SMZ yapoteza Dola Millioni 16
Na SalmaSaidWAZIRI wa Biashara Viwanda na Masoko, Nassor Ahmed Mazrui amelieleza baraza la wawakilishi kwamba katika kipindi cha miaka 10 iliyopita, serikali imepoteza kiasi cha dola za Marekani millioni 16, kutokana na vitendo vya usafirishaji nje kwa magendo ya zao la karafuu.
Mazrui alisema magendo ya karafuu yamekuwa yakiathiri kwa kiasi kikubwa mapato ya Serikali katika zao hilo kutokana na kuwa zao hilo kuuzwa nje ya nchi na kutia hasara kubwa kwa serikali ambapo aliwaeleza wajumbe wakati akichangia bajeti ya serikali ya mwaka 2011/2012.
Waziri huyo alisema vitendo vya usafirishaji magendo karafuu nje ya Zanzibar vimekuwa na athari kubwa kwa uchumi wa Zanzibar kutoka na kuikosesha mapato serikali.
Mazrui alisema usafirishaji magendo wa zao la karafuu limeishanya nchi yake Kenya kuwa muuzaji mashuhuri wa zao la karafuu kwa zaidi ya tani 2,000 katika soko la dunia huku ikizingatiwa kuwa katika nchi hiyo hakuna mikarafuu inayolimwa.
“Nawasihi sana, tuache kuuza karafuu kwa magendo, zao la karafuu litumike kuwanufaishana wananchi wa Zanzibar. Serikali itapandisha bei nzuri sana na ni lengo letu kukifufua kilimo cha karafuu”, alisema waziri huyo.
Alisema kasi ya magendo imeongezeka ambapo zipo baadhi ya nchi zimekuwa zikisafirisha na kuuza karafuu nje ya nchi wakati hazizalishi karafuu hizo.
Mazrui alisema kwamba karafuu hizo zinazouzwa na nchi hizo jirani ni karafuu zinazotoka nchini za magendo jambo ambalo linatia linahitaji kushughulikiwa na wananchi wote.
Alitoa habari njema kwa wananchi na wakulima wa karafuu na kusema kwamba bei ya karafuu katika soko la dunia ni nzuri hivyo wakulima waongeze kilimo hicho kwa kuwa kina tija kubwa.
Aidha aliwataka wakulima wa karafuu Unguja na Pemba kuongeza kasi ya kulima zao hilo ambalo tija yake kwa wananchi ni kubwa na litainua kipato cha wananchi wengi.
“Serikali inatoa wito kwa sasa ni kuwataka wakulima wa zao la karafuu kuongeza nguvu ya kilimo hicho kwani bei yake katika soko la dunia ni kubwa na ni bora kazi ya kuongeza zao la karafuu izidi kwa saabu kuna faida kwa wananchi wetu” alisisitiza Mazrui.
Bei ya karafuu kwa wakulima wa soko la ndani nchini ni kilo moja shilingi 5,000 kwa karafuu ya daraja la kwanza huku daraja la pili na kuendelea kwenda chini ni chini ya bei hiyo ambapo wananchi wengi wanalalamikiwa kazi kubwa yenye kipato kidogo.
Zao la karafuu limekuwa likiendelea kudhibitiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo huuzwa kupitia kwa Shirika la Taifa la Biashara (ZSTC).
Hata hivyo kilio kikubwa cha wakulima pamoja na jumuiya zinazojishungulisha na kilimo cha zao hilo wanataka kuona kwamba zao la karafuu linabinafsihwa na kuingia katika soko huria.
Mazrui akizungumzia suala la Zanzibar kuwa bandari huru, alisema kuna kampuni imeajiriwa kulifanyia utafiti la kuifanya Zanzibar kuwa ni miongoni mwa eneo tengefu kiuchumi.
Aliwaahidi wajumbe wa baraza hilo kwamba baada ya ripoti kukamika itawasilishwa katika baraza la wawakilishi kupata michango ya viongozi hao na kuifanya Zanzibar kuwa nchi itakayokuwa uchumi wake unakuwa kwa kasi kubwa.
Akizungumzia juu ya tatizo la upandaji ovyo wa bei za vyakula alisema upo mpango ambao utahakikisha uwekaji wa bei za bidhaa muhimu za vyakula unashirikisha baina ya serikali na wafanyabishara.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Baraza la Mapinduzi Dk Mwinyihaji Makame Mwadini alisema kilimo cha karafuu bado ni mkombozi wa uchumi wa Zanzibar.
