Tuesday, 15 March 2011


SMZ yaitanulia misuli EU

Dk Mwinyihaji Makame Mwadini
SERIKALI ya Mapinduzi Zanzibar imezitahadharisha nchi za Umoja wa Ulaya (EU) kutoingilia mambo ya ndani ya Zanzibar.
Akifungua mafunzo kwa masheha mjini hapa Waziri Nchi Afisi ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mwinyihaji Makame Mwadini amesema pamoja na misaada wanayoitoa kwa zanzibar,inathamini mchango yao lakni isiwe sababu ya kuingilia utendaji wa serikali.
“Waandaaji wamenidokeza kwamba warsha hii imewezekana kutokana na uhisani wa watu wa Norway kupitia ubaozi wao hapa Tanzania. Norway kwa kuchangia maendeleo ya Zanzibar. Norway, pamoja na kuunga mkono juhudi za kuleta maridhiano Zanzibar. Tunapenda kwa dhati kabisa kuwashukuru na kuwaomba waendelee na moyo huo huo. Tunapenda kwa dhati kabisa kuwashukuru na kuwaomba waendelee na moyo huo huo. Lakini tunawaomba wasiingilie mambo ya utendaji wa serikali sisi kwa upande wetu tungependa kusisitiza kuwa tuna tuna nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa Zanzibar inakuwa na amani, utulivu na mshikamano” alisema Mwadini.
Hata hivyo Waziri huyo hajafafanua kauli yake hiyo wakati akifungua semina hiyo ya siku mbili ilifanyika jana kwa watendaji wa ngazi za serikali za mitaa (Masheha) katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Mjini Unguja.
Waziri Mwadini alisema serikali ya Norway imesaidia sana katika kuhakikisha maridhiano yanasimama hapa Zanzibar lakini licha ya msaada huo serikali ya Zanzibar haingependa kuona nchi hiyo ikiingilia katika masuala la utendaji wa kazi wa serikali yake.
Alisema serikali ya Zanzibar inataka kupiga hatua ya kimaendeleo ili iendane na kazi ya mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia duniani, ambapo yote hayo yatawezekana kama kila mtu popote alipo awe mtendaji wa serikali au anayefanya shughuli zake binafsi atatimiza wajibu wake.
Waziri licha ya kuwa hajaweka wazi kwa namna gani Norway wameingilia serikali ya Zanzibar lakini alisema kwamba wanashukuru kwa kupata msaada wa mambo mbali mbali kuoka serikali hiyo ambayo imekuwa ikiendelea kuisaidia Zanzibar katika masuala mbali mbali ikiwemo ya kijamii na kisiasa.
Akiwageukia watendaji wa serikali Waziri huyo amewataka Masheha kufanya kazi chini ya misingi ya mabadiliko ya sheria ya yalioamuliwa na wananchi ambayo yameweka mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa hapa Zanzibar.
Kwa muda mrefu mashaha masheha wamekuwa wakionekana maadui na wananchi kutokana na kufanya kazi kunakodaiwa kwa ugaguzi wa kisiasa ambapo kwa kiasi kikubwa wananchi wanawalalamikia kujikweza pande wa Chama Cha Mapinduzi na kuwadhalilisha wapinzani katika maeneo yao huku mashaha nao wakiata tabu kuishi katika baadhi ya mitaa kutokana na na kulipiziwa visasi vya kupigwa na kuchomewa nyumba zao moto.
Waziri Mwadini alisema masheha ni lazima wajifunze na waendelee kufanya kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo chini ya sheria mpya zilizoleta mabadiliko ya siasa za maridhiano na serikali ya umoja wa kitaifa.
Alisema mafanikio ya kiutendaji katika ngazi za shehia kwenye mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa yanategemea kwa kiasi kikubwa ufanisi wa masheha katika maeneo yao na kuwataka waishi na jamii kwa vizuri bila ya kuwepo na migombano kwa kuwa wao ni watendaji wa serikali na sio wanasiasa.
