Na Paulina David, Mwanza
JESHI la Polisi mkoani hapa limesema litatoa ulinzi wa kufanikisha maandamano ya amani yatakayofanywa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) yanayotarajiwa kufanyika leo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Simon Sirro, alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanzia Buzuruga hadi viwanja vya Furahisha.
Alisema Jeshi la Polisi linatoa ulinzi baada ya chama hicho kukubaliwa ombi lao la kufanya maandamano ya kupinga malipo ya Dowans, kutaka kuishinikiza serikali kutaifisha mitambo ya Downs na kuishinikiza serikali kupunguza gharama kubwa za umeme.“Polisi tumejipanga kutoa ulinzi wa uhakika kuhakikisha maandamano yanayofanyika yanakuwa ni ya amani na yanamalizika kwa utulivu,” alisema Kamanda Sirro.
Aidha, aliwaomba wananchi watakaoshiriki maandamano hayo kuacha kufanya maandamano baada ya mkutano, kwani hatua hiyo itasaidia kuondoa vurugu zisizo za lazima.

No comments:
Post a Comment