Monday, 16 April 2012

Dk Shein Aendelea na Ziara Kisiwani Pemba


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la MapinduziDk.Ali Mohamed Shein, akizungumza na watendaji wa Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa huo,katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba jana,(kulia) Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Hamadi Mberwa Hamadi, na (kushoto) Mkuu wa Mkoa huo Dadi Faki Dadi.



Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akisalimiana na wananchi waliojitokeza kumpokea katika uwanja wa karume Pemba alipowasili kisiwani humo kwa ziara maalum kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za kijamii.




Baadhi ya watendaji wa Ofisi mbali mbali za Taasisi za serikali za Mkoa wa Kaskazini Pemba,wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,alipokuwa akizungumza na watendaji hao,wakati alipofanya ziara ya kuangalia maendeleo katika sekta mbali mbali za Mkoa wa kaskazini Pemba,katika ukumbi wa Jamhuri Hall Wete Pemba.

No comments:

Post a Comment