| Bakhresa washusha bei ya unga |
![]() |
| Patricia Kimelemeta KAMPUNI ya Said Salim Bakhresa imepunguza bei ya unga wa mahindi inayozalisha kutoka Sh950 mpaka Sh600 iliyopangwa na serikali kwa ajili ya wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Said Muhamad alisema punguzo hilo limetokana na serikali kuwapa tani 300 za mahindi ili wakoboe na kuuza bei ya serikali ya Sh600 kwa kilo. Alisema wananchi wanaohitaji kununua unga kwa bei hiyo wanapaswa kununua viroba vitano vya kilogramu 25 kwenye maduka ya kampuni hiyo. “Tunawakaribisha wananchi kununua unga kwa bei ya serikali kutoka Sh950 mpaka Sh600 kwa kilogramu, jambo ambalo tunaamini wananchi watanufaika,”alisema Muhamad. Alisema wananchi wanapaswa kwenda makao makuu ya ofisi zao za Bakhresa zilizoko kwenye maeneo tofauti jijini ili kununua bidhaa hiyo. Alisema kutokana na hali hiyo wauzaji wa rejareja wanapaswa kuuza kwa bei hiyo kwa sababu mahindi hayo ni ya msaada hivyo basi hawapaswi kupandisha bei. Kwa mujibu wa Muhamad, bidhaa wanazozitengeza kwenye kiwanda chao zina ubora unaohitajika, jambo ambalo limewafanya wauze ndani na nje ya Bara la Afrika. |

No comments:
Post a Comment