Shamsi Nahodha aapishwa kuwa Mwenyekiti tume ya Usuluhishi
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha
Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amemwapisha Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha (pichani), kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Usuluhisho wa Migogoro ya Jeshi la Polisi na Magereza.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam baada ya kuapishwa kiapo hicho, Nahodha alisema kuwa kazi kubwa ya tume hiyo ni kusimamaia usuluhisho wa migogoro.
Alisema ataisimamia vyema tume hiyo na kuhakikisha kuwa inafanya kazi kwa mujibu wa sheria bila kuwepo na upendeleo wowote.
“Nitafanya haki kwa kuzingatia sheria kwani chombo hicho kazi yake ni kusimamia upatikanaji wa haki kwa wananchi na sio vinginevyo,” alisema Nahodha.
Nahodha alisema tume hiyo itakuwa inashughulikia kesi za kazi ikiwemo kusimamia rufaa zinazokatwa.
No comments:
Post a Comment