Wakulima Zanzibar Kujengeza Uwezo
Na Salma Said
MIKAKATI maalum imewekwa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar katika kuwajengea uwezo wakulima hapa nchini hivyo uwamuzi wa Serikali ya Iran kuiunga mkono Zanzibar katika sekta ya kilimo utasaidia kwa kiasi kikubwa.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi. Dk. Ali Mohamed Shein aliyasema hayo leo wakati alipokuwa na mazungumzo na Balozi wa Iran nchini Tanzania. Mohsin Movahhedi Ghomi, Ikulu mjini Zanzibar.
Katika mazungumzo hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa miongoni mwa mikakati iliyowekwa na serikali katika kuhakikisha sekta ya kilimo inaimarika ni pamoja na kuwajengea uwezo wakulima kwa kuongeza vifaa vya kilimo yakiwemo matrekta.
Alisema kuwa kutokana na juhudi za kuimarisha kilimo cha kisasa serikali imeona ipo haja ya kuongeza vifaa na vitendea kazi vyengine vya kilimo hivyo uwamuzi wa Iran kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha sekta hiyo utasaidia kufikia lengo lililokusudiwa
Rais Dk. Shein alisema kuwa kutokana na sekta ya kilimo kuwa na mchango mkubwa katika uchumi na maendeleo ya wananchi wa Zanzibar serikali imeona haja ya kuiimarisha sekta hiyo hasa kukiimarisha kilimo cha umwagiliaji maji.
Aidha, Dk. Shein alimueleza Balozi huyo kuwa kuna kila sababu za kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya nchi mbili hizo ambazo zina historia ya siku nyingi ya uhusiano wake. Alisema kuwa uhusiano na ushirikiano wa nchi mbili hizo pamoja na wananchi wake unazidi kukua siku hadi siku, hivyo ipo haja ya kuimarisha kwa pamoja.
Akizungumzia juu ya sekta ya kilimo, Dk. Shein alimueleza Balozi Ghomi kuwa kuna haja kuwepo kwa mashirikiano ya Vyuo Vikuu vya Iran na Zanzibar hatua ambayo itajenga uwezo na ufanisi mkubwa katika sekta ya elimu.
Alisema kuwa kuwepo kwa mahusiano ya Vyuo Vikuu vya nchi hiyo na Zanzibar kutaweza kuimarisha sekta ya elimu na kuleta manufaa kwa pande zote mbili kwani Vyuo vikuu hivyo vitaweza kubadilishana uzoefu, taaluma, wanafunzi na hata Wakufunzi.
Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Balozi Ghomi kuwa azma ya Iran kushirikiana katika kuimarisha sekta ya utalii hapa Zanzibar kutasaidia kwa kiasi kikubwa kwani sekta hiyo itapelekea kuimarika kwa sekta nyenginezo ikiwemo kilimo na uvuvi.
Dk. Shein aliwakaribisha wawekezaji wa Iran kuja kuekeza hapa Zanzibar katika sekta ya utalii na sekta nyenginezo kwani mazingira mazuri tayari yameshawekwa na serikali.
Dk. Shein alieleza matumaini yake makubwa ya kuimarika kwa sekta ya kilimo kutokana na utalii na kueleza kuwa licha ya udogo wa ardhi ya Zanzibar pato kubwa la kilimo linaweza kupatikana kutokana na kukua kwa sayani na teknolojia.
Sambamba na hayo, Dk. Shein aliipongeza Serikali ya Iran pamoja na kumpongeza Balozi huyo kwa salamu za pongezi juu ya kuchaguliwa kwake kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na kusisitiza kuwa kufanana kwa tamaduni za nchi mbili hizo ni kiashirio kikubwa cha mahusiano ya muda mrefu.
Nae Balozi wa Iran nchini Tanzania Mhe. Mohsin Movahhedi Ghomi alimueleza Rais Dk. Shein kuwa Iran imeazimia kuiunga mkono Zanzibar katika sekta za maendeleo ikiwemo sekta ya kilimo.
Alisema kuwa kutokana na sekta hiyo kupata mafanikio makubwa nchini Iran ni sababu tosha kwa nchi hiyo kuweza kuisaidia Zanzibar.
Balozi Ghomi alisema kuwa juhudi za makusudi zitachukuliwa na nchi yake katika kuhakikisha inaisaidia Zanzibar katika kuimarisha sekta ya kilimo juhudi ambazo tayari zimeshaanza kuoneshwa na serikali anayoiongoza Dk. Shein.
Alisema kuwa mbali ya sekta ya kilimo, Iran itaendelea kuwa balozi wa kuitangaza Zanzibar Kiutalii nchini humo kutokana na vivutio mbali mbali vilivyopo hapa nchini.
Aidha, Balozi Ghomi alieleza kuwa nchi yake itaendelea kutoa mashirikaino kwa Zanzibar katika kuimarisha sekta ya elimu na kukubali wazo la kuwepo kwa mahusiano kati ya Vyuo Vikuu ya Iran na Zanzibar.
Sambamba na hayo, Balozi huyo alieleza kufurahishwa kwake na uhusiano na mashirikiano ya kihistoria yaliopo kati ya nchi hiyo na Zanzibar na kuadi kuwa nchi yake itaimarishwa zaidi uhusiano huo kwa manufaa ya pande zote mbili.
Pia, Balozi huyo alieleza nia ya nchi yake kukuza ushirikiano kwa wafanyabiashara wa Iran na Zanzibar ili sekta hiyo iweze kuleta manufa kwao na nchi zote mbili

No comments:
Post a Comment