Dk Mwadini alisema zao la karafuu bei yake katika soko la dunia bado ni nzuri na kuwataka wakulima kuendelea kuimarisha kilimo hicho kwa wingi hasa kwa siku za baadae.
Alisema kazi kubwa ambayo inatakiwa kufanywa kwa sasa ni kupanda mikarafuu mipya ambayo itachukuwa nafasi ya mikarafuu ya zamani ambayo imechoka kwa sasa.
Waziri huyo alisema kwamba miti ya mikarafuu inachukuwa muda mrefu kuota vizuri katika mashamba ya wakulima,na kuwataka wakulima kubadilika na kutumia mbinu za kisasa za kilimo.
Akichangia bajeti hiyo Waziri wa Ardhi Makazi Maji na Nishati, Ali Juma Shamuhuna alisema serikali ya awamu ya saba iaendelea na msimamo wake kwamba mafuta na gesi asilia lazima yatolewe katika orodha ya mambo ya Muungano.
Waziri huyo alisema shindikizo la kutaka kuiondoa rasilimali hiyo katika mamlaka ya Muungano lazima lipigwe na lifikishwe Bungeni kwa ajili ya kuondolewa kwani suala la uchumi si katika mambo ya Muungano.
Alisema katika visiwa vyote vya Unguja na Pemba kana akiba kubwa ya gesi asilia na wala hakuna ubishi wa kufanywa utafiti wa mafuta kwani yapo ya kutosha.
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Fatma Abdulhabib Ferej alisema kutokana na serikali kutopandisha kodi, ni vyema msisitizo na mkazo ukawekwa katika kudhibiti mvujo wa mapato, wigo wa kuongezwa ukusanyaji mapato, kuondosha misamaha ya kodi pamoja na kupunguza matumizi ya serikali.
Aidha waziri huyo alionesha kuridhishwa kutokana na bajeti huyo kutoa vipaumbele zaidi katika sekta za jamii ikiwemo afya, elimu na maji huku akisema hukuwa hizo ndizo kero zinazowakabili Wazanzibari.
MADAKTARI KUTOJUWA KIINGEREZA
WIZARA ya Afya Zanzibar imesema madaktari wote wa kigeni wanaokuja nchini kufanya kazi wanafahamu lugha ya kiingereza kwa ajili ya mawasiliano ingawa baadhi yao hawajui vizuri lakini wanaweza kuwasiliana na wagonjwa.
Naibu Waziri wa Afya Dk Sira Umbwa Mamboya amewaambia wajumbe wa baraza la wawakilishi wakati akijibu swali la msingi la Mwakilishi wa Jimbo la Wawi (CUF) Saleh Nassor Juma aliyetaka kujua kwa nini madaktari wengi wa kigeni wanaokuja nchi kufanya kazi hawafahamu lugha ya kiingereza.
Dk Sira alisema kwamba serikali inapokea madaktari wengi kutoka nchi mbali mbali za nje ikiwemo Cuba pamoja na China lakini wanapofika hapa nchini hufundishwa lugha rahisi ya mawasiliano licha ya kuwa hawafahamu kiingereza lakini kiinereza cha kuwasiliana wanakifahamu.
“Kwa kawaida madaktari wote wa kigeni wanaokuja hapa nchini kutoka nchi za nje wanajua kiingereza hata kama sio kizuri” alisema naobu waziri huyo.
Alisema kinachotakiwa wakati wa kutoa huduma kwa wagonjwa waambatanishwe na wafanyakazi na madaktari wazalendo wengine kwa ajili ya kutoa huduma mbali mbali.
“’Hilo tatizo lipo lakini kama madaktari hao wataalamu hawafahamu lugha basi tunawaambatanuisha na madaktari wazalendo na pale sio pahala pa mazungumzo lugha ya vitendo wanaifahamu na wanafanya kazi zao bila ya matatizo sasa mnataka wafanye nini na wao wakiingia katika upasuaji wananyoosha mkono wanapewa mkasi …wakinyoosha ena mkono wanapokewa mkasi ….sasa?’alihoji naibu waziri huyo.
