Sunday, 6 March 2011

Mbunge wa Mji Mkongwe atoa vifaa

NaSalma Said
Mbunge wa Mji Mkongwe Mohammed Ibrahim Sanya akiwakabidhi wakaazi wa Jumba Maro vifaa vya ujenzi
MBUNGE wa Jimbo Mji Mkongwe Ibrahim Mohammed Sanya amesema viongozi wa majimbo wana nafasi kubwa ya kuwatimizia shida zao wananchi katika maeneo yao kutokana na kuwa serikali haiwezi kumaliza shida zote za wananchi.
Sanya amesema licha ya juhudi za serikali katika kutatua shida na kero za wananchi laini viongozi wanapaswa kuwa karibu sana na wananchi wa maeneo yao katika majimbo ili kujua shida za wananchi na kuzitekeleza kwa vitendo hasa zile ahadi zilizokuwa zikitolewa wakati wa kampeni za uchaguzi.
Akikabidhi vifaa vya ujenzi ikiwemo mabati 100 na mbao za kuezekea zenye thamani ya shilingi zaidi ya millioni 3 kwa ajili ya jumba la kihistori liitwalo Jumba Maro lililopo maeneo ya Mtendeni Mjini Zanzibar.
Sanya alisema utoaji wa vifaa hivyo ni kutekeleza ahadi zake kwa vitendo wakati wa kampeni ambapo yeye na mwakilishi wa jimbo hilo Ismail Jussa Ladhu waliahidi kutoa vifaa hivyo.
Sanya alisema zaidi ya shilingi milioni 11 zinahitajika kufanyia ukarabati wa jengo hilo ambalo ni linaishi familia 36 na linakabiliw ana uchakavu mkubwa ikiwa baadhi ya sehemu kuaza kuporomoka.
Hata hivyo amesema ukarabati huo wa Jumba Maro wa kufanyiwa matengenezo utafanywa kwa awamu hadi kufikia kumalizika matengenezo kwa vile linahitaji matengenezo makubwa na fedha zitakazotumika ni nyingi hivyo kila msaada utakapopatikana utatolewa ili kumalizwa ujenzi wake.
Nae Bw. Saidi Mdungi kiongozi wa kamati ya wakazi wa Jumba Maro alisema wamefarijika sana kufanyiwa matengenezo hayo kwani wao ni wakazi lakini wasingeliweza kufanya hivyo kutokana na hali ya unyonge waliyokuwa nayo.
Alisema ipo haja na viongozi wnegine kuiga mfano huo wa kusaidia na kutekeleza ahadi ziliztolewa ili kuwapungua mzigo wananchi wa gharama za matengenezo makubwa kama hayo ambapo familia zinazoishi humo zinakabliwa na matatizo mbali mbali ya kimaisha.
Kiongozi huyo alisema jumba hilo ni la kihistori la ni kongwe ambapo limejengwa zaidi ya karne moja ambalo awali walikuwa wakiishi wananchi wenye asili ya Asia (Wahindi) baadae walilikabidhi jumba hilo serikalini ambapo kwa sasa lipo chini ya Wakfu na Maliyaamana zanzibar ambalo linaishi familia masikini.
Jumba hilo lilitolewa na serikali mnamo mwaka 1994 na kupatiwa wananchi wa sehemu mbali mbali ambao hivi sasa wanaishi humo.
Msaada huo uliotolewa na mbunge na mwakilishi wa jimbo hilo ni moja kati ya misaada iliyokwisha kutolewa kuchimbwa visima na kuwapatia wanafunzi 26 udhamini wa kujiunga na vyuo mbali mbali nchini .

No comments:

Post a Comment