Wednesday, 2 November 2011

TUNA MATUMAINI MAKUBWA NA SALHA



Miss Tanzania 2011, Salha Israel amefanikiwa kuingia nusu fainali ya taji la Urembo wenye malengo maalum (Beauty with Purpose) yaliyofanyika juzi nchini Uingereza.

Akizungumza kutoka London jana, Salha alisema kuwa katika taji hilo, mrembo huyo aliwasilisha kazi yake ya Jamii aliyoifanya kwenye hospitali ya Muhimbili ambako alisaidia watoto wenye matatizo ambao wanazaliwa chini ya mwezi moja.

Salha alisema kuwa katika shindano hilo, Salha aliwakilisha DVD inayonyesha jinsi gani alivyomsaidia mtoto aliyezaliwa kwenye hospitali hiyo huku akiwa na kidonda kikubwa mgongoni. “Haikuwa kazi rahisi kwa majaji wa shindano hilo kuona ninavyofanya kazi ya kumsaidia mtoto huyo, ni kazi ambayo imewafanya waikubali kwani ipo katika majukumu ya Kamati ya Miss World mbali ya shindano lenyewe la urembo,” alisema Salha kwa njia ya simu.

Alisema kuwa amefarijika kuingia katika hatua hiyo ya 16 bora katika shindano hilo ambalo lilishirikisha jumla ya warembo 122 kutoka nchi mbali mbali. “Ninachokisubiri sasa ni fainali ya taji hili ambapo mshindi ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo ambayo itashirikisha si chini chini ya warembo 20,” alisema.
 

No comments:

Post a Comment