WAKULIMA wa zao la Mpunga katika bonde la Tumbe Magharibi Kisiwani Pemba, wameshauriwa kulima zao hilo kwa wingi huku wakizingatia ushauri wa wataalamu ili kuweza kuepuka balaa la njaa linaloendelea kutokea katika baadhi ya mataifa duniani.
Ushauri huo umetolewa na Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, kabla ya kusitisha ziara yake kisiwani Pemba wakati akizungumza na wakulima wa bonde hilo baada ya kukagua tuta lililojengwa kwa msaada wa Mfuko wa TASAF na waananchi.
Tuta hilo limejengwa kwa madhumuni ya kuzuiya maji ya chumvi kutoka baharini ambayo yamekuwa yakiingia mashambani na kusababisha wakulima kusitisha shughuli zao za kilimo hicho.
Alisema ili wakulima wa bonde hilo waweze kufanya vizuri katika kilimo cha mpunga watapaswa kuzingatia ushauri wa wataalamu jambo ambalo litawawezesha kujitosheleza na chakula na kuondokana na matatizo ya ukame uliopo katika baadhi ya nchi duniani.
Alieleza kuwa baadhi ya nchi hivi sasa ambazo zimekuwa zikizalisha kwa wingi mpunga Ikiwemo China, Japan na Vietnam tayari zimeanza kutetereka uzalishaji wao kunakosababishwa na mafuriko yasioisha, jambo ambalo huwafanya kulinda masoko yao ya ndani zaidi kuona bidhaa ya mchele haiwapungukii.
Hali hiyo alisema inachukuliwa na mataifa hayo kwa lengo la kunusuru wananchi wao kutopata balaa la njaa jambo ambalo linaweza kwa kiasi kikubwa kuziumiza nchi ambazo zinategemea sana kupata bidhaa hizo kwa kuagiza.
Alisema kuwapo kwa mitazamo hiyo ni wazi kuwa wakulima wa Zanzibar watapaswa kuona wanabadili njia za kilimo cha asili na kuyatumia mabonde waliyonayo kuzalisha mpunga mwingi kwa kufuata njia za kitaalamu ili wajitosheleze kwa chakula.
Hilo alisema watalazimika kulizingatia kutokana na wengi wananchi wa Zanzibar kupenda chakula cha wali ambao asilimia kubwa ya mchele wanautumia hutegemea kupatikana katika masoko hayo ya nje.
Alisema kwa vile tayari wakulima wa bonde hilo, wameamua kuaanzisha mradi huo, ni vyema hivi sasa wakaanza kulima kisasa ili waweze kupata uzalishaji mkubwa na utaowawezesha kukabiliana na njaa.
Alisema tahadhari hiyo ni lazima waifanyie kazi kisawa sawa kutokana na miongo ya mvua kuanza kubadilika kiasi ambacho hivi sasa kuwapo na kutonyesha mvua kwa wingi katika misimu husika.
Akiendelea alisema hali hiyo inakuja zaidi ni kutokana na maji ya chumvi kupanda juu na kiasi cha kuingilia mashamba ya wakulima kama ilivyojitokeza katika kijiji hicho vikiwemo vya Unguja kwa kijiji cha Jozani na Nungwi.
Kutokana na kuwapo kwa hilo Makamu huyo aliwataka wananchi hao kuona Bonde hilo baada ya kuzuiliwa kuingia maji ya chumvi imundo mbinu hiyo inalindwa ili maji yasiweze kupita na kuingia katika mshamba yao.
Alisema Serikali itahakikisha itaendeleza kutoa misaada mbali mbali kwa wakulima ili kuona wanakuwa katika hali nzuri ya kulima katika mfumo wa kisasa.
Baadhi ya wananchi ambao walizungumza na kiongozi huyo walieleza wameridhishwa na hatua iliyochukuliwa na mfuko wa TASAF kufanikisha mpango huo kwani walilazimika kusitisha kilimo hicho kutokana na mashamba yao kuingiliwa na maji ya chumvi.
Hali hiyo walieleza kuwa imewafanya kutegemea zaidi kupata vyakula kutoka madukani ingwa wao wenyewe wakiwa na hamu ya kushiriki katika kilimo kwenye bonde hilo.
Nae Sheha wa Shehia hiyo Masoud Khamis, alisema zaidi ya ekari 25 wananchi wa eneo hilo wamekuwa wakizitumia katika kufanya kazi zao.
Mtaalamu msimamizi wa Mfuko wa TASAF, alisema kuwa mradi huo hadi kumalizika kwake umeweza kutumia milioni 35 na ulinaza mwezi Mei mwaka jana.
Kayika ziara hiyo Balozi Iddio alifuatana na Mkewe Mama Pili Juma Iddi na baadhi ya Wazee wa serikali.

No comments:
Post a Comment