Changamoto za maji safi
Hayo yalielezwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe Balozi Seif Ali Iddi katika mazungumzo yake na Balozi wa Marekani nchini Tanzania Mhe Alfonso E. Lenhardt aliyefika Ofisini kwa Makamu huyo kuagana naye, baada ya kumaliza muda wake hapa nchini.
Alisema upungufu au uhaba wa maji katika maeneo mengi ya Zanzibar umeleta kero kubwa kwa jamii ya Wazanzibari na hata kuchangia miripuko ya maradhi kwa baadhi ya sehemu hasa katika nyakati za mvua
Hivyo aliiomba Serikali ya Marekani kuangalia uwezekano wa kuliingiza suala hilo katika mpango wake wa misaada kwa Zanzibar katika kipindi kijacho.
Ambapo aliafiki ushauri wa Balozi Lenhardt wa kutumia maji ya bahari kwa ajili ya kunjwa na kuitaka kampuni husika kuja fanya mazungumzo juu ya mradi huo.
Halikadhalika Mhe Balozi Iddi alieleza changamoto nyengine na namna Serikali ilivyojipanga kuzishughulikia ikiwemo mipango imara ya kuimarisha kilimo cha umwagiliaji na zao la karafuu, uvuvi, umeme na Viwanda vidogo vidogo.
Kuhusu tatizo la Maji Balozi Alfonso Lenhardt alisema tatizo la maji kwa Zanzibar linaweza kutatuka iwapo Serikali itaweza kutumia maji ya bahari yaliokizunguuka kisiwa kizima, ingawa mradi huo utakuwa na gharama kubwa mwanzoni.
Hivyo aliishauri Zanzibar kuelekeza azma hiyo kama mojawapo ya njia la kulimaliza kabisa tatizo hilo na pia alieleza hatua za matayarisho yaliyofikiwa katika utengenezaji wa waya wa Umeme wa MCC kutoka bara
No comments:
Post a Comment