Ripoti: Uzembe wa zahanati ulisababisha kifo cha mjamzito Na Beatrice Shayo
Sakata la mama aliyejifungua mapacha na kufariki katika zahanati ya COH ya Ukonga Mazizini, jijini Dar es Salaam, sasa limefika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo ndiyo itatoa hatma ya wauguzi waliosababisha kifo cha mwanamke huyo.Akizungumza na NIPASHE jana, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk Aisha Mahita, alisema ripoti hiyo wameshaiwasilisha wizarani, kwa Mkurugenzi na Mganga Mkuu wa Jiji.Alisema manispaa yake haina uwezo wa kuchukua hatua zozote zile kutokana na zahanati hiyo kuwa ni mali ya mtu binafsi pamoja na watumishi wake.Akizungumzia kilichobainika baada ya uchunguzi, alisema walichobaini ni kwamba zahanati hiyo haikutakiwa kuendelea kumshikilia mgonjwa huyo kutokana na kwamba tayari alishajifungua, hivyo walitakiwa kumpatia kibali cha kwenda katika hospitali kubwa ili apatiwe matibabu zaidi.“Zahanati ilitakiwa kumruhusu kuondoka pale tu alipomaliza kujifungua ili aende hospitali kubwa kwa ajili ya matibabu kwa kuwa alifika zahanati hapo kwa ajili ya dharura kwani tangu awali hakutakiwa kujifungulia hapo kutokana na kuwepo kwa ukosefu wa damu,” alisema.Alisema zahanati hiyo ilimshikilia mgonjwa huyo kwa siku mbili huku wakijua anakabiliwa na upungufu wa damu.Alisema kwa upande wa watumishi wa zahanati hiyo wameonekana kudai gharama kubwa kinyume na sheria kwani walitakiwa kumdai Sh. 30,000, lakini walimtoza mara mbili.Alisema suala hilo wameliangalia katika uchunguzi wao na kulielezea katika ripoti ambayo wameiwasilisha wizarani.Mahita alisema kuwa maamuzi yote yatatolewa na wizara hiyo kwa kupitia Baraza la Wauguzi kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.“Sijajua Wizara itaamua kitu gani kwani sisi tumeshawapatia ripoti yetu ila kama wataendelea na uchunguzi au la hilo mimi sijajua kwani wao ndio wenye maamuzi wa suala hilo,” alisema Mahita.Alisema tume hiyo ilishindwa kuwahoji ndugu wa marehemu kwa kuwa walikuwa wamesafiri kuelekea Dodoma kwa ajili ya mazishi.Tukio hilo lilitokea Februari 7, 2011 katika eneo hilo ambao mama huyo Sabela Mganga (31) alijifungua mapacha wawili katika zahanati hiyo na kuzuiliwa kwenda katika Hospitali ya Amana kwa madai kuwa hajamaliza deni analodaiwa.Baada ya kujifungua, daktari aliyekuwa zamu, Dk. Babu Machondela, alishauri mzazi huyo ahamishwe, lakini wauguzi walikaidi kwa madai kuwa hajamaliza deni lake.Hali ya mzazi huyo iliendelea kuwa mbaya na ndipo ndugu wa marehemu huyo walipoamua kumchukua kwa nguvu na kumpandisha katika gari kwa ajili ya kupelekwa Amana.Hata hivyo, muuguzi huyo aliwachukulia simu zao mbili zenye thamani ya Sh. 30,000.Mama huyo alifariki dunia wakati wanaanza safari ya kwenda Amana.Baada ya kupata taarifa hizo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala iliunda timu maalum kuchunguza chanzo cha kifo hicho na serikali iliifunga zahanati hiyo hadi kukamilika kwa uchunguzi.
Na Beatrice Shayo
Sakata la mama aliyejifungua mapacha na kufariki katika zahanati ya COH ya Ukonga Mazizini, jijini Dar es Salaam, sasa limefika Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo ndiyo itatoa hatma ya wauguzi waliosababisha kifo cha mwanamke huyo.
Akizungumza na NIPASHE jana, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilala, Dk Aisha Mahita, alisema ripoti hiyo wameshaiwasilisha wizarani, kwa Mkurugenzi na Mganga Mkuu wa Jiji.
Alisema manispaa yake haina uwezo wa kuchukua hatua zozote zile kutokana na zahanati hiyo kuwa ni mali ya mtu binafsi pamoja na watumishi wake.
Akizungumzia kilichobainika baada ya uchunguzi, alisema walichobaini ni kwamba zahanati hiyo haikutakiwa kuendelea kumshikilia mgonjwa huyo kutokana na kwamba tayari alishajifungua, hivyo walitakiwa kumpatia kibali cha kwenda katika hospitali kubwa ili apatiwe matibabu zaidi.
“Zahanati ilitakiwa kumruhusu kuondoka pale tu alipomaliza kujifungua ili aende hospitali kubwa kwa ajili ya matibabu kwa kuwa alifika zahanati hapo kwa ajili ya dharura kwani tangu awali hakutakiwa kujifungulia hapo kutokana na kuwepo kwa ukosefu wa damu,” alisema.
Alisema zahanati hiyo ilimshikilia mgonjwa huyo kwa siku mbili huku wakijua anakabiliwa na upungufu wa damu.
Alisema kwa upande wa watumishi wa zahanati hiyo wameonekana kudai gharama kubwa kinyume na sheria kwani walitakiwa kumdai Sh. 30,000, lakini walimtoza mara mbili.
Alisema suala hilo wameliangalia katika uchunguzi wao na kulielezea katika ripoti ambayo wameiwasilisha wizarani.
Mahita alisema kuwa maamuzi yote yatatolewa na wizara hiyo kwa kupitia Baraza la Wauguzi kwani wao ndio wenye maamuzi ya mwisho.
“Sijajua Wizara itaamua kitu gani kwani sisi tumeshawapatia ripoti yetu ila kama wataendelea na uchunguzi au la hilo mimi sijajua kwani wao ndio wenye maamuzi wa suala hilo,” alisema Mahita.
Alisema tume hiyo ilishindwa kuwahoji ndugu wa marehemu kwa kuwa walikuwa wamesafiri kuelekea Dodoma kwa ajili ya mazishi.
Tukio hilo lilitokea Februari 7, 2011 katika eneo hilo ambao mama huyo Sabela Mganga (31) alijifungua mapacha wawili katika zahanati hiyo na kuzuiliwa kwenda katika Hospitali ya Amana kwa madai kuwa hajamaliza deni analodaiwa.
Baada ya kujifungua, daktari aliyekuwa zamu, Dk. Babu Machondela, alishauri mzazi huyo ahamishwe, lakini wauguzi walikaidi kwa madai kuwa hajamaliza deni lake.
Hali ya mzazi huyo iliendelea kuwa mbaya na ndipo ndugu wa marehemu huyo walipoamua kumchukua kwa nguvu na kumpandisha katika gari kwa ajili ya kupelekwa Amana.Hata hivyo, muuguzi huyo aliwachukulia simu zao mbili zenye thamani ya Sh. 30,000.
Mama huyo alifariki dunia wakati wanaanza safari ya kwenda Amana.
Baada ya kupata taarifa hizo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala iliunda timu maalum kuchunguza chanzo cha kifo hicho na serikali iliifunga zahanati hiyo hadi kukamilika kwa uchunguzi.
No comments:
Post a Comment