Waziri Makame alifahamisha kuwa masheha ni kiungo kikubwa baina ya serikali na wananchi walio katika ngazi za chini ambazo ni shehia hivyo wana wajibu wa kufanya kazi zao za kiutendaji kwa mujibu wa sheria zilizowekwa na serikali yao.
Aidha alisema ni jukumu la masheha kutokujishughulisha na mambo ya siasa wajifunze katika kufanya kazi zao kwa mustakabali wa mageuzi yaliyopo hivi sasa ya kisiasa na waache tabia ya kujiingiza katika siasa ambazo zitarejesha nyuma juhudi za serikali ya kuwaweka wananchi katika muelekeo wa umoja na mshikamano.
“Nchi hii imekumbwa na changamoto nyingi za siasa na msaada kutoka nje haukuweza kusaidia miafaka iliyosimamiwa na mataifa ya njeyote ilifeli hivi sasa tumeingia katika maridhiano Alhamdulillah sasa hatutaki kurudi tulipotoka tunataka kusonga mbele katika maelewano zaidi”.alisema Mwadini.
Hata hivyo alisema ni wajibu wa serikali pamoja na asasi nyingine kama Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) kuhakikisha kuwa zinatoa elimu zaidi juu ya maana ya serikali ya Umoja wa Kitaifa ni kwa nini iliundwa na changamoto inayoweza kuikabili hapo baadae ili wananchi wapate kujua muelekeo mzima wa serikali yao.
Waziri huyo alisema nchi ya Zanzibar kama ilivyo nchi nyengine imekumbwa na changamoto na matatizo mengi katika kipindi cha uhai wake lakini pamoja na changamoto zake ilijitahidi kukabiliana na matatizo yaliyojitokeza bila kutegemea msaada mkubwa kutoka nje jambo ambalo kila mmoja anawajibu wa kujua wapi wazanzibari wametoka na wapi wanaelekea .
“Lakini hata hivyo ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa nchi ya Norway kwa kuchangia maendeleo ya Zanzibar, Norway pamoja na nchi nyengine za umoja wa Ulaya zimekuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono juhudi za kuleta maridhiano Zanzibar”alisema.
Aidha alisema anapenda kwa dhati kabisa kuwashukuru watu na serikali ya Norway na kuwaomba waendelee na moyo huo huo wa kutoa misaada lakini akaonya kutoingilia mambo ya utendaji wa serikali.
kwa upande wake angependa kusisitiza kuwa serikali ya mapinduzi ina nia ya dhati ya kuhakikisha kuwa Zanzibar inakuwa na amani utulivu ma mshikamano.
Lengo ni Zanzibar kupiga hatua kubwa ya kimaendeleo ili iendane na kasi ya mabadiliko ya kisayanzi na kiteknolojia duniani,yote haya yanawezekana kama kila mtu popote alipo awe mtendaji wa serikali au anaefanya shughuli zake binafsi atatimiza wajibu wake.
Mkuu wa Idara ya siasa na utawala mwenyekiti mwenza Dr Benson bana alisema mafunzo yaliyotolewa na REDET yamewezesha kufanya utafiti wa shughuli mbali mbali za kisiasa na kiuchumi.
Alisema katika mafunzo hayo masheha watasaidia kubadilisha maarifa ya nafasi ya kiongozi katika ujenzi wa msingi ya utawala bora na vile vile watasaidia katika utendaji wa kazi za Serikali ya pamoja.
Warsha hiyo ya siku mbili iliyowashirikisha masheha mbali mbali imeandaliwa na chuo kikuu cha Dar es salam chini ya Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia Tanzania (REDET) kwa lengo la kuwapa somo la utendaji kazi chini ya mfumo wa serikali ya umoja wa kitaifa hapa Zanzibar.

No comments:

Post a Comment