Friday, 8 July 2011

SERIKALI YA DENMARK KUJENGA MELI YA ABIRIA NA UCHUKUZI TANZANIA

Jovina Bujulu na Ismail Ngayonga
MAELEZO
Dodoma
SERIKALI chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Denmark (DANIDA) inatarajia kujenga meli mpya kwa ajili ya kurahisisha usafiri wa abiria na uchukuzi katika maziwa makuu nchini yakiwemo ziwa Tanganyika na ziwa Nyasa.
Akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Mpanda Vijijini (CCM) Mhe. Seleman Kasoko Bungeni mjini Dodoma leo , Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dkt. Athuman Mfutakamba alisema hatua za awali za mpango wa ujenzi huo tayari zimekwishaanza.
Alizitaja hatua hizo ni pamoja upembuzi yakinifu unaofanywa na kampuni ya OSK ya nchini Denmark.
Aidha alisema upembezi huo utahusu tathimini ya gharama kwa kila meli na aina ya meli inayofaa katika eneo la usafiri, na upembuzi huo unatajia kukamilika mwishoni mwa mwaka 2011.
Aliongeza kwamba Serikali inatambua matatizo ya hali ya usafiri katika maziwa makuu nchini ikiwemo ziwa Tanganyika, na Serikali imefanya jitihada za haraka ili kuhakikisha kuwa hali ya usafiri katika maeneo hayo inarejea katika hali ya kawaida.
Awali akijibu swali la msingi la mbunge huyo, Dkt. Mfutakamba alisema Serikali ya Ujerumani imetoa kiasi cha Tsh Bilioni 16 kwa ajili ya matengezo makubwa ya meli ya Mv. Liemba pamoja na Serikali kurekebisha tatizo lililokuwepo hapo awali la Meli ya Mv. Mwongozo.
Katika swali lake la nyongeza Mbunge huyo alitaka kujua mikakati ya Serikali ya kuboresha usafiri wa melki katika ziwa Tanganyika ili kurahisisha huduma hiyo kwa wananchi wa maeneo yanayozunguka ziwa Tanganyika

No comments:

Post a Comment