Hata hivyo alisema wizara haina mpango wa kutenga muda kwa ajili ya kufundisha madaktari hao lugha ya kiswahili kwa kufanya mawasiliano na wagonjwa kwa kuwa kipindi wanachokuja kufanya kazi hapa nchini ni kifupi hivyo wizara haiwezi kumega muda wao wa kufanya kazi wakautumia kwa ajili ya kuwasomesha lugha ya kiswahili.
Awali Mwakilishi wa Wawi alisema hospitali za Zanzibar ikiwemo hospitali ya chakachake mara nyingi hutegemea madaktari wa kigeni kutoka Cuba na kwa kuwa baada ya kufanya uchunguzi imebainika kuwa baadhi ya madaktari hao hawafahamu Kiswahili wala kiingereza jambo ambalo linaleta usumbufu kwa wagonjwa na hata madaktari wenzao.
Mwakilishi huyo alihoji kwa nini madaktari hao hawapewi mafunzo ya lugha ya Kiswahili wanapoingia nchini ili waweze kuelewana na wagojwa na badala yake wanawasumbua wananchi katika kuwasiliana kwa kutokujua lugha ya Kiswahili wala kiingereza.
Naibu waziri huo alisema ni kweli kwa kawaida madaktari wengi wanaokuja nchini hawafahamu lugha ya kiingereza ingawa wapo ambao wanafahamu vizuri na wanaweza kufahamiana na wagonjwa.
Naye Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF) Hijja Hassan Hijja alisema kamati yake ya ustawi wa jamii ilipokuwa ikifanya kazi ilifana mahojiano na madaktari mbali mbali akiwemo daktari dhamana wa hospitali hiyo chakacheke ambapo alisema madaktari hao hawafahamu kabisa kiingereza na kuleta usumbufu mkubwa kwa wagonjwa wanaofata huduma pale hospitali kutokanana kutofahamiana na madaktari hao wageni hivyo ipo haja ya serikali kuimarisha chuo chake cha Afya ili kutoa elimu ya digirii ya kwanza ili kupunguza wimbi la madaktari kutoka nje.
Naibu waziri hata kama serikali itafungua chuo chake bado madaktari kutoka nje ya nchi watahitajika kwa kuwa Zanzibar bado ina upungufu wa madaktari kutokana na kuwa wanapomalzia kusoma hukataa kufanya kazi nchini kwa kisingizio cha maslahi madogo.
SMZ HAINA SHERIA YA RUSHWA
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema kwamba hadi sasa hakuna sheria ya maadili ya viongozi na kuzuwia rushwa kwa watumishi wa serikali kwa sheria hiyo haijaanzishwa.
Hayo yalisemwa na Kaimu Waziri wa Nchi Afisi ya Rais, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Dk Mwinyihaji Makame Mwadini wakati akijibu swali aliloulizwa na Mwakilishi wa Jimbo la Kiwani (CUF)Hijja Hassan Hijja aliyetaka kujuwa serikali imefikia wapi kuhusu kuwepo kwa sheria ya kuzuwia rushwa Zanzibar.
Dk Mwadini alisema kwamba sheria haipo lakini serikali imeamuwa kulifanyia kazi suala hilo kwa kuwa sio jambo la kulichukulia mashara kwa kuwa linahitaji muda na mazingatio makubwa hasa kwa kuzingatia huko Tanzania bara ambao wameanzisha lakini taarifa zilizopo wapo watu wanashitakiwa kwa kutokwenda kuorodhesha mali zao.
Alisema sheria ya kuzuwia rushwa na kusimamia maadili itakapopitishwa serikali itawajibika kutangaza mali kwa viongozi wa serikali.
Mwadini alisema kwamba suala hilo limekuwa gumu utekelezaji wake tangu awamu iliyopita kutokana na kuwepo kwa fitina na watu kutafutana.
‘Mheshimiwa spika hili ni suala gumu sana….kuna fitina ndani yake hata wabunge kule walichukuwa muda mrefu kutekeleza sheria hiyo na kama mnavyosikia wengine wanaitwa kujieleza kwa sababu tu hawajenda huko” alisema.
Waziri huyo alisema hivyo wakati alipojibu swali la nyongeza la Mwakilishi wa Chakechake (CUF) Omar Ali Shehe aliyetaka kujuwa suala hilo kwa nini limechukuwa muda mrefu utekelezaji wake tangu awamu iliyopita.
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika mwaka 2000 iliunda wizara ya katiba na utawala bora ambayo miongoni mwa majukumu yake ni kuanzishwa kwa mamlaka ya kuzuwia rushwa.
