Na Mwandishi wetu, Kampala, Uganda
MTANZANIA, Hija Suleman Nyamondondo (31), amekamatwa kwa tuhuma za kuhusika na matukio ya mashambulizi ya mabomu yaliyotokea nchini hapa mwaka jana.
Mashambulizi hayo yaliyotokea mjini Kampala nchini hapa yalisababisha kuuawa kwa watu zaidi ya 70.
Taarifa zinasema Mtanzania huyo alikamatwa baada ya kufanyika kwa msako wa polisi nchini hapa, kwa kushirikiana na polisi wa nchi jirani na wa kimataifa wa Interpool.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, alikamatwa na kuletwa nchini hapa kwa usafiri wa ndege na kushushwa Jumanne katika Uwanja wa Ndege wa Entebbe na kupokewa na maofisa wa polisi akiwa chini ya ulinzi mkali.
Ilielezwa kwamba alikuwa amefungwa pingu pamoja na minyororo miguuni.
Taarifa zinasema Mtanzania huyo mchango wake mkubwa katika tukio hilo ilikuwa ni kusafirisha mabomu hayo na kuyaingiza nchini hapa.
Hata hivyo taarifa hazikusema aliyatoa wapi mabomu hayo lakini imesisitizwa Mtanzania huyo alibeba jukumu la kuyafikisha nchini hapa.
Katika mabomu aliyoleta moja ililipuka katika uwanja wa mchezo wa raga wa Kyandondo, eneo la Lugogo, ambapo watu wengi waliuawa na jingine katika mgahawa mmoja wa Ethiopian Village katika Mtaa wa Kabalaga.
Mwaka jana Mkuu wa Polisi nchini hapa alikuwa ameilalamikia nchi ya Tanzania kwa kukataa kushirikiana naye kumleta mtuhumiwa huyo nchini hapa.
Kukamtwa kwa mtuhumiwa huyo kunafanya idadi ya waliotiwa mbaroni kufikia 30.
Katika tukio hilo kundi la wapiganaji la Kisomali la al-Shabab lilidai kuhusika na mashambulio hayo kutokana na serikali ya nchini hapa kuiunga mkono Serikali ya Somalia mjini Mogadishu.

No comments:
Post a Comment