Saturday, 14 April 2012

             CAG ashauri Serikali ivunje ATCL


 
Air Tanzania flight
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 
 

    
Daniel Mjema, Dodoma
MDHIBITI na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amesema, Serikali inavyoendesha Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) kwa sasa ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.

Utouh amependekeza ATCL ivunjwe na liundwe shirika jipya lenye mtaji, menejimenti nzuri na mikakakati madhubuti ili kumudu ushindani.

“Ni mapendekezo yangu kwamba kama shirika hili litaundwa upya, likapewa mtaji wa kutosha na likawa na uongozi bora, hakika litafanya kazi vizuri,” alisema Utouh.

CAG Utouh alitoa pendekezo hilo mjini Dodoma juzi wakati akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuwasilisha bungeni Ripoti ya Ukaguzi wa Hesabu za Serikali kwa mwaka wa fedha ulioishia Juni 30,2011.

Alisema ATCL kwa sasa haina ndege hata moja inayofanya kazi baada ya iliyokuwepo, kuanguka huko Kigoma wiki iliyopita wakati ikiruka.

Utouh pia amerejea pendekezo lake la kutaka wabunge wasiwe wajumbe wa bodi za wakurugenzi wa mashirika ya umma, kwani kwa kufanya hivyo watashindwa kuyasimamia.

“Serikali ichukue hatua kama alizochukua gavana wa Benki Kuu za kuwaondoa wabunge kwenye taasisi za fedha za umma ambazo ni mabenki na mifuko ya pensheni,” alisisitiza Utouh

Historia ya ATCL
ATCL ilianzishwa baada ya Shirika la Ndege la Tanzania ATC kuingia ubia na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA) mwaka 2002.

Hili ni moja ya mashirika ya ndege yaliyoonyesha kukua kwa kasi miaka ya 1980 na 1990 lakini lilianza kuyumba kutokana na uendeshaji mbovu na hali ikawa mbaya zaidi baada ya kuingia ubia na SAA.

Serikali iliingia ubia na SAA mwaka 2002 kwa matumaini ya kuifanya ATCL moja ya mashirika makubwa ya ndege Afrika lakini hali ikawa kinyume.

Kwenye mkataba huo, Serikali ilibaki na hisa 49 huku SAA ikimiliki hisa 51, ambazo zilimfanya mbia huyo kuwa na nguvu katika maamuzi mengi.

Septemba 2006, Serikali ilivunja mkataba na SAA baada ya kubaini kuzidi kudorora ATCL huku ikiandamwa na madeni makubwa.

Baada ya kuvunja mkataba huo, ATCL ilirejeshwa chini ya menejimenti ya wazalendo iliyokuwa inakabiliwa na changamoto nyingi yakiwemo madeni makubwa, ukosefu wa fedha, mishahara ya wafanyakazi na kutokuwa na ndege zinazofanya kazi.

Ndege mbili ilizokuwa nazo, zote zilikuwa za kukodi na zilifanya kazi kwa kusuasua kiasi cha kulifanya shirika hilo kusitisha safari kutokana na idadi ndogo ya abiria pamoja na ndege hizo kuwa na matatizo mara kwa mara.

Miaka mitatu iliyopita Serikali ilikuwa kwenye mkakati wa kuingia ubia mwingine na China lakini mpango huo baadae uliyeyuka.

UDOM haina mmiliki
Katika hatua nyingine CAG alisema katika ukaguzi wake amebaini kuwa majengo ya Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM) hayajulikani yanamilikiwa na nani kati ya Serikali na mifuko ya hifadhi ya jamii iliyotoa fedha za ujenzi.

Utoah alifafanua kuwa mifuko ya hifadhi za jamii inafahamu kwamba fedha zilizotumika kujenga majengo ya chuo hicho zilikuwa mkopo kwa Serikali wakati Serikali kwa upande wake inatambua kuwa fedha hizo zilikuwa ni uwekezaji wa mifuko hi

No comments:

Post a Comment