2011
'Wanaoishi kunyume cha sheria wakamatwe'
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment