Rwanda Air kuanzisha safari za Zanzibar
na Mauwa Mohammed, ZanzibarBALOZI wa Rwanda nchini Fatma Ndangiza amesema shirika la ndege la nchi hiyo (Rwanda Air) limepanga kuanzisha safari kati ya Kigali na Zanzibar kwa lengo la kukuza utalii.
Alizungumza hayo jana katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Serikali ya Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, Migombani Zanzibar, alipokuwa akiagwa kumaliza muda wake wa kazi hapa nchini, Balozi Fatma alisema nchi mbili hizo zinaweza kutumia fursa hiyo kufanya shughuli za utalii kwa ushirikiano.
Alisema watalii wanaoingia Rwanda wanaweza kuja Zanzibar kwa usafiri huo wa ndega ya uhakika na wale wanaokuja Zanzibar wanaweza kwenda Rwanda.
Naye Maalim Seif alisema hatua hiyo ya kutaka kuanzishwa safari za moja kwa moja za ndege kuja Zanzibar kutoka Kigali ina umuhimu wa kipekee katika kukuza utalii.
Alisema hiyo ni fursa nzuri ya kibiashara na uwekezaji, pia wafanyabiashara watapata fursa ya kujitangaza

No comments:
Post a Comment