Saturday, 18 December 2010

CUF kuweka mambo hadharani leo



                                                               





                                                      
Na Waandishi Wetu, jijini

CHAMA Cha Wananchi (CUF) leo kinatarajia kuweka mambo hadharani katika viwanja vya Temeke mwisho ambapo pia Makamu wa kwanza wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Maalism Seif Sharif Hamad, anatarajiwa kuhudhuria.Akizungumza na gazeti hili leo asubuhi, mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahimu Lipumba, amesema mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho.

“Lengo la mkutano ni kumpongeza Maalim Seif kwa kuteuliwa kwake na pia tutazungumzia maana ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa, hivyo tunawaomba wananchi na wanachama kufika kwa wingi katika viwanja hivyo,” amesema

Pia amesema katika mkutano huo watazungumzia suala la umuhimu wa kupata katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano na kutoridhishwa na usimamizi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kwenye Uchaguzi Mkuu uliopita.

“Hatukuridhishwa na tume hiyo kwenye uchaguzi, kwa hiyo hilo ni kati miongoni mwa mambo tunayotarajia kuyazungumza kwenye mkutano huo. Tunataka tume huru isiyopendelea upande wowote,” amesema mwenyekiti huyo.

Pia amesema Maalim Seif atazungumzia changamoto mbalimbali zilizojitokeza Zanzibar katika kipindi cha uchaguzi.

Ameelezea kuwa Maalim Seif ataelezea kwa kina juu ya uchaguzi mkuu uliopita na tathimini ya kina kwa kujiimarisha zaidi ili kukabaliana na siasa za wakati uliopo na matokeo ya undwaji wa serikali ya umoja wa kitaifa.

Amewaomba wananchi kujitokeza kwa wingi kuhudhuria mkutano huo ili kufahamu masuala mbalimbali na mikakati iliyowekwa na chama hicho kuhakikisha kuwa kunakuwa na mabadiliko.

No comments:

Post a Comment