*Ni baada ya kumkagua kibaka *Alirubuni kwa vivazi vya kike Na Waandishi Wetu, Mbagala WAKAZI wa Mbagala jana walishikwa na bumbuwazi baada ya mwanamume mmoja anayedhaniwa kuwa kibaka kunaswa akiwa amevaa mavazi ya kike. Tukio hilo limetokea jana saa 4 asubuhi katika nyumba ya Rose Andrea ambapo kijana huyo, baada ya kubanwa ndani ya nyumba hiyo, alijitetea kuwa amekwenda kutoa taarifa za msiba. Akisimulia tukio hilo mwenye nyumba hiyo, Rose amesema akiwa njiani akimpeleka mtoto shule ghafla alishtuka kuwa amesahau maji ya kunywa na ndipo alipoamua kugeuza kurudi nyumbani. Mara baada ya kugeuza alishangaa kumuona mwanamke akiwa amevalia suruali yake maridadi huku akiwa amejipamba kwa ‘shedo’ na mapambo mengine ya kike. Kuona hivyo, mwenye nyumba huyo aliamua kupiga mayowe kuomba msaada na ndipo walipojitokeza wananchi mbalimbali na baada ya kumhoji mtuhumiwa huyo alidai kuwa amefika katika nyumba hiyo kwa ajili ya kutoa taarifa za msiba wa jirani na nyumba hiyo. Hata hivyo, baada ya kumchukua na kumpeleka katika nyumba ya msiba ambayo kuna mpemba amefariki walikana kumfahamu kijana huyo na ndipo walipoamua kumfikisha kituo cha Polisi cha Maturubai Mbagala. Wakati polisi wakijiandaa kumfanyia upekuzi kama kuna kitu aliiba katika nyumba ile kijana huyo alianza ubishi jambo lililosababisha polisi wa kike aliyekuwa akimkagua kuomba nguvu ya ziada kwa wenzake. Mara baada ya polisi wengine wa kike kumvamia mtuhumiwa huyo ndipo walipobaini kuwa, kumbe ni mwanamume na si mwanamke kama ambavyo alikuwa amevalia mavazi yale. Mwanamume huyo awali alijitambulisha kuwa ni Fatma Ramadhan mkazi wa Gongo la Mboto Mzambarauni na baadaye ilibainika kuwa, ni Mussa Ramadhan. Mtuhumiwa anashikiliwa na polisi na atafikishwa Mahakamani baada ya upelelezi kukamilika. |
Kheri yote inapatikana pale Mwenyezi Mungu anaporidhika na mja wake, na funguo za kheri zimo katika Dua pamoja na unyenyekevu kwa Mwenyezi Mungu na kuonesha kumpenda kwa kutenda yale yanayomridhisha na pia kumuogopa kwa kuepukana na makatazo yake. Mja anapokabidhiwa na Mola wake funguo hizi basi ajue kuwa Mola wake anamtakia kheri, na anaponyimwa basi ajue kuwa amefungiwa milango ya kheri
Tuesday, 25 January 2011
Polisi wa kike wakumbwa na kiwewe
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment