Thursday, 10 November 2011

BALOZI SEIF ALI IDDI AKUTANA NA BALAZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA




Balozi Mpya wa Japan Nchini Tanzania Bwana Masaki Okada. akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd Ofisini kwake Vuga

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameihakikishia Japan kwamba misaada inayotowa kwa Tanzania na Zanzibar kwa jumla itaendelea kutekelezwa kama ilivyopangwa.

Balozi Seif ametoa kauli hiyo hapo Ofisini kwake Vuga wakati wa Mazungumzo yake na Balozi Mpya wa Japan Nchini Tanzania Bwana Masaki Okada.

Alisema Misaada ya Nchi hiyo ukiwemo ule mkubwa wa Maji Safi ndani ya Mkoa wa Mjini Magharibi utawawezesha Wananachi na hata Wawekezaji kutumia huduma hiyo kwa ufanisi. Balozi Seif alimueleza Balozi Masaki kwamba Japan bado ina nafasi kubwa ya kusaidia Maendeleo ya Kilimo, Maji na hata Mafunzo katika Fani tofauti.

Hatua hii itaziwezesha pande hizo mbili kuendeleza kushirikiana katika ile dhana na uhusiano wa muda mrefu uliopo kati ya Zanzibar na Japan.

Akizungumzia Uwekezaji Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema Zanziba inahitaji Wawekezaji Kutoka Nchini Japan katika kuimarisha uchumi wake. Alisema ni vyema kwa Makampuni na Taasisi za Uwekezaji Nchini Japan zikaangalia uwezekano wa kufungua Miradi yao Zanzibar hasa katika Sekta ya Utalii ambayo hivi sasa ina wawekezaji wengi zaidi kutoka Nchi za Bara la Ulaya.

Kuhusu suala la Usafiri wa Baharini Balozi Seif aliiomba Japan kuangalia uwezekano wa kusaidia mpango wa SMZ wa Upatikanaji wa Meli kwa ajili usafirishaji Wananchi kati ya Visiwa vya Unguja na Pemba.

Balozi Seif alisema Zanzibar inahitaji Meli mpya kwa ajili ya kutoa huduma za uhakika zitakazoondoa hofu za wananchi ambao kwa sasa wanategemea usafiri wa Boti.

No comments:

Post a Comment