Wednesday, 26 January 2011

Mtatiro: Uchaguzi ukirudiwa CUF itashinda Tandahimba

 

Chama Cha Wanachi (CUF), kimedai kuwa kitalitwaa jimbo la Tandahimba mkoani Mtwara ikiwa kitapata ushindi katika kesi waliyoifungua Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga matokeo yaliyompa ushindi mbunge wa sasa kupitia CCM, Juma Njwao.
Msimamo huo ulitolewa hivi karibuni jimboni humo na Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, Julius Mtatiro, alipowahutubia wananchi wa jimbo hilo katika mikutano mbalimbali ya hadhara.
Mtatiro alisema CUF kina uhakika wa kufanya vizuri na kutwaa ubunge katika jimbo hilo kutokana na wananchi wengi kuonyesha moyo wa kukiunga mkono.
Aliwahakikishia kuwa CUF kipo pamoja nao na kuwataka wawe wavumilivu wakati kesi waliyoifungua mahakamani ikiendelea kuunguruma.
Alisema jimbo la Tandahimba ni ngome ya chama hicho hivyo ana uhakika ikiwa watamsimamisha aliyegombea mwaka jana, Katani Ahmed Katani, atapata ushindi.
Mwaka jana Njwao wa CCM alishindana na mgombea wa CUF katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba.
Kama noma na iwe noma piga ua garagaza ushindi wa Katani ni lazima katika jimbo hili la Tandahimba,” alisema Mtatiro.

No comments:

Post a Comment