Thursday, 23 June 2011

URUSI YAKIRI KUWA RUBANI NDIYE MWENYE MAKOSA KATIKA AJALI YA NDEGE




Ndege ya Shirika la RusAir iliyoanguka mapema wiki hii na kuuwa watu arobaini 44 nchini humo.

Wakati wachunguzi nchini Urusi wakijaribu kutafuta sababu ya kuanguka kwa ndege kaskazini mwa nchi hiyo ambayo iliuwa abiria 44 , naibu waziri mkuu wa nchi hiyo ameelekeza lawama zake katika ajali hiyo kwa rubani.

Sergei Ivanov amesema rubani wa ndege hiyo alijaribu kuangalia njia ya kutua ndege bila ya kutumia vifaa wakati wa hali mbaya ya hewa.

Ndege hiyo ya shirika la ndege la RusAir kutoka Moscow ilijaribu kutua katika uwanja wa ndege wa Petro-za-vodsk siku ya Jumatatu, lakini ilishindwa kupata njia ya kutua na badala yake ikaanguka katika barabara ya kawaida kiasi cha kilometa moja kutoka uwanja wa ndege.

Msemaji wa wizara inayoshughulikia masuala ya dharura amesema kuwa saba kati ya watu wanane walionusurika wako katika hali mbaya , na wanatibiwa majeraha ya kuungua.

No comments:

Post a Comment