MATAIFA YA MAGHARIBI KARIBIA KUFIKIA MAKUBALIANO…!!!
Mataifa ya Magharibi yanayoshiriki katika kikosi cha Umoja wa Mataifa kutekeleza marufuku ya ndege kuruka katika anga ya Libya, yanakaribia kufikia makubaliano kuhusu jinsi ya kuihusisha Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika juhudi za kijeshi.
Hata hivyo bado haijajulikana wazi jinsi muungano huo utakavyohusishwa na nani atakayeongoza operesheni hizo za kijeshi.
Baadhi ya nchi ikiwemo Ufaransa na Uturuki zina wasiwasi kuwa kikosi kinachoongozwa na NATO huenda kikaonekana kuwa na sifa mbaya katika ulimwengu wa nchi za Kiarabu.
WAKATI HUO HUO
Ujerumani imetangaza kujiondoa katika operesheni za Jumuiya ya Kujihami ya NATO katika eneo la Mediterranean kutokana na jeshi la muungano kushiriki katika mgogoro wa Libya.
Msemaji wa wizara ya ulinzi amesema manowari mbili na meli nyingine mbili zitarejea katika kikosi cha Ujerumani.
Manowari hizo za Lübeck na Hamburg ni sehemu ya operesheni za juhudi za NATO katika kupambana na ugaidi kwenye eneo hilo.
Takriban wanajeshi 70 wa Ujerumani wanaoshiriki katika operesheni za NATO pia wataondolewa.
No comments:
Post a Comment