Friday, 28 January 2011

 Malindi itakuwa Bandari ya Kimataifa-SMZ





SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imesema ina lengo la kuifanya bandari ya Zanzibar kuwa inakidhi viwango vya kimataifa kuanzia mwezi Mie mwaka huu.
Akijibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Jimbo la Kitope Makame Mbarouk Mshimba, Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano, Hamad Masoud Hamad alisema kazi ya kutafuta vifaa kwa ajili ya kuboresha huduma katika bandari hiyo imeanza.
Alisema nia ya mpango huo ni kuiwezesha bandari hiyo kuwa na vifaa vyote kwa ajili ya huduma muhimu, vikiwemo vya uokozi wakati wa matukio ya ajali.
Makame alitaka kujua mpango wa serikali kuiwezesha bandari ya Zanzibar kuwa na vifaa vya kisasa kwa ajili ya shughuli za uokoaji wakati wa matukio ya ajali na vya utoaji wa mizigo ili kuondoa msongamano.
“Tumeanza kutafuta “crane” itakayotusaidia kurahisisha upakuaji wa mizigo bandarini,” alisema Makame bila kutaja muda utakaotumika kutafuta na kuvileta Zanzibar vifaa hivyo.
Mapema Naibu Waziri wa Miundombinu na Maswasiliano, Issa Haji Ussi, akijibu swali la msingi la Mbarouk Wadi Mussa (Mkwajuni) alisema Bandari ya Malindi ina uwezo wa kuhudumia meli za aina mbali mbali za mizigo mchanganyiko.
Alisema meli hizo ni pamoja na zinazosafirisha makontena, mafuta, magari na vifaa vya kijeshi, zikiwemo zenye urefu wa hadi kufikia mita 200 (LOA) na ukubwa wa GRT 26,000 na uzito wa tani 13,000 (DWT) nah ii ni kwa kuzingatia ukubwa wa gati.
Hata hivyo Ussi alisema bado bandari haijajitosheleza kwa vifaa vya kutosha kukidhi mahitaji ya kuharakisha utoaji wa mizigo bandarini hapo.
“Tagi zinazotumika hivi sasa kusaidia ufungaji wa wa meli zina uwezo mdogo kulinganisha na ukubwa wa meli zinazokuja Zanzibar,” alisema Ussi.

No comments:

Post a Comment