Friday, 25 February 2011

Ukosefu wa Maji Wathiri Wagonjwa Mnazi moja


zanzibar166: Stone Town, Zanzibar, Tanzania: Mnazi Mmoja Hospital, named after Lenin in more ideological times - Hospitaliya Mnazimmoja Zanzibar - Kaunda road - Vuga area - photo by M.Torres - (c) Travel-Images.com - Stock Photography agency - Image Bank
Na Salma Said Zanzibar
HUDUMA za maji zimetoweka kwa siku ya pili katika hospitali ya rufaa ya Mnazimmoja mjini Zanzibar na kuathiri wagonjwa wasiopunguwa 400 mjini Zanzibar.
Fundi Mkuu wa Hospitali hiyo, Juma Ali Hamad amethibitisha kutokea kwa tatizo hilo na kuathiri wodi za wagonjwa 12 waliolazwa katika hospitali hiyo.
Amesema tatizo hilo limeanza kujitokeza jana majira ya saa 10:00 za jioni na kulazimika uongozi wa hospitali hiyo kuitisha kikao cha dharura kujadili uhaba huo wa maji.
Hata hivyo amesema kwamba tayari wamekwisha itaarifu Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA), wakati wakiendelea na juhudi za kutengeneza kisima cha hakiba katika bustani ya Victoria na hadi jana mchana walikuwa wakiendelea na kazi ya kuchimba mitaro ya mabomba.
Msaidizi Katibu wa Hospitali hiyo ya Mnazimmoja, . Omar Abdallah Ali, amesema kwamba huduma za upasuaji na wodi ya wazazi zimeathirika kwa vile zinahitaji maji masa 24, pamoja na shughuli za usafi katika hospitali hiyo.
Nae msemaji wa Mamlaka ya Maji Zanzibar, Zahor Salum amesema kwamba tatizo hilo limetokana na mabadiliko ya hali ya hewa baada ya uzalishaji w amaji kupunguwa katika vyanzo vya maji vya Mwanyanya na Mtopepo ambavyo vinatowa huduma kwa wilaya ya mjini.
Amesema tatizo la ukame lililoanza kujitokeza limeathiri uzalishaji katika vyanzo hivyo vya maji na kuathiri maeneo yaliyopkuwa yakipokea maji kutoka katika matanki ya Saateni ikiwemo Mji Mkongwe , Maisara, Kikwajuni na maeneo ya mchangani.
Wakati huo huo wananchi wa Kijiji cha Mpapa wilaya ya Kati Unguja wameiomba Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) kukifanyia matengenezo kisima cha maji kilichopo kijijini hapo, ili kuweza kupata huduma ya maji inayowasumbuwa kwa muda mrefu sasa.
Wito huo kwa Mamlaka hiyo umetolewa na wananchi wa kijiji hicho walipokuwa wakizungumza na mwandishi wa habari hizi huko Mpapa Mkoa wa Kusini Unguja.
Walisema kuwa kisima hicho kimekuwa hakitoi maji kwa muda mrefu sasa hali ambayo inawasababisha kufuata huduma hiyo katika masafa marefu.
“Kisima hiki kwa muda mrefu sasa kimekuwa hakina uwezo wa kutoa maji, hivyo ni tunakuwa tunafata huduma hii katika masafa marefu jambo ambalo ni usumbufu”, alisema Bi Khadija Kassim Ali mkazi wa Bambi.
Kutokana na hali hiyo wanakijiji hjayo wameiomba Mamlaka hiyo kukifanyia matengenezo kisima hicho ambacho kimechimbwa miaka mitano iliyopita, ili kuweza kutoa huduma ya maji katika kijiji hicho na maeneo ya jirani ya kijiji hicho.
Khadija alisema kuwa licha ya jitihada mbali mbali walizozifanya ya kutoa mabomba yaliyokuwa yameziba na kulisafisha tangi lao la kuhifadhia maji lakini hadi sasa bado jitihada zao hizo hazijaweza kufanikiwa.
Ttaizo kubwa ambalo limekikumba kisima hicho kishindwe kutoa maji ni pamoja na kuziba kwa baadhi ya mabomba ambayo yamepelekea maji kushindwa kutoka na kisima hicho kukauka.

No comments:

Post a Comment