Maandamano Tripoli baada ya swala
Majeshi ya usalama ya Libya yanatumia mabomu ya kutoa machozi kutawanya mamia ya waandamanaji mitaani baada ya swala ya Ijumaa kwenye eneo ambapo Kanali Gaddafi amelidhibiti mjini Tripoli.
Mwandishi wa BBC katika kitongoji cha mashariki mwa Tajoura alisema waandamanaji walikuwa wakichoma moto bendera rasmi ya Libya.Makachero walidhibiti usalama eneo hilo, na wanaomtii Gaddafi wameweka vituo vya kukagulia magari.
Majeshi ya serikali yameanza mashambulio mapya kupitia anga kwenye maeneo ya waasi upande wa mashariki.
Uasi huo, ulioanza katikati ya mwezi Februari kuung'oa uongozi wa miaka 41 ya Kanali Gaddafi, unaonekana kugonga ukuta.
' Viashiria vya Al-Qaeda'
Mwandishi wa BBC Wyre Davies huko Tajoura alisema waandamanaji walikuwa mitaani wakitoa wito wa kuangushwa kwa serikali ya Gaddafi."Walirusha mabomu ya kutoa machozi," alisema mwandishi mmoja wa shirika la habari la Reuters aliyekuwa katika eneo la tukio. " Nilisikia milio ya risasi. Watu wanatawanyika."
Hali ilikuwa ya wasiwasi hapo awali wakati swala ya Ijumaa ilipoanza kwenye msikiti mkuu, huku makachero wakiwa nje.
Pia kulikuwa na wanajeshi wengi katika barabara kuu Tajoura, huku eneo wanalomtii Gaddafi wamekuwa wakikagua magari katika vituo mbalimbali.
Kumekuwa na ripoti ambazo hazijathibitishwa kuwa misikiti imefungwa na watu kukamatwa usiku, huku huduma za tovuti zikiwa zimefungwa.
No comments:
Post a Comment