Thursday, 24 February 2011

Mabomu yatua Kinondoni
*DC Kinondoni ashtuka
Na Grace Ndossa, Kinondoni

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Jordan Rugimbana, amebaini kuwapo kwa mabomu saba katika maeneo ya Kimara na Mbezi na kuwatadharisha wananchi kutoshika kitu ambacho hawakielewi.Akizungumza jana baada ya
kutembelea maeneo hayo, amewataka wananchi wa maeneo hayo kutochoma moto na kushika vipande vya chuma ambavyo hawavitambui.

“Mabomu yaliyolipuka mwishoni mwa wiki katika kambi ya Jeshi la Wananchi (JWTZ) ya Gongo la Mboto yamesambaa katika maeneo tofauti, hivyo nawaomba wananchi kutoshika kitu ambacho hakieleweki,” amesema Rugimbana.

Hata hivyo, amesema kutokana na hali hiyo pia wanatakiwa kuepuka kuchoma moto maeneo yao ovyo ili kuepuka athari inayoweza kutokea.

Amesema wananchi wanatakiwa kuwa makini kutokana na mabomu mengine kuingia hadi ardhini, jambo ambalo ni vigumu kulibaini.

No comments:

Post a Comment