Majaribio kwenye eneo la gesi la Pweza yamekamilika; hifadhi ya gesi yenye ubora wa juu imethibitishwa
BG Group leo imetanganza kukamilisha kikamilifu majaribio ya uchimbaji kwenye eneo la gesi la Pweza ndani ya bahari kusini mwa Tanzania, na kuhitimisha programu kubwa ya kufanya tathmini kwenye Kitalu namba 4. Hii inathibitisha matarajio ya ubora katika hifadhi hii ya gesi asilia na kufanya maendeleo chanya.
Hifadhi ya gesi ya Pwezainakadiriwa kuwa kilometa 70 kutoka kwenye pwani ya Tanzania kwenye kina cha maji cha meta1 400 . Matokeo ya awali kutoka kwenye majaribio ya uchimbaji wa gesi kwenye kitalu namba 3 cha Pweza yamethibitisha kuwepo na hifadhi ya gesi yenye ubora wa hali juu, Majaribio ya uchimbaji ni utaratibu unaokubalika katika shughuli za utafutaji wa gesi, na ni utaratibu unaotumika katika kubaini ubora wa hifadhi ya gesi.
Majaribio matatu yalifanyika katika hifadhi ya gesi ya Pweza , jaribio la kwanza lilifanyika kwenye Kitalu namba 4, ambapo mtiririko wa gesi ulikuwa katika kiwango cha futi za ujazo milioni57 cha gesi kwa siku, kulingana na uwezo wa mwisho wa kifaa kilichotumika katika majaribio ya uchimbaji. Muhimu zaidi, majaribio haya yameonyesha kwambavisima vitakavyochimbwa kwa uzalishaji vinaweza kutiririka gesi kwa kiwango cha juu na kwamba hifadhi ya gesi ya Pweza kimsingi ina uzalishaji mkubwa kulinganisha na visima vingine vilivyochimbwa na kampuni ya BG Tanzania.
Rais na Meneja Mkuu wa kampuni ya BG Afrika Mashariki, Derek Hudson,alisem“Tumefurahishwa na matokeo ya majaribio yetu na tathmini katika Kitalu namba 4 cha gesi;kuna raslimali za gesi za futi za ujazo wa trilioni4 (tcf). Kazi iliyofanyika inaonyesha gesi yenye ubora wa hali ya juu kwenye maeneo hayana tunaendelea kushirikiana na washirika wetu Serikalini na katika sekta binafsi kuhusumatarajio ya kuweka mtambo wa Gesi Asilia (LNG) , ambapo uzalishaji kutoka kwenye vitalu hivi vya gesi utakuwa ukitegemea mtambo huu.”
Majaribio haya katika kisima cha Pweza pia yamethibitisha rasilimali ya gesiambapo kampuni ya BG hivi karibuni imetangaza kuwa na raslimali za jumla za gesi nchini Tanzania zinazofikia futi za ujazo trilioni13.
Meli ya uchimbaji katika kina kirefu iliyokodiwa na kampuni ya BG iitwayo Deep SeaMetro-1kwa sasa imehamiaupande wa kusini katika Kitalu namba 1ambapo inafanya uchimbaji wa tathmini (appraisal) kwenye eneo jingine ilipogunduliwa gesi liitwalo Mzia.
No comments:
Post a Comment