OFISI ya Makamu wa Rais-Mazingira, imesema matumizi ya mafuta ya Transfoma na vifaa vyake vilivyogundulika kuwa na kemikali kali (Pcb), vimewaathiri wananchi na samaki katika maziwa na bahari, hivyo ni lazima matumizi hayo yakomeshwe. Aidha imeitakaTANESCO kupitia vituo vyake Tanzania Bara na Visiwani, kuhakikisha halitumii mafuta hayo na majenereta yake yaliyopigwa marufuku kuingizwa nchini na kufanya hivyo kutapunguza athari za uharibifu wa mazingira unayosababishwa na kemikali ya Pcb. Mkurugenzi Msaidizi kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Magdalena Mtenga, aliyasema hayo juzi jijini hapa, muda mfupi baada ya kutembelea shughuli za usambazaji umeme kupitia transfoma zisizokuwa na kemikali zenye athari kwa binadamu jijini Mwanza. Mtenga pia alitembelea maeneo tofauti ya TANESCO katika wilaya za Ilemela na Nyamagana kwa lengo la kujifunza. “Upo uchafuzi mkubwa wa mazingira ambao husababishwa na mafuta haya ya transfoma na majenereta yake yaliyogundulika kuwa na athari kwa binadamu na samaki kutokana na kemikali yake kali. “...Serikali inataka mafuta ya aina hii ya Pcb yasitumike tena hapa nchini na wananchi waache kuiba mafuta kwa sababu wanaweza kuathirika na mafuta ya aina hii yanapomwagika huharibu mazingira,” alisema Mtenga. Kutokana na hali hiyo, alieleza kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi duniani zilizoridhia kuteketezwa kwa mafuta hayo mabaya ya transfoma yenye kemikali kali mara ifikapo mwaka 2025 ili kuondoa hali ya uchafuzi wa mazingira. Akizungumzia juu ya kuteketezwa kwa mafuta hayo mara ifikapo mwaka 2025 Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Enock Masanja, alisema Tanzania haina mitambo maalumu ya kuteketeza mafuta hayo, hivyo yatapelekwa nje ya nchi kwa ajili ya kuteketezwa. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Wednesday, 22 December 2010
Mafuta ya transfoma hatari kwa viumbe hai
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment