Tuesday, 25 October 2011

ZEC: Mahabusu na wagonjwa waruhusiwe kupiga kura Z`bar

 
 
Mwenyekiti wa Zec, Khatibu Mwinyichande

Tume ya Uchaguzi Zanzibar (Zec) imesema wakati umefika kwa mahabusu na wagonjwa waliyolazwa hospitalini wapewa nafasi ya kupiga kura wakati wa uchaguzi mkuu.
Hayo yamelezwa katika mapendekezo ya ripoti ya Uchaguzi ya Mwaka 2010 iliyotolewa na Mwenyekiti wa Zec, Khatibu Mwinyichande, jana.
Kwa mujibu wa mapendekezo hayo Mahabusu na wagonjwa waliolazwa hospitali wamekuwa wakikosa haki yakushiriki uchaguzi kutokana na sheria ya uchaguzi kutoeleza utaratibu wa watu hao licha ya kuwa na haki yao ya kikatiba
Ripoti hiyo imesema mujibu wa sheria ya uchaguzi mahabusu ni watu ambao bado hawajapatikana na hatia na wana haki ya kikatiba ya kupiga kura..
Aidha, ripoti imependekeza sheria ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar ya mwaka 1992 iandikwe upya kwa kuzingatia mabadiliko yote yaliyotokea tangu kutungwa kwa sheria hiyo na matakwa ya katiba Zanziabar ya mwaka 1984 ibara ya 119 (9) (13) ili iendane na mabadiliko ya demokrasia na na utawala bora.
Alisema sheria ya sasa haikueleleza utaratibu wa kupiga kura kwa wapiga kura ambao siku ya kupiga kura watakuwa wamepangiwa kazi kama Polisi, waangalizi wa ndani wa uchaguzi na madaktari.
Aidha, alisema kwamba sheria hiyo haijaeleza dhamana ya mgombea aliyewekewa pingamizi na kuondolewa katika orodha ya wagombea juu ya hatima ya fedha yake aliyokuwa ameweka zamani.
Ripoti hiyo inapendekeza kuanzishwa kwa mfuko maalum utakaowezesha tume hiyo kupata fedha nakuendesha shughuli zake katika muda mwafaka hasa katika kuuandikisha wapiga kura waliofikisha umri wa mika nane ambao wanahitaji kuingizwa katika daftari la kudumu la wapiga kura kila mwaka.
Aidha tume hiyo imependekeza utaratibu wa mgombea kulipia fumu sheria ibadilishwe na wagombea waanze fedha hizo wakati wa kuchuku fomu badala ya kurejesha.
Kwa mujibu wa sheria mgombea urasi unatakiwa kuweka dhamana ya Sh. milioni mbili, mgombea uwakilishi Sh. 200,000 na udiwani Sh.15,000.
Aidha ripoti hiyo imependekeza kila Mzanzibari mwenye haki ya kupata kitambulisho cha Mzanzibari mkaazi apewe bila ya usumbufu kwa vile kinatumika kama sharti la kuandikishwa kuwa mpiga kura kabla ya kufanyika kwa uchaguzi.
Katika uchaguzi uliopita wananchi wengi walilalamika kukosa haki ya kuandikishwa kuwa wapiga kura kutokana na urasimu wa viongozi wa serikalli za mitaa (Masheha) katika utoaji wa fomu za vitambulisho hivyo.
Hata hivyo Ripoti hiyo imesema uchaguzi huo kwa mujibu wa ripoti za wangalizi wa ndani na nje ulikuwa huru na haki licha ya kasoro ndogo ndogo zilizojitokeza.
CHANZO: NIPASHE

No comments:

Post a Comment