Tuesday, 8 March 2011

Wananchi wazuiwa kwenda Lolilondo

Patients get their dose of the ‘magical’ healing potion from a medicineman, Mr Ambilikile Masapila (right), at Samunge Village, Digo-Digo ward, Ngorongoro District, at the weekend. Thousands of people continue to flock the remote Sonjo plains in search of the wonder drug. (Photo by Marc Nkwame)

Patients get their dose of the ‘magical’ healing potion from a medicineman, Mr Ambilikile Masapila (right), at Samunge Village, Digo-Digo ward, Ngorongoro District, at the weekend. Thousands of people continue to flock the remote Sonjo plains in search of the wonder drug.
*Ni kwa yule mchungaji anayeponya magonjwa
*Serikali sasa yajipanga kuimarisha ulinzi


Christina Gauluhanga na Stella Aron, jijini

KUTOKANA na umati wa watu kufurika kwa ajili ya kwenda kupata tiba ya jadi ya magonjwa sugu inayotolewa kwa gharama ya sh. 500 tu Loliondo mkoani Arusha, Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Elius Wawa Lali, amelazimika kuingilia kati na kuwazuia wananchi kufika eneo hilo.

Akizungumza leo asubuhi katika mahojiano maalumu kwenye kipindi cha Nipashe, Lali amesema amefikia hatua hiyo baada ya kuona kuna hali ya hatari inaweza ikatokea wakati wowote.

Amesema tangu kutangazwa kwa dawa hiyo kumekuwa na makundi makubwa ya wananchi kutoka mikoa mbalimbali na nchi jirani wanaofika kupata huduma hiyo, hali ambayo imesababisha kuwapo kwa msongamano wa watu na kusababisha ugumu wa usafiri pamoja na kupanda kwa gharama za maisha, hususan nyumba za kulala wageni na vyakula.

Amesema hivi sasa soda inayouzwa sh. 500 sasa inauzwa sh. 1,000 na maji ya kunywa ni sh. 2000 huku mahitaji mengine yakiwa juu.

Ameongeza kuwa kutokana na msongamano huo kumekuwa na taarifa za wagonjwa wengi kuelekea kwa mchungaji mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile, umbali wa zaidi ya kilomita 400 kutoka Arusha mjini na kusababisha ukosefu wa usafiri kwa watalii.

Amesema wamiliki wengi wenye magari aina ya Toyota Land Cruiser na Land Rover 110 wamelazimika kuyapeleka magari yao huko ambapo madalali wamepandisha nauli kutoka sh. 60,000 hadi sh. 125,000 kwa mtu mmoja na kusababisha watalii kushindwa kupata usafiri.

Mkuu wa wilaya hiyo amesema pia tangu kuwapo kwa taarifa hizo ndugu za wagonjwa wenye virusi vya UKIMWI, saratani, kisukari na pumu waliokuwa wamelazwa hospitalini wameondolewa na kuwapeleka kwa mchungaji huo hali ambayo imechangia kukosekana kwa usafiri wa kurudi.

Amesema msururu na foleni umesababisha wagonjwa wengine kukosa huduma na kupoteza maisha ambapo ilimlazimu mchungaji huyo kusaidiwa na wachungaji wengine. Hata hivyo, hali ilizidi kuwa mbaya kutokana na idadi ya watu wanaotaka huduma kuongezeka.

Mchungaji huyo ambaye anatoa tiba hiyo ya maji mara moja na inadaiwa kuwa kwa wenye virusi vya HIV hutibu baada ya siku 21 ambapo kwa wenye kisukari inadaiwa wanapona mara moja baada ya kuinywa dawa hiyo.

Mchungaji huyo amesema alioteshwa dawa hiyo ya uponyaji ambayo inatokana na mti aina ya Mugariga ambao ni chakula cha Twiga.

No comments:

Post a Comment