Sunday, 21 July 2013

 MAPOKEZI YA MIILI YA WANAJESHI WA JWTZ WALIOKUFA KWA SHAMBULIZI HUKO DAFUR

 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwaongoza wananchi na viongozi wengine kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la kulinda amani, waliopoteza maisha katika Jimbo la Darfur, wakati miili hiyo ilipokuwa ikiwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jana jioni
 
 
 
 
 
 
Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum kabla ya kuondolewa katika uwanja wa jeshi
 
 
Baadhi ya askari wa JWTZ wakibeba miili ya wanajeshi wenzao waliouwawa Darfur kuiingiza kwenye magari maalum


 
Baadhi ya askari wa JWTZ wakifunika majeneza ya askari hao kwa bendera ya taifa mara baada ya kushushwa kwenye ndege maalum


 
 
 
Baadhi ya wanajeshi na wahudumu wa ndege wakishusha miili ya wanajeshi wa JWTZ waliouwawa Darfur hivi karibuni


 
Baadhi ya maofisa wa JWTZ na maofisa wa UN waliosindikiza miili ya wanajeshi wa JWTZ waliouwawa Darfur wakishuka kwenye ndege


 
Askari wakishusha majeneza yenye miili ya askari wenzao waliofariki dunia huko Darfur
 
 
 
Mama mmoja ambaye hakuweza kufahamika jina lake, ambaye ni mmoja kati ya wafiwa akishikiliwa na wenzake wakati akilia kwa uchungu baada ya kuona majeneza yakishushwa kwenye ndege
 
Askari wa Jeshi wakijipanga kupokea miili hiyo kwa heshima
 
 
 
 
 
Msafara wa magari ya Jeshi yaliyobeba miili hiyo ukianza safari ya kuelekea Lugalo. 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, jana jioni amewaongoza watanzania kupokea Miili ya Askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) waliopoteza maisha Jimboni Darfur nchini Sudan kutokana na shambulizi la ghafla. 

Miili hiyo imewasili kwa ndege maalum katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere – Terminal one (Air Wing) leo jioni majira ya saa kumi. 
 
Mara baada ya kuwasili miili hiyo iliongozwa na msafara kuelekea hospitali ya rufaa ya Jeshi, Lugalo, kwa ajili ya kuhifadhiwa hadi siku ya Jumatatu Julai 22, 2013 itakapoagwa rasmi kwa heshima zote katika Uwanja wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Upanga Jijini Dar es Salaam, ambapo ni Makao Makuu ya Jeshi Mkabala na Ukumbi wa Diamond Jubilee kuanzia majira ya saa tatu asubuhi. 
Waandishi wa habari mnaombwa kuhudhuria na kufanya ‘Coverage’ katika mapokezi na hatimaye siku ya kuaga miili hiyo ya mashujaa wetu waliopoteza maisha wakitetea amani duniani.

No comments:

Post a Comment