*Yadai TV, simu, redio kutotumika *Matumizi kumalizika 2012 Na Stella Aron, jijini MAMLAKA ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imetoa tahadhari kubwa kwa wananchi kuacha kununua vifaa vya elektroniki vinavyotumia mfumo wa teknolojia ya zamani (‘analogy’) kwani mwisho wa matumizi yake ni Juni 2012. Akizungumza kwenye kipindi maalumu katika kituo cha redio cha Wapo jijini, Kaimu Meneja wa TCRA Kanda ya Juu Kusini, Injinia Deogratius Moyo, amesema vifaa vyote vinavyotumia mfumo huo havitatumika tena ufikapo wakati huo.Amesema hivi sasa kumekuwa na ongezeko kubwa la uingizaji wa vifaa vinavyotumia mfumo wa ‘analogy’ ambavyo huuzwa kwa bei nafuu. Meneja huyo amesema wananchi wanaotumia vifaa kama simu za mkononi, redio na televisheni ambavyo hutumia mfumo huo wa ‘analogy’ watatakiwa kuingia gharama ili kuondokana na mfumo huo. “Zamani tulikuwa tukitumia redio kama za santuri, lakini hivi sasa hazitumiki tena kutokana na matumizi yake kupitwa na wakati, hivyo wananchi watakaotaka kuendelea kutumia vifaa vya zamani watatakiwa kuingia gharama kwa kuunganishwa kwenye mfumo wa teknolojia ya kisasa (‘digital’),” amesema meneja huyo. Mbali na vifaa hivyo vya majumbani, pia amesema kuwa vituo vya redio na televisheni vinavyotumia mfumo wa ‘alalogi’ pia matumizi yake yanatarajiwa kumalizika 2020. “Si vifaa vya majumbani tu bali hata vituo vya redio na televisheni vinavyotumia mfumo wa ‘analogy’ pia havitaweza kufanya kazi ifikapo mwaka 2020,” amesema. Amesema kabla ya wananchi kununua vifaa hivyo kwanza watatakiwa kuuliza kwa wafanyabiashara ni aina gani ya mfumo unaotumia kifaa anachohitaji kununua. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Saturday, 18 December 2010
TCRA yatoa tahadhari
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment