Salim Said CHAMA cha Wananchi (CUF), kimesema kitawasilisha kwa Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani, nakala ya rasimu sifuri ya mapendekezo ya Katiba mpya ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Desemba 28 mwaka huu kwa maandamano ya amani yatakayoanzia Buguruni.Hayo yalisemwa jana na Mwenyekiti wa chama hicho,Profesa Ibrahim Lipumba alipokuwa akitoa salamu zake za Krismas na Mwaka Mpya kwa Watanzania. Profesa Lipumba alisema maandamano yataanzia katika Kituo cha Mafuta cha Buguruni na kwamba yatapitia katika Barabara ya Uhuru na kuishia katika Wizara ya Sheria na Katiba. Kwa mujibu wa kiongozi huyo wa CUF,baadaye waandamanaji warudi katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambako kutakuwa na mkutano wa hadhara utakaohutubiwa na wadau kutoka taasisi na vyama mbalimbali vya siasa. "Baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2005, CUF iliongoza mjadala wa kupata katiba mpya hadi kufikia kuandikwa kwa rasimu sifuri ya katiba hiyo,"alisema. Alisema maandamano ya kuwasilisha rasimu hiyo, yatawashirikisha wadau kutoka vyama vya siasa,wanaharakati na taasisi zisizo za kiserikali. Profesa Lipumba alisema maandamano hayo yataongozwa na Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria wa CUF, Julius Mtatiro na viongozi mbalimbali wa kitaifa katika chama hicho. Alisema maandalizi yote muhimu kwa ajili ya maandamano hayo, yameshakamilika ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa kwa Jeshi la Polisi na kwa Waziri wa Sheria na Katiba. "Tukifika kwa waziri tutamkabidhi rasimu na baadaye maandamano yatageuka na kurudi katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambako wawakilishi kutoka vyama na taasisi mbalimbali watawahutubia Watanzania na kuelezea umuhimu wa kuwa na katiba mpya," alisema Profesa Lipumba. Alisema hatua hiyo itakuwa ya kwanza kubwa na shirikishi katika madai ya katiba mpya. Profesa Lipumba alisema ni vizuri serikali ikaheshimu kilio na madai ya Watanzania kuhusu katiba mpya kwa kuweka mchakato shirikishi wa kupata katiba yenye misingi ya kidemokrasia. Alimshauri Rais Jakaya Kikwete, kuunda tume huru itakayongoza mjadala wa kitaifa wa mchakato wa kupata katiba hiyo. "Ni vizuri tume hiyo ikaongozwa na watanzania wanaoheshimika na waliobeba katika fani ya sheria na katiba kama vile Profesa Issa Shivji, Jaji Mkuu mstaafu Barnabas Samatta na Jaji Robert Kisanga. Lakini iwahakikishie Watanzania kwamba haitachakachua ripoti ya tume hiyo kama ilivyofanya katika Tume za Jaji Francis Nyalali na ya Kisanga," alisisitiza Profesa Lipumba. Alisema wazo la Waziri Mkuu, Mizengo Pinda la kumshauri Rais Kikwete kuandaa mchakato wa kupata katiba mpya, lakini kwa muda alioweka wa miaka mitatu halitakuwa na tija kwa sababu haitatumika katika uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2014 au wa rais, wabunge na madiwani wa mwaka 2015. "Kama tunahitaji kuwa salama na kuepuka shari na vurugu za kisiasa, lazima chaguzi zijazo zifanyike chini ya katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, la sivyo tutakuwa katika hatari kwa sababu watanzania hawako tayari kuchakachuliwa kila mwaka," alisema. Alipoulizwa kuhusu maandamano hayo, Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alikiri kupata taarifa na kwamba atatoa taarifa Jumatatu ijayo. Kwa upande wake, waziri Kombani alisema yeye hajui lolote kuhusu wa CUF. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Saturday, 25 December 2010
CUF kukabidhi rasimu ya katiba kwa maandamano
Subscribe to:
Post Comments (Atom)

No comments:
Post a Comment