Aidha Serikali imesema kwa sasa imeliona tatizo la kuwepo kwa tofauti ya mishahara kwa watumishi wa Serikali katika viwango mbali mbali,ambapo suala hilo linafanyiwa kazi.
SIO KILA MTU ANAWEZA KUWA JAJI
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema mtu yeyote hatoweza kuteuliwa kuwa Jaji wa Mahkama Kuu mpaka awe na sifa zilizoelezwa ndani ya katiba hivyo rais analazimika kikatiba kuhakikisha kwamba mteuliwa amekamilisha zifa zote.
Waziri wa katiba na sheria Abubaka Khamis Bakari akijibu suala la msingi lililoulizwa na mwakilishi wa jimbo la chaani Usi Jecha Simai aliyeataka kujua mbali na sifa zilizomo ndani ya katiba je, Mhe rais analazimika kuhakikisha kwamba mteuliwa amekamilisha sifa zote au anaweza kwa busara zake kuteua hata kama mteuliwa hakutimiza sifa zote?.
Waziri bakari amesema majaji wa Mahkama kuu watateuliwa na rais kutokana na mapendekezo ya Tume ya utumishi wa Mahkama.
Hata hivyo alisema mtu yeyote hatoweza kuteuliwa kuwa jaji wa Mahkama kuu mpaka awe na shahada ya sheria ya chuo kikuu kinachotambulika au chuo cha aina hiyo.
Samba na hilo awe amaewahi kuwa jaji wa Mahkama zilizofanana na mahkama kuu ya Zanzibar kwa kesi zote za jinai na madai katika Tanzania au sehemu yaeyotae ile ya Jumuiya ya Madola au mahkama yenye mamlaka ya Rufaa katika Mahkama hizo.
Aidha awe ni mwansheria wa Zanzibar au Tanzania kwa kipindi kisichopungua miaka saba.
Hata hivyo Waziri huyo alieleza kuwa Wizara yake haifahamu ni sababu zipi ambazo zilipelekea Jumuiya ya wanasheria Zanzibar kuelezea kwamba uteauzi wa Majaji hao haufai kisheria.
Alisema kwa mujibu wa kifungu cha 94 (2) cha katiba ya Zanzibar ya 1984 kinaelezea kuwa jaji mkuu atateuliwa na rais kutoka miongoni mwa Majaji wa Mahkma kuu na baada ya kushauriana na Tume ya Utumishi wa Mahkama.
Majibu hayo yamekuja baada ya Mwakilishi wa Chaani Ussi Jecha (CCM) kutaka kujua sababu zilizopelekea Jumuiya ya wanasheria Zanzibar kushauri kwamba uteuzi huo haufai kisheria.
SERIKALI KUTOA MAKAAZI
SERIKALI imesema itaweka umuhimu wa kuwapatia waananchi wa kipato cha chini nyumba za kuishi kwa kuzingatia mahitaji halisi ya kila muhusika na itahakikisha nafasi ya mwanzo inatolewa kwa yule mwenye shida ya kweli ya makazi .
Naibu Waziri wa Ardhi, Makazi, Maji na Nishati Haji Mwadini alipokuwa akijibu suala la msingi aliloulizwa na Mwakilishi wa nafasi za wanawake, Mgeni Hassan Juma (CCM) aliyetaka kujua, Wizara imejipanga vipi katika kuhakikisha wananchi wanapata nyumba za makaazi.
Naibu Waziri huyo amesema kwa kuwa utekelezaji wa sera ya nyumba serikali imejipanga kuwapatia wananchi wa visiwa vya Unguja na Pemba makazi bora na salama .
Amesema kaatika kutekeleza mpango huo serikali imetenga maeneo mbali mbali kama vile Binguni, Kibuteni na Chuini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za kisasa za makazi kwa upande wa Unguja.
Na kwa upande wa Pemba serikali inandaa maeneo ili kufanikisha mpango huo wa ujenzi wa nyumba za makaazi
Aidha alisema nyumba hizi zinatarajiwa kujengwa na
wawekezaji mbali mbali wa nje na ndani ambao serikali imefanmya jitihada za kuwashajihisha .
Hivi sasa tayari baadhi ya wawekezaji wamejitoleza na mazaungumzo yanaendelea ili kufanikisha mpango huo wa ujenzi wa nyumba za makaazi.
No comments:
Post